Vimbwanga vya Fesibuku

NewDawnTz

JF-Expert Member
Nov 15, 2010
1,667
362
Hizi teknolojia zinaleta mambo.

Dogo anatumia jina la baba yake kwenye facebook yake matokeo yake mama mmoja wa makamo ambae nae ni memba wa facebook katika pitapita yake akakutana na facebook page na akamtumia dogo message na kumuuliza anaendeleaje na havbari za siku.

Dogo akamuuliza mazeri kuwa mbona sina kumbukumbu kama nakufahamu sawia basi mama akaanza kushuka nondo "mie niko Morogoro, hunikumbuki wako wa zamani tuliachana wakati wewe umeenda kambini ujedani na kunitupa moja kwa moja na baadhi ya story za wakati wanafurahia ujana wao na mengine mengi".

Dogo alipokuta ujumbe akaona haya makubwa sasa, ikabidi aweke wazi kuwa labda huyu mazaa alikuwa anamtafuta baba ake na kumpa mawasiliano nae...

Jamani hizi facebook tuwe nazo makini......

Weekend njema na facebook njema
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom