Kuna picha za hivyo vimini?
na vikuku navyo
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
MIGUU ya wabunge wanawake iliyoshiba na kupambwa na cheni maarufu kwa jina la vikuku ni miongoni mwa mambo yaliyokuwa vivutio katika mkusanyiko wa wabunge wakati wa kuapishwa mjini Dodoma, Amani limesheheni data.
Katika viwanja vya Bunge, mapema wiki iliyopita, wabunge wanawake kadhaa walionekana wakiwa wamejipamba na vikuku, hali iliyowafanya baadhi ya waheshimiwa wanaume kuikodolea macho miguu yao na kuijadili.
Wakikatiza mbele ya macho yake, Mbunge mmoja wa Chadema kutoka mkoani Mwanza ambaye Amani linamhifadhi jina alisikika akisema: Miguu hiyo bwana, kama mwanamke hana mguu wa bia hawezi kuvaa kikuku.
Mwenzake, kutoka CCM Unguja, Zanzibar akadakia: Kwanza kitampwaya. Maana kikuku chataka mguu hasa.
Amani lilibahatika kuongea na mbunge mmoja miongoni mwa waliokuwa wametinga urembo huo ambaye sharti lake la kwanza alisema si lazima kutumia jina lake gazetini kwa sasa, na alikuwa na haya ya kusema:
Kusema kweli kikuku ni urembo wa mwanamke kama ulivyo urembo mwingine, mfano bangili, hereni, cheni ya shingoni na vikorombwezo kibao, unajua mwanamke kujipamba, au siyo?
Akaongeza: Lakini si wanawake wote wanaovaa vikuku, kama ilivyo kwa cheni shingoni au bangili mkononi, sifa mojawapo ya kuvaa kikuku ni kuwa na mguu mnene kiasi.
Utafiti wa kina uliofanywa na Amani umejua kwamba, ni kweli wanawake wanaovaa vikuku ni wale waliojaliwa miguu yenye maumbile maarufu kama mguu wa bia ambapo huvaa ndani ya viatu vya kutumbukiza na vyenye visigino virefu.
Mbali na wabunge wavaa vikuku, lakini pia waheshimiwa wengine wanawake walioneshana umahiri wa kujipamba kwa suti za nguvu huku wakibeba mikoba yenye rangi sawa na suti hizo, hali iliyowafanya waonekane warembo zaidi kuliko wakati wa kampeni za ubunge zilizokwenda kwa takriban miezi miwili na nusu, katika Uchaguzi Mkuu wa 2010.