Vilio Misibani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vilio Misibani

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MaMkwe, Mar 14, 2010.

 1. M

  MaMkwe JF-Expert Member

  #1
  Mar 14, 2010
  Joined: Sep 5, 2007
  Messages: 284
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Inapotokea umekwenda msibani ukamkuta rafiki yako mnayefahamiana vizuri hadi kwenye familia zenu analia na kusaga meno kuliko hata mke/mume na ndugu wa marehemu wakati unajua kuwa hawakuwa na uhusiano wowote wa karibu utalichukuliaje suala hilo? Jamaa umeshawahi kwenda naye kwenye misiba mingi pamoja na ya ndugu zake wa karibu lakini hajawahi kuangua kilio kiasi hicho. Hata siku mama yake mzazi alipofariki mlikuwa wote lakini hakulia hivyo. Nimeshindwa kumuuliza kilichomsibu.
   
 2. vukani

  vukani JF-Expert Member

  #2
  Mar 14, 2010
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 245
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Inaonekanan huo msiba ulimgusa sana, kwa kawaida sisi binaadamu tunapoondokewa na mtu wa karibu na tuliyeshibana naye tunakuwa kama tumepoteza sehemu ya miili yetu.

  Kuna mengi yanayoweza kuwaliza watu katika misiba, kama vile ukaribu, utegemezi, (yaani ulikuwa unamtegemea sana marehemu au alikuahidi kukusaidia jambo fulani ambalo lingekuletea manufaa,) na mambo mengine kama hayo, mara nyingi watu wa aina hiyo wanahitaji ushauri nasaha maana wanakumbwa na kukata tamaa, kiasi kwamba wanaweza hata kuyumba katika shughuli zao.......
   
 3. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #3
  Mar 14, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  ipo namna hapo, nakumbuka miaka mwanzoni ya themanini nikiwa hata sijaanza drs la kwanza tulifiwa na babu mzaa baba, alikuja mama mmoja alilia sana tena sana, eti mh baba aheli ya mama kuliko mh baba, basi jinsi alivyokuwa analia tukatunga na kawimbo tehe. watu walishangaa lkn yakaisha. huwezi amini 30 yrs on yuleyule mama ananipigia simu eti anamtafuta my father amwonyeshe mwanawe, na huyo mtoto anaongea na mie anadai eti nawakumbuka utadhani alishawahi kutuona, bahati mbaya my both parents are not in this world anymore. so ukiona mtu analia sana lzm kuna jambo hapo
   
 4. M

  MaMkwe JF-Expert Member

  #4
  Mar 14, 2010
  Joined: Sep 5, 2007
  Messages: 284
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Bahati njema wote nawajua. Mliaji ni rafiki yangu tangu tukiwa watoto na marehemu ni jirani yangu. Ninachojua wanafahamiana wote kupitia kwangu na hawakuwa na ukaribu wowote ndiyo maana nimeshangaa sana nilipomuona jamaa analia kupita hata mume wa marehemu. Baadhi ya waombolezaji walidhani rafiki yangu ni mume au ndugu wa karibu wa marehemu. Mwanzoni nilidhani labda alikuwa amelewa lakini si hivyo kwani hata tulipokuwa makaburi alishindwa hata kusimama na ndipo hata watu wengine wakajua kuwa hawakuwa na uhusiano wa katibu na marehemu kwani mchungaji alimwita mume wa marehemu kuweka udongo na shada la maua kaburini.
   
 5. Lily Flower

  Lily Flower JF-Expert Member

  #5
  Mar 14, 2010
  Joined: Oct 16, 2009
  Messages: 2,555
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Kuna kitu unataka kusema au unataka wachangiaji mada waseme, labda walikuwa wana uhusiano wa kimapenzi kwa hiyo analia kwa uchungu kumpoteza mpendwa wake.
   
 6. Injinia

  Injinia JF-Expert Member

  #6
  Mar 14, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 850
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mambo mengi yanawezekana:
  - alikuwa na uhusiano ambao haukua wazi kwako
  - hicho kifo kimemkumbusha kitu, labda kifo cha mtu wake wa karibu
  - alikuwa anamdai marehemu
  - alikumbuka mambo yake yasiokuwa na uhusiano na huo msiba
   
 7. vukani

  vukani JF-Expert Member

  #7
  Mar 14, 2010
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 245
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35

  Hili nalo neno! yawezekana labda....
   
Loading...