Vilema wana haki gani katika jumuia yetu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vilema wana haki gani katika jumuia yetu?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Fundi Mchundo, Jan 7, 2008.

 1. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #1
  Jan 7, 2008
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Kwa wenzetu kuna kitu kinaitwa universal accesibility kwenye public spaces zote kuanzia vyombo vya usafiri( mabasi yanashuka ilikumwezesha mlemavu, na mama mwenye mtoto mchanga kwenye kigari) apande bila bughudha, majengo( milango ni mipana kuruhusu walemavu kupita, matumizi mbadala ya ngazi, kuwa na corridor pana n.k), barabarani ( traffic light zinatoa sauti kumruhusu kipofu kujua wakati gani anaweza kuvuka, nafasi maalum za kusimamisha magari walemavu n.k). Mtazamo huu haulengi tu kwenye kumfikisha mlemavu kwenye ghorofa za juu bali zinamrahisishia naye kuweza kutoka panapotokea ajali. Ni sheria nchi nyingi kuwa katika public spaces zote lazima pawe na vyoo kwa ajili ya walemavu na sehemu nyingine hata sehemu za kumbadilishia nepi mtoto mchanga. Haya yote yanawezekana na pamoja na kumtambua mlemavu kuwa sehemu muhimu ya jumuia inamruhusu naye kutoa mchango wake inavyopaswa.Mtu unajiulize je Hawkins angezaliwa bongo ingekuwaje? Bila shaka angeishia kubeba kibakuli posta kuomba msaada. Kwa nini kweli tunashindwa kuweka sheria zitakazompa haki sawa mlemavu kati yetu? Tusisahau vilevile hata sisi wengine tunapata ulemavu wakati tofauti wa maisha yetu ( wanawake wanapokuwa wajawazito si rahisi kupanda ngazi, tunapokuwa watu wazima vilevilen.k). Hivi mlemavu atatambaa mpaka lini ili kuweza kumuona mkuu aliyeghorofa ya sita kwenye penthouse? Najua si wote wenye baiskeli au vigari kama ilivyo kwa wenzetu lakini inabidi tuanze mahali. Huyu mama angesusia mkutano.Pengine tungeanza kumsikiliza. Na kumuona.

  Naomba title ibadilishwe isome walemavu badala ya vilema!
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Jan 7, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Hili ni mojawapo ya matatizo ambayo yanatusumbua sana hasa nyumbani. Barabara za kupitia, milango ya majengo n.k Mfano wa hapo juu wa huyuo Mbunge ni muhimu sana kueleweka; walemavu wengi mara nyingi wanajikuta kama "usumbufu" kwa sababu sehemu nyingi zina vizuizi vingi vinavyofanya maisha ambayo tayari yana kizuizi kuwa magumu zaidi... Mtu ambaye anatembea kwa shida kumuongezea ngazi ni kumtesa!
   
 3. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #3
  Jan 7, 2008
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  1. Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inayoratibu mambo ya walemavu- ina ghorofa 4- na hakuna hata lift pamoja na ukarabati mkubwa uliofanyika hivi karibuni!

  2. Kwa nini isipitishwe sheria kuwa majengo yote haswa ofisi za serikali ziwe zinaweza kufikika na watu wote?

  3. Kipimo cha ustaarabu wa watu hupimwa kwa jinsi jamii inavyojali na kuhudumia walemavu!

  4. Hivi huko Wilayani ni Idara ipi inaangalia mahitaji wa walemavu? Au ndo zimeachiwa taasisi za dini- na wanafamilia?

  5. Juzi tu nimesikia Maalbino wanauwa kwa imani za kishirikina! JK amekemea ktk hotuba- je kukemea tu inatosha?
   
 4. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #4
  Jan 7, 2008
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Si maalbino tu! Hata vilema wamewahi kuuawa. Kama nakumbuka vizuri ni hivi karibuni tu mwalimu mmoja huko Arusha alishitakiwa kwa kumuua mtoto wake mchanga aliyezaliwa na ulemavu.
   
 5. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #5
  Jan 8, 2008
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Moja ya vitu ambavyo naamini vinaturudisha nyuma kimaendeleo kama jamii ni hii apathy yetu kuhusu masuala kama haya. Hii apathy inaendelea mpaka kwenye masuala ya mazingira, elimu n.k. Ukiangalia watu walio'bother' kuisoma thread hii na wale ambao wanasoma ishu nyingine zinaonyesha wazi priorities zetu. Jamii yakitanzania inapenda majibu rahisi yasiyowalazimisha kujiangalia kwenye kioo. Tumegeuza siasa kuwa kama mchezo wa mpira. Kwa bahati mbaya, hatutaweza kujikomboa kama jamii bila kumjali yule aliye mnyonge katika sisi. Kwa mtaji huu, hawa walemavu watazidi kusota maana jamii yetu haiwatambui na haioni umuhimu wao. Asante Mzee MwanaKijiji na Mzalendo kwa kuonyesha concern zenu.
   
 6. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #6
  Jan 8, 2008
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Fundi Mchundo,

  Mimi pia niliwahi kuweka hii hoja- siku za nyuma- na kupata wachangiaji wachache including akina Mamalao n.k! Sema watu JF wapo ktk siasa zaidi-- sii kwamba wanaJF hawawapendi walemavu!

  Ila kwangu binafsi kama binadamu huwa nawahurumia sana wenye ulemavu- sema tu sina jinsi ya kuwasaidia- huwa nawatetea siku zote!

  Watu wanashindwa tu kutambua kuwa hakuna mtu anachagua kuwa mlemavu- hii inatokea tu- na hata leo hii mtu uu mzima- ukipata ajali au ugonjwa pia unaweza kuwa mlemavu!

  Mimi maalbino ni rafiki zangu sana- yaani hata kama naendesha gari- nikikutana neo lazima nishuke, niwashike mkono na kuwasalimia kwa upendo! Yaani huwa wanfurahi sana.. na kama nina pesa tunakula nao lunch wote ni furaha tu!

  Siku zote nawasihi Watz kuwa na attitude positive towards walemavu- na kama kuna nafasi ktk kazi kuwapa upendeleo- disability is not inability!

  Pia nakushukuru Fundi Mchondo for bringing this matter ktk hii thread!
   
 7. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #7
  Jan 8, 2008
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Nimekusikia Mkuu Mzalendo. Ingawa ningependa kuamini kuwa jamii yetu ina mapenzi kwa walemavu nasita kufanya hivyo. Wengi katika jamii yetu wanaona walemavu kama mzigo( wengine huoona kuwa ni laana kutoka kwa mwenyezi) na wasingependa kukumbushwa kuwepo kwao. Mtazamo huu vilevile upo katika tunavyowaona wenye ukimwi. Ni aghalabu mtu kuutangazia umma kuwa ndugu yake anaumwa ugonjwa huo na pale mwenyezi anapomchukua magonjwa mbadala yanatafutwa kuelezea kifo chake. Isingekuwa aibu wengi wangewakimbia walioathirika. Ukija kwa walemavu hali kama hiyo nayo imeenea. Ni wachache wanaoona neema ya mtoto mlevu ( hapa najumuisha hata wale wenye matatizo ya akili) na ingewezekana wengi wangejitua mzigo huu. Ukiangalie vilevile tunavyowachukulia wanyama. Angalia tunavyowatendea mbwa wetu, hatuwakemei watoto wetu wanapozunguka na manati kuuwa paka, tunawafunga tumbili minyororo shingoni na kuwatumia kututumbuiza. Hapana, Mzalendo, jamii yetu neno empathy kwa wale walio wanyonge iliondoka zamani.
   
 8. M

  Mama Lao JF-Expert Member

  #8
  Jan 9, 2008
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 238
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tafadhalini sana wana JF...neno vilema si sahihi hapa tutumie, watu wenye ulemavu. Ni muhimu kuonyesha kuwa hawa ni binadamu wenzetu! Tuanze sasa kwa sababu wengine hufikiri watu wenye ulemavu si watu!
  Nakusihi pia muanzisha thread urekebishe. Hata kuku anaweza kuwa kilema!. Lugha tunazotumia ku address watu wenye ulemavu saa nyingine huwa stigmatize zaidi!
   
 9. M

  Mama Lao JF-Expert Member

  #9
  Jan 9, 2008
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 238
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wandugu hatuhitaji "kuwahurumia" walemavu. wanchohitaji watu wenye ulemavu ni sera bora na kuwezeshwa, mfumo wa jamii utakaosimamia na kulinda haki zao, fursa zitakazowawezesha na wao kuchangia ktk maendeleo ya taifa.
  Hii "charity model" sio sahihi.....
   
 10. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #10
  Jan 9, 2008
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Mama Lao, ukisoma vizuri post yangu ya kwanza,nimetumia neno mlemavu wakati wote na mwishoni niliomba msaada kubadilisha title. Nawaomba radhi wale wote ambao matumizi yangu ya neno vilema limewakera. Nitajaribu tena kuirekebisha. Lakini tukiondoka kwenye semantics nadhani hoja ya msingi ni namna sisi kama jamii tunavyowaona na kuwatendea wale wenye ulemavu. Je tumefika mahali ambapo jamii inaona mlemavu anastahili haki sawa na wale wasio na ulemavu? Kama si hivyo, nini tunapaswa kufanywa ili wapate hiyo haki? Pamoja na kutambua kuwa ni muhimu tutumie jina sahihi ni hatua gani 'concrete' ambazo tunaweza kufanya?
   
 11. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #11
  Jan 9, 2008
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Nimejaribu tena kubadilisha title nimeshindwa. Ingawa kweli walemavu wanachohitaji ni 'acceptance' na sio 'tolerance' hauoni kuwa huu huruma ni heri kuliko pale tulipo sasa kama jamii? Nadhani utumwa ulianza kupigwa vita na wale waliowahurumia watumwa kwanza na baadaye ndipo ikaja acceptance ya kuwa watu weusi nao ni watu. Ningependa wote tuweze kuruka kwenda kwenye acceptance( naamini Mzalendo anawakubali wenye ulemavu kama watu wenye haki sawa na yeye) lakini kwa sasa hata hiyo huruma nitaikubali.
   
 12. M

  Mama Lao JF-Expert Member

  #12
  Jan 9, 2008
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 238
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nope....sikubaliani na wewe kuhusu huruma. Hii inaitwa charity model, kwamba watu wenye ulemavu ni "wakuhurumiwa". Ndio maana unaona kazi hii ilichwa kwa philanthropist..makanisa etc. Model hii inaendeleza "umaskini" kwa wenye ulemavu kwamba they are people to be pitied!
  Tuwape nafasi...
   
 13. Sanda Matuta

  Sanda Matuta JF-Expert Member

  #13
  Jan 9, 2008
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 950
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Kumbukeni siasa za Kitanzania ni kama mipasho (muziki wa Taaraabu)
  Wengi wetu tunapenda udaku na kuchafuliana majina kiasi cha kwamba tunakua blind kwenye mambo ya muhimu yana yotugusa sisi kama wana jamii kama swala hili.
  Naomba nieleweke kwamba hata siasa inatugusa ila kama kuna jambo la muhimu zaidi kama hili la kupaswa kukemea basi tufanye hivyo.
   
 14. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #14
  Jan 9, 2008
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Kwa hiyo mama Lao unaona kuliko kuhurumiwa heri waachwe kama walivyo mpaka jamii itakapofikia mahali pa kuwakubali? Si heri tujenge kwenye hiyo huruma, tuibadili kuwa kuwaku bali? Si hawa hawa wenye huruma ndiyo wanaopandikiza mbegu kwa wenye ulemavu kuweza kusimama na kudai utambulizi kama sehemu ya jamii?
   
 15. M

  Mama Lao JF-Expert Member

  #15
  Jan 9, 2008
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 238
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Admin tafadhali namba ubadilishe title ya FM! I cannot stand this ...
  Tafadhali ondoa neno "vilema" weka "watu wenye ulemavu". Please.
   
 16. M

  Mama Lao JF-Expert Member

  #16
  Jan 9, 2008
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 238
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  FM huruma haitajenga...sanasana itaendelea kuongeza watu wenye ulemavu wenye vibaba wakiomba kama unavyoona pale Salender!
  Kinachohitajika ni
  Sera..zinazolinda haki za watu wenye ulemavu na kuwapa fursa mbalimbali kama huduma za utengemao, elimu, ajira etc.
  Mfano wale wenye baiskeli maalum kundi kama la watu 10 kwanini waendelee kuwa ombaomba pale Salender? Je kwa mfano wangepewa mkopo na kazi ya kuuza vocha za simu...si wange survive? au wangepatiwa eneo maalum la kufanya biashara ambalo liko accessible kwao na kwetu ...
   
 17. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #17
  Jan 9, 2008
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
   
 18. M

  Mama Lao JF-Expert Member

  #18
  Jan 24, 2008
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 238
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [​IMG]
  (Picha kwa hisani ya Michuzi spot)
  Naona Mh Muhidhihir yeye kabahatika kupata mkono bandia ambao kwa hesabu za haraka si chini ya 20million. Sasa je hao kina wenzangu na mie walioko kijijini.....huwa wanamudu vipi maisha????????????????
  Hii pia inaleta changamoto kwa viongozi wetu kwamba "hujafa hujaumbika" mtu yeyote anaweza kuwa mlemavu saa yoyote. Boresheni mazingira ya watu wenye ulemavu kupatiwa huduma bora. Hongera sana kwa kupata nyenzo na karibu sana kwenye kundi la watu wenye ulemavu!
   
 19. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #19
  Jan 24, 2008
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Mamalao,

  Point nzito sana- hakuna immunity mtu yoyote aweza kupata ulemavu saa yoyote!

  Hope Mudhhir sasa atatetea haki za walemavu bungeni kulipo hapo awali, the wearer of shoes knows where it hurts most!
   
Loading...