Vile mashauzi yalivyoniumbua

Ni mwaka huu mwanzoni alipita mdada tulikuwa tumesimama sehemu na washkaji kama 4 hivi tunapiga story akapita mdada huyo mrembo huyo sijui kama wengine walimuona vizuri wakakaa kimya sijui mimi nilimuona juu mpaka chini jicho likagota kwenye zipu mrembo wa watu hajafunga zipu

Nikakamuita Dada akakauka lengo langu nimwambie afunge zipu coz anapoenda ni mjini amevaa chup ya pink na zipu imeachia kabisa kila kiasi kwamba kila anaekutana naye lazima ataona

Dada akawa busy na simu yake nikasema huyu ngoja asogee hatua chache mbele nimwambie kwa sauti

Kama hatua tano mbele kulikuwa na wamama wanakuja nikwambia wewe DADA TUMEKUITA UMEKATAA ZIPU IKO WAZI HAUJAFUNGA aibu yake ilikuwa siyo Nchi hii Dada alitaka kurudi alikotoka aliruka huyo.
 

Ulikuwa unanilia timing tu au siyo!
Dah bahati nzuri hujaniita lile jina unaloandikaga kule selfika
Nilikua nakuangalia tu nikajisemea dawa yake ipo jikoni mtoto mdogo huyu 🤣🤣

Leo dadako lazima akuchape 'kibao or two'
 
Ila hizi mambo zetu wadada za kuignore na kuringa tukiitwa barabarani na watu tusiowafahamu sometime sio kabisa

Imewahi nitokea nakumbuka enzi za chuo hiyo siku weekend tumetoka hostel na shosti yangu lengo tukatafute msusi ila tukaenda mtaa ambao hatuufahamu vizuri.

Sasa tuko busy tunabahatisha njia tukapita sehemu wakaka wamekaa kama wa4 hivi na ilikua kama garage hizi za mtaani tu ambazo sio rasmi wakawa wanatuita aah tukakaza huku tunaambiana hao vipi kutuita ita hamna kuitika! Lahaulaaa kumbe tulipokua tunaelekea mbele hakuna njia inatoka hiyo njia ilikua inaenda ishia nyumbani kwa mtu! Kufika mbele hatuoni njia yaan kwanza tulijikuta tunacheka na aibuu maana tutapita vipi pale na tumegoma kupokea salamu zao.

Ikabidi turudi na kukutana nao tena tukawasalimia kwa aibu yaan walitupa maneno kibao tukajikaza na kuwauliza njia wakatuelekeza tukaendelea na safari yetu.
Kiukweli tangia siku hiyo kiburi barabarani niliweka pembeni salamu za watu naitikia vema na kwa adabu.

hii jamaa yangu askari ffu,yuko bank analinda mcity pale sasa amekaa karibu na ATM,akaja sister du wa haja kampita mlangoni kimya yeye huyoo kwenye ATM,kaingia ndani huko sekunde kadhaa anatoka,afande ATM hazitoi hela eeeh!!!!jamaa lilimtoka zima zima.wee **** nini ndio unaniona saa hizi???
dada aliondoka anatamani kukimbia.
 
Nilikua nakuangalia tu nikajisemea dawa yake ipo jikoni mtoto mdogo huyu

Leo dadako lazima akuchape 'kibao or two'
Dah
Kumbe huwa unaona upupu wangu???
Umeniotea leo.

Nilivyoona umeanza kuwataja akina bia yetu nikawaza tu kwamba sijui kama nitasalimika.
Nikapita kimya,kumbe umenipangia leo


Nasubiri shambulizi lingine kutoka kwako,
Sijui litahusu nini Mungu wangu.

...............
Pep unataka kunigombanisha na dada yangu mzuri?
 
  • Kicheko
Reactions: Pep
Kuna mshkaji wangu anaishi Kawe. Nishawahi kuishi kwao kwa zaidi ya mieizi miwili kwahiyo nazijua njia za maeneo hayo vizuri tu. Kisha nikaondoka Dar kwa zaidi ya mwaka nilivyorudi tena Dar nikawa naishi kwetu sasa nikapanga kwenda kumtembelea mshkaji.

Siku imefika nikafunga safari nikaelekea Kawe. Kipindi hicho wimbo maarufu ni Prakatatumba wa Cabo Snoop na nilivaa kama mshkaji. Supra, jinzi chupa (enzi hizo haziitwi model), halafu jinzi inaingizwa ndani ya supra na fulana nikachomekea.

Nikafika sehemu ambayo ina kibaraza natakiwa niambae kufuata kibaraza kisha nikutane na kichochoro halafu hiko kichochoro kimekunja kulia halafu hapo ndo kinitoe kwenye njia pana ndiyo nikute uwanja anapokaa mshkaji.

Kwenye kibaraza nikakuta mabinti na wanawake wanasukana, nikawapita mwendo mdundo. Nikaingia kichochoroni nikakunja kulia nakuta kumezibwa kwa michongoma. Nikafikiria mwendo niliowapita pale nikaona kurudi siyo kweli na nilivyovaa itakua aibu.

Nikaparamia ile michongoma.

Kumbe katikati waliweka na miti ili michongoma isimame.

Nikakomaa. No backing down hapa.

Paramia na teke kwa mara ya pili pakalegea. Nikajipenyeza penyeza nikafanikiwa kupita.

Bwana wee nilijichana chana na ile miiba maeneo ya usoni na mgongoni. Fulana imechafuka kwa vumbi.

Did I learn anything? No. Am the same nigga who is shy kusalimia kundi la wamama.

nadhani hata wao walibaki wanajiuliza,huyu cabo snoop kapotelea wapi
 
Dah
Kumbe huwa unaona upupu wangu???
Umeniotea leo.

Nilivyoona umeanza kuwataja akina bia yetu nikawaza tu kwamba sijui kama nitasalimika.
Nikapita kimya,kumbe umenipangia leo


Nasubiri shambulizi lingine kutoka kwako,
Sijui litahusu nini Mungu wangu.

...............
Pep unataka kunigombanisha na dada yangu mzuri?
Hapana, huwa huongea upupu mama mtumishi

Huwa unakua na hoja ambazo huwa zina make sense.

Bia yetu na wenzake wao wana shida moja tu, huwa hawakubali mawazo mbadala. Halafu hawanaga hoja ku back up hoja zao.

Hufanani nao walau hata kwa mbali.

_______________
Dadako lazima akurarue vibao kadhaa, 'najivoluntia' kusimamia hilo 🤣🤣
 
Hapana, huwa huongea upupu mama mtumishi

Huwa unakua na hoja ambazo huwa zina make sense.

Bia yetu na wenzake wao wana shida moja tu, huwa hawakubali mawazo mbadala. Halafu hawanaga hoja ku back up hoja zao.

Hufanani nao walau hata kwa mbali.

_______________
Dadako lazima akurarue vibao kadhaa, 'najivoluntia' kusimamia hilo

Mimi huyu tangu lini nikawa na hoja?
Asante baba umefanikiwa kunipaka mafuta kwa mgongo wa chupa.


...............
Kumbe haunipendi eeeh!?!
Wataka nipigwe na dada jamani
 
  • Kicheko
Reactions: Pep

Mimi huyu tangu lini nikawa na hoja?
Asante baba umefanikiwa kunipaka mafuta kwa mgongo wa chupa.


...............
Kumbe haunipendi eeeh!?!
Wataka nipigwe na dada jamani
Nasema ukweli, si unajua msemakweli ni mpenzi wa nani?

______

Nampenda mtumishi mwenzangu ndo maana nataka dadake amnyooshe 🤣🤣
 
Wanaume kweli wanasumbua ila nikipita sehemu hata salamu huwa najibu japo najua wengine wanasalimi kwa sababu zao, hata barabarani mtu akinisimamisha huwa namsikiliza ndo naendelea na safari. Nilijifunza hii kwamba sio kila anaekuongelesha anataka kukutongoza wengine ni watu wema wanataka kukusaidia jambo so ni bora umsikilize halafu uamue lakini sio kumpotezea mtu.

Nilishawahi simamishwa na mkaka akaniambia zipu ya jeans iko wazi. Nikamshukuru nikafunga. Sasa ningejifanya mrembo mimi ndo mrembo sana nisimsikilize ningeumbuka vibaya sana maana nilipokua naenda kuna watu wengi.

Juzi juzi nimeenda kwenye ATM askari akaniita moyoni nikasema huyu hana lolote ila wacha tu nimsikilize, akaniambia kuwa makini dada wanaiba simu maeneo haya. Hata hakunitongoza baba wa watu nikasema ningekua wale wanawake washamba wa kuvimbia wanaume ningeibiwa angeishia kunicheka tu.
 
hii jamaa yangu askari ffu,yuko bank analinda mcity pale sasa amekaa karibu na ATM,akaja sister du wa haja kampita mlangoni kimya yeye huyoo kwenye ATM,kaingia ndani huko sekunde kadhaa anatoka,afande ATM hazitoi hela eeeh!!!!jamaa lilimtoka zima zima.wee **** nini ndio unaniona saa hizi???
dada aliondoka anatamani kukimbia.
Tabia ya kupita watu bila kusalimia sio kabisa
 
Tulienda kwenye harusi,muda wa kufungua champagne Mc akatangaza anataka watu nane watu hakuna nikasema ngoja niende na mimi.

Jamani wote champagne zao zilifunguka faster mimi sasa nilijikuta mwenyewe mbele watu wananiangalia na chupa haijafunguka.Niliitikisa ile chupa kama chibuku.

Mpaka kuja kufunguka watu walishachoka kuniangalia,sherehe niliiona chungu sikunyanyuka tena mpaka muda wa kuondoka.

 

Similar Discussions

Back
Top Bottom