Kuna mshkaji wangu anaishi Kawe. Nishawahi kuishi kwao kwa zaidi ya mieizi miwili kwahiyo nazijua njia za maeneo hayo vizuri tu. Kisha nikaondoka Dar kwa zaidi ya mwaka nilivyorudi tena Dar nikawa naishi kwetu sasa nikapanga kwenda kumtembelea mshkaji.
Siku imefika nikafunga safari nikaelekea Kawe. Kipindi hicho wimbo maarufu ni Prakatatumba wa Cabo Snoop na nilivaa kama mshkaji. Supra, jinzi chupa (enzi hizo haziitwi model), halafu jinzi inaingizwa ndani ya supra na fulana nikachomekea.
Nikafika sehemu ambayo ina kibaraza natakiwa niambae kufuata kibaraza kisha nikutane na kichochoro halafu hiko kichochoro kimekunja kulia halafu hapo ndo kinitoe kwenye njia pana ndiyo nikute uwanja anapokaa mshkaji.
Kwenye kibaraza nikakuta mabinti na wanawake wanasukana, nikawapita mwendo mdundo. Nikaingia kichochoroni nikakunja kulia nakuta kumezibwa kwa michongoma. Nikafikiria mwendo niliowapita pale nikaona kurudi siyo kweli na nilivyovaa itakua aibu.
Nikaparamia ile michongoma.
Kumbe katikati waliweka na miti ili michongoma isimame.
Nikakomaa. No backing down hapa.
Paramia na teke kwa mara ya pili pakalegea. Nikajipenyeza penyeza nikafanikiwa kupita.
Bwana wee nilijichana chana na ile miiba maeneo ya usoni na mgongoni. Fulana imechafuka kwa vumbi.
Did I learn anything? No. Am the same nigga who is shy kusalimia kundi la wamama.