BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,789
- 288,015
Sidhani kama kwa kutumia sanduku la kura kuwatimua haiwezekani. Tukiwakataa katakata kwenye sanduku la kura itawafanya hata wao wajishtukie kuiba kura. Mara nyingi kura huibwa kama idadi haijapishana sana.
Kama hilo likishindikana, basi tunaweza na sisi kuwa Orange Revolution yetu kama ilivyokuwa kule Ukraine. Kama hujui Orange Revolution ni nini jaribu ku google na utaelewa ilikuwa ni nini na faida zake zilikuwaje. Nakwambia massive civil disobedience, passive resistance, sit-ins, na migomo mingine inafanya kazi. Ilifanya kazi Marekani wakati wa civil rights, ilifanya kazi Ukraine na kwingineko duniani na nina imani itafanya kazi Tanzania. Tatizo wengi wetu hatuko tayari kulipa gharama. Tuko waoga.
Labda hilo la kufanya Orange Revolution ndilo litakalofanikisha kuiondoa CCM madarakani, lakini kuwatoa CCM madarakani kwa kutumia kura kwa maoni yangu haitawezekana kabisa. Watawanyanyasa wanachama na viongozi wa vyama vya upinzani kwa kila namna wakati wa kampeni tena kwa kutumia vyombo vya dola kama FFU, polisi na hata Wanajeshi. Pale ambapo wanajua kuna uwezekano wa kushindwa wataweka mikakati mikali sana ya wizi wa kura