Vikwazo vya maendeleo katika nchi yetu ni... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vikwazo vya maendeleo katika nchi yetu ni...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by WomanOfSubstance, Mar 20, 2010.

 1. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #1
  Mar 20, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Jamii inaongozwa na ujumla wa mifumo na taratibu zinazoathiriwa na belief systems ( imani za kidini, mila, desturi, haki na uhuru wa kujieleza au kudai haki etc).

  Nchi nyingi hasa za Kiafrika zimeshikilia sana imani ( za kidini au kimila) kama nguzo za jamii zao na kuwa na kiwango kidogo cha uhuru wa mawazo au hata kudai haki mbalimbali..nchi hizi nyingi hujikuta zina maendeleo hafifu. Nchi kama Sweden au Uholanzi ambazo hutoa uhuru mwingi kwa wananchi wake..kuna haki za watoto na wanawake za kiwango cha kutisha - zimepiga hatua kubwa kimaendeleo.....

  Kwa maneno mengine... kadiri jamii inavyoshikilia mila ( traditions) ndivyo kiwango cha maendeleo kinavyokuwa chini..

  Je, ina maana mila, desturi au hata imani za kidini hudumaza maendeleo?
   
 2. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #2
  Mar 20, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Mila ,desturi na imani ni identity ya jamii

  Mila yoyote , desturi yoyote au dini yoyote inayopandikizwa kwenye jamii bila kuwa na chimbuko kwenye jamii yenyewe ni kurudi nyuma kimaendeleo.

  Hatuwezi kuendeleea kwa kuambiwa tukataze ukeketaji na wakati huo huo tupandikize desturi ya kukubali ushoga kwenye jamii zetu.

  Kwa hiyo kuangalizia mila na desturi za za waholanzi au wasweeden sio suluhisho.
   
 3. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #3
  Mar 20, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,605
  Likes Received: 6,174
  Trophy Points: 280
  Kwanza usichanganye traditions fulani katika tamaduni za wenzetu ambazo labda- labda- zinaweza kuwa objectionable, na positive trends za freedom zilizopo katika cultures hizo. Ni sawasawa na kupima mito ya continent inamwaga maji upande gani kwa kutumia kichuguu cha uwani kwako. Unakosa statistician wanachokiita "sample space" ya kutosha ku lend credibility to your observations.

  As long as tunaongea dini kupandikizwa katika jamii, hatuwezi kuacha kutaja imani ya mungu, hususan mungu wa Judeo-Christian traditions, lakini pia idea nzima ya ku submit kwa authority ya kiungu kuwa kikwazo kikubwa cha maendeleo. Huko Sweden si kama wanalazimisha watu kuwa mashoga, wanatoa uhuru tu kwa mtu anayetaka kuwa shoga awe shoga, sasa kama wewe unaona ku impose views zako kwa wenzako ndiyo sawa utajionyesha jinsi gani uko medieval.

  Halafu huu uongo kwamba Africa hakuna mashoga na habari za mashoga zinatoka west ni delusion, kuna habari za ushoga afrika zilizokuwa documented as far back as the original egyptians. Kwa hiyo tuache kudanganyana kwamba ushoga ni kitu foreign africa.Tatizo letu wafrica mambo tunayaficha under the carpet halafu tunajidai kama hayapo, wenzetu wanayaanika wazi, tunafikiri kwamba kwetu hayapo.

  Ukishaanza kuamini kwamba kuna huyu mungu kakaa juu anaangalia mambo yote, unaacha kuchukua personal responsibility, unaanza kuomba na kusali zaidi kuliko ku reason na kufanya kazi.

  Watu wanakufa migodini Arusha rais anasema ni "mapenzi ya mungu". Kumbe tungekuwa na safety laws zilizo proactive na teknolojia za kutosha tusingekuwa na haja ya kumsingizia huyu non-existent godhead.

  Mafisadi wanatanua, watu wanajifariji kwamba "watakiona cha mtema kuni siku ya hukumu" etc etc, mifano mingi.

  Guess what, Waswahili walisema "Dua la kuku halimpati mwewe" hamna siku ya hukumu, mungu wala shetani, mbingu wala moto in the traditional sense.

  Siku ya hukumu ni leo, mungu na shetani ni wewe kutegemea na matendo yako at any moment (unaweza kutenda kiungu au kishetani kwa maana ya vizuri au vibaya, lakini hakuna entity ya mungu huyu wala shetani) na mbingu na moto viko hapa hapa duniani.

  Ndiyo maana Wu wanakwambia,

  What do you believe in, heaven or hell.
  We don't believe in heaven cause we're living in hell.
   
 4. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #4
  Mar 20, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135

  yaani mkuu, umenikuna hadi natoka unga hapa...

  Kweli tusisingizie mila na desturi bali tuache utani katika kusimamia rasilimali zetu na kuweka mipango madhubuti ya maendeleo............... ukeketaji wetu hadi kwa vyovyote vile ni bora mara elfu nyingi ukilinganisa na ushoga na usagaji wanaohalalisha huko kwao na kuidhinishwa kisheria....

  kuna watu wanachanganya mambo wanachukulia uliberari mojakwa moja kuwa ni maendeleo bila kuzingatia mmomonyoko uliomo ndani yake...... kumbe hata mazingira hayahayaha tuliyomo tukifanya something tangible kitakuwa tu bila kukubali utumwa wa magharibi.....

  Lets put this way, ukeketwe usikeketwe, ukisonga ugali vizuri utaiva tu.......... so kukeketa ama kutokeketa can never be a precedent...........
   
 5. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #5
  Mar 20, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  hee!!!!!!!! ndivyo wewe ulivyoelewa mwenzetu????????? pole sana............. msiwe mnavamia mambo kabla hajayaelewa vizuri.....................
   
 6. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #6
  Mar 20, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Unajua hata hizi dini mbili kuu tulizonzo zilipandikizwa kwenye jamii zetu. asili za jamii zetu ku commmunicate na mungu tuliambiwa kuwa ni kuabudu miungu na tukaamini. No wonder hatuendelei sababu tunakopi utamaduni,mila ,a imani zao
   
 7. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #7
  Mar 20, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Mungu hakumuumba Mwanadamu awe Mpumbavu au Mjinga. Hatukushushiwa dini tulizonazo iwe ni mapokeo ya Uyahudi, Ukristo au Uislamu au hata dini zetu za Asili ili tuwe wanyonge.

  Lakini tumetumia udhaifu wa kibinadamu kuziimarid=sha hizi dini kwa kunyanyasa watu na jamii kwa kisingio cha misingi ya kidini.

  Iweje leo Kasisi au Shekhe atoe mahubiri akilaani Wezi na Wanaohodhi mali huku yeye ni Mzinzi au ni ******?

  Ni udhaifu wa Kibinadamu unaotufanya tutumie dini kudhibti watu na nyendo kwa woga wa ama kudindiwa na kupingwa au watu kuwa huru kuamua.

  Chukulia Mzazi anayeamrisha Mtoto aende Sunday School au Madrass, ili iwe nini? Kwa nini Mtoto huyu asipewe Uhuru wa kuhiari anachotaka alimradi analelewa katika misingi ya kawaida ya kijamii inayomfanya awe muadilifu, mchapa kazi na mwenye kujua mipaka?
   
 8. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #8
  Mar 20, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,605
  Likes Received: 6,174
  Trophy Points: 280
  Wewe umeelewa kwamba mimi nimeelewaje? Maana unaweza kufikiri kwamba umeelewa nilivyoelewa kumbe hujaelewa hata punje.

  Pole sana, how condescending.Condescension is a sure flag for ignominy.Pole wewe unayejiona kuwa unaweza kumpa pole Chief mwenyewe Kiranga.

  As for kuvamia mambo nisiyoyaelewa vizuri, angalia isije kuwa wewe ndiye unayevamia mambo usiyoyaelewa vizuri.

  Kama unabisha kwamba unayaelewa mambo haya vizuri, let's go toe to toe with a reasoned exchange.

  Sio one liners zinazofuatiwa na nukta nyingiiii (............................) WTF does that even mean? Are you writing a table of contents?

  One liners hizi zinaonyesha uvivu wa kufikiri na ku develop positions, sasa kama huwezi hata kuandika coherently kutetea positions zako, au kama huwezi ku explain ukaeleweka unamaanisha nini kwa kusema "wewe ndivyo ulivyoelewa mwenzetu" unategemea tunaweza kwenda toe to toe tuka discuss Hegelian dialectics, Anselm, Augustine, Kant, Popper, Russell, Mbiti, Diop na some new spontaneous stuff?

  I don't mean to be crude, but I find intellectual laziness to be cruder

  Gtfakadahere
   
 9. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #9
  Mar 20, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Nliwahi kumsikia mtu akiitwa mwanafalsafa wa imani za kijamaa na kikoministi, Karl Max, katika maandiko yake anasema "...religion is opium of the people",kwamba kwa imani za watu kama hata kama unaonewa na mabwanyenye,hutakiwi kurudisha "..just turn the other cheek.."

  Ila nitofautine kidogo na mtoa maada,kwa heshima kabisa,si kuwa imani,mila na desturi ndizo zinazoduma maendeleo ya Waafrika,nataka hapa niungane na Marehemu Dr.Walter Rhodney, ambaye aliweka wazi kuwa kwa tamaduni za kiafrika zilivyokuwa karne ya 15 na 16, ziliwawezesha Waafrika kupiga hatua kubwa za kimaendeleo kwa wakati huo kuliko hata nchi za Ulaya. Kumbuka hata mapinduzi ya viwanda yalikuwa bado Uingereza,tayari waafrika walikuwa na system nzuri za utawala...mfano tawala kama za Ghana, Mali, Timbuktu... Mwanamutapa, Congo, Zulu...Maghreb, zilishakuwa na hata mifumo ya taaluma na sayansi na hisabati ambazo wazungu walipokuja walizikuta mfano kama Algebra zilikuwa maarufu Afrika Magharibi kabla ya kuja wazungu.


  Tamaduni za waafrika zilishika katika kazi na kujenga jamii miji na ustawi wa watu...kabila kama za Fulani,Tuareg...tamaduni za watu kama Nok zilishastawi katika teknolojia ya chuma na zana za chuma mbali sana kabla ya wazungu kutia mguu Afrika.

  Si kweli kuwa tamaduni au mila hizi ndizo zilizorudisha nyuma maendeleo ya Waafrika, ni wakati wa vugu mechi ya wazungu kuingia Afrika na kuharibu kila asili ya jambo la kimaendeleo la Waafrika,kuanzia mifumo ya utawala,imani,mila na hata mazingira..vyote vilihamishwa na kupewa muonekano na mtazomo wa kizungu usisaidia kupiga hatua yoyte ya uvumbuzi na ujenzi wa jamii ya kiafrika.

  Angalia wasomi wa shahada za juu tuliouwa nao sasa,wote walitokana na mifumo ya elimu za kikoloni ambzo haziwawezeshi wasomi hawa kuvumbua hata sindano,zaidi ya kupiga makelele tu, elimu ya kiafrika ilimwezesha mwafrika kuweza si tu kujitegemea mwenyewe bali hata kutegemewa na jamii yake, kwani ilimjenga kuwa mbunifu na mtendaji wa mambo ya faida na maendeleo kwake na kwa watu wake,tokea akiwa mdogo naye hurithisha kwa watoto wake na watoto kurithisha kwa watoto wao kwa namna mpya inayoendana na wakati huo,jamii ziliendelea na mabaki ya historia ya kazi hizo mengine mpaka leo yapo.

  Haya yote yameharibiwa na wazungu,kama nilivyosema kwa kupandikizo system mbovu zenye madhara mpaka leo kwa waafrika,tokea biashara ya utumwa, ukoloni,ubeberu,ukoloni mambo leo,utandawazi...hatua zote hizi zimechangia kufuta kabisa mila na tamaduni za kiafrika zenye faida kwa mazingira ya kiafrika.

  Sikatai kuwa kuna sehemu ya lawama kwa waafrika wenyewe kushindwa kutumia fursa ya kujitawala,walau kupunguza hizi legacy..kama alivyosema Prof.A.A. Mazrui "...pasingekua tatizo wakati nchi zetu zinapata uhuru viongozi wakakaa na kufikiria mifumo sahihi ya uwongozi kwa mujibu wa mazingira ya kiafirka,kama wangekaa wakafikiria tu tuwe na baraza la mji kama la mfalme wa Buganda, Wolof,Calabar, Ghana n.k...bdala yake tumekwenda mbali kutaka vyombo vyetu vya kimaamuzi viwe kama bunge la Cananada au WestminsterAbbey model.."
   
 10. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #10
  Mar 20, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  misingi ya kawaida unayotaka mtoto alelewe ndiyo misingi ya mzazi wake na alwayz inahusisha njia bora ya maisha ni bayana na imani kwa Mungu wa kweli kadiri ya imani ya mzazi................mzazi anayempenda mtoto wake hawezi kumuamini Mungu kisha akamuacha mtoto wake kipenzi aishi maisha yasiyompendeza Mungu (kadiri ya imani yake) hadi atakapokuwa mkubwa aamue mwenyewe!!!!!!!!!!! itakuwa ajabu kubwa na hatari..................

  kama ingekuwa watoto wapaswa kuachwa huru waamue wenyewe wakiwa wakubwa kamwe tusingewafundisha kuamkia wakubwa hadi watakapouwa wakubwa waamue wenyewe............ hata shule wasingepelekwa hadi wawe wakubwa waamue wenyewe............ hata kuvaa nguo tusingewafundisha .............nk. nk..... na mabo yote ya adabu, heshima na utii nk tusingewafundisha na tungewaacha hadi wawe wakubwa waamue wenyewe kujifunza ama la.................... itakuwa hatari kubwa hakika....................

  malezi ya watoto ni moja ya masuala magumu na yasiyotabirika matokeo yake hapa duniani................ kuna watoto wamekosa malezi, wakakulia mitaani lakini wakawa raia wema sana wenye matendo mazuri sana yanayompendeza Mungu na wanadamu............... wakati huohuo kuna wale waliolelewa katika maadili mema na wakatokea kuwa wahuni na waovu hata kukatisha tamaa wazazina jamii kwa ujumla............. lakini kama una mtoto/watoto utakuwa unanielewa vizuri............... hata hivyo vyovyote iwavyo........... the goal of every aprent ni kumlea mtoto wake katika missingi amabayo yeye mwenyewe (mzazi) anaamini mtoto ataongezeka umri na kimo na atampendeza Mungu na mwanadamu..................

  nilitaka kukusaidia hapo tu, niliona kama unavuka mstari.............
   
 11. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #11
  Mar 20, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  si kweli, nchi karibu zote za Kimagharibi, kimaadili na kimisingi zimejengwa kutoka katika Ukristu; nchi za Kiarabu na Kiislamu ambazo leo zimefanikiwa sana au zinapiga hatua ya maendeleo zinaongozwa na imani na desturi zao, hilo laweza kusema pia kuwa ni kweli uko Uchina, Japani, na India!

  Ni Afrika tu ambapo hatutaki kukubali kuwa na sisi tuna desturri na mila zetu ambazo tunaweza kuzitumia kuchochea maendeleo. Tunaamini maendeleo ni pamoja na kukumbatia desturi na mila za wageni!!

  Mila na desturi zetu si kikwazo cha maendeleo; mila na desturi za wageni zawezekana kuwa ndiyo kikwazo!

  lakini swali la nyongeza ambalo ni la kifalsafa ni JE, katika mila na desturi zetu kama Waafrika kuna mambo mazuri ambayo tukiyashikilia yanaweza kutusaidia katika kuelekea maendeleo? kama yapo ni yapi? Je, ili tuendelee ni lazima tupokee mila na desturi za watu wengine kwa sababu tunazihusisha na ubora na maendeleo?
   
 12. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #12
  Mar 21, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,605
  Likes Received: 6,174
  Trophy Points: 280
  Wazungu walivyokuwa wanaamini sana dini na authority za kina Aristotle tulikuwa nao sawa, mpaka juzi juzi hapa kwenye 1500's

  Wakapata matatizo sana, wakauana sana kwenye vita za kipuuzi kuwania ardhi na ufalme. Wakapata bubonic plague iliyoua mtu mmoja katika kila watatu katika population nzima ya Europe.

  Wakaanza kujiuliza, huyu mungu kama yupo kweli mbona anatutesa hivi?

  Pole pole wakaanza ku question vitu, wakaanza ku question authority ya Pope, wakaanza ku question authority ya diktats za kina Aristotle, sayansi na reason ikazaliwa upya katika enzi za Renaissance na Reformation.

  Ndipo hapo Ptolemy alipopinduliwa, mfumo wa uongo kwamba dunia ipo katikati ya ulimwengu na jua pamoja na nyota zote vinazunguka dunia ulipopinduliwa na sayansi za uchunguzi, Copernicus akaonyesha dunia inazunguka jua.Hapa tunaona revolutions zinavyoendana pamoja na ku debunk authoritarian myths.

  Galileo akaonyesha kwamba ukiondoa air resistance, kanuni za Aristotle kwamba vitu vizito huanguka kwa kasi zaidi ya vitu vyepesi si ya kweli, kwa kutumia sayansi ya majaribio.

  Hapo ndipo maendeleo ya Europe kupita Afrika yalipoanzia, kabla ya hapo tulikuwa almost sawa.

  Kwa hiyo tusitake kusema Ulaya wameendelea despite kuamini mungu, actually ulaya wameanza kuendelea baada ya kuacha kuamini mungu na kuanza kuweka mkazo kwenye uchunguzi wa kisayansi.

  Waarabu wamejaliwa natural resources kwa wingi na wameanza kuzi exploit kitambo, lakini zaidi ya hapo wana maendeleo gani ukiacha legacy ya kihistoria.Waarabu wamegundua nini recently? Na mimi naweza kuhusisha hii dormant nature yao na imani za kidini, wana madrasa zaidi ya madarasa.

  My point remains, habari za kuamini mungu na kuogopa mapokeo/ authority zinadumaza maendeleo.

  Kila kitu kinapaswa kuwa challenged.

  Kama wanavyosema TVZ/ SMZ (sijui kama bado wana hii slogan ya Karl Marx)

  Mapinduzi Daima.
   
 13. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #13
  Mar 21, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  mkuu inaonekana unajitahidi sana katika lusoma na kujisomea............. hongera na kaza buti zaidi............. inapendeza kuona unafahamu kidogo falsafa na wanafalsafa japo kwa majina yao lakini unahitaji pia kufahamu kidogo kuhusu maisha................ na pia japo kidogo kuhusu dini.......................... kung'ang'ana na falsafa bila kujua maisha ni nini ni sawa na mtu anayemtamani panzi anayeruka porini huku akiwa anampuuza njiwa aliye mkononi!!!!!!!!!............

  nimeshindwa kushiriki mashindano uliyopendekeza kwa sababu sijajua tutatumia lugha gani................. pili sijajua kama utajadili kwa kutumia mawazo yako ama ya hao mabingwa wako ulionirodheshea............. na tatu sijajua kama dini yako ya sasa inauruhusu kujifunza kuhusu dini zingine na Mungu wa kweli................ ukinisaidia hapo, hata haya ya "table of contents" (kama ulivyoyaita) utayaelewa................
   
 14. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #14
  Mar 21, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  On the other hand Taifa lililoendelea zaidi duniani na lenye nguvu zaidi limejengwa kutoka katika misingi ya kuamini juu ya Mungu huyo! Kwao huyo Mungu hakuwa kikwazo cha maendeleo bali ndio sababu hasa ya maendeleo hayo.
   
 15. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #15
  Mar 21, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,605
  Likes Received: 6,174
  Trophy Points: 280
  Condescending as usual, and the condescension continues to expose the naked ignominy.Nani kakwambia situmii uzoefu wa maisha? Ukisoma posts zangu za juu hapo utaona ninavyopraise experimenting in the real world as opposed to kukariri, utaona nilivyomsifia Galileo kwa kum debunk Aristotle, utaona nilivyomsifia Copernicus kwa kum debunk Ptolemy, sasa how can you say kwamba mimi nakuja na ungwini academic bila actual world experiment? Nimeflow kutoka the ancients, the medievals, the orients mpaka modern day Shaolin. Na naandika hivi kuonyesha kwamba ninavyoongea si crackpot theory ni vitu vinavyotambulika. Wewe unaendelea kujaza post na nukta kama table of contents bila kuelezea wala aibu.

  Chagua lugha yoyote inayotumika widely hapa JF, Kiswahili au Kiingereza.Mchagua jembe si mkulima, na kwa kuanza ku make a big deal about lugha kunakuonyesha kwamba huna hoja.Maana unataka kufanya viroja kuwa hoja.

  Mawazo yangu yakirandana na ya hao mabingwa yanaacha kuwa yangu wala ya hao mabingwa, yanakuwa mawazo tu kuhusu kitu fulani, huwezi kuyaangalia mawazo bila ya kuangalia nani kayatoa? Nilivyokutajia majina hayo si kwamba nayapa uzito mawazo kwa majina ya watu - sina tabia ya kubabaikia majina na wala sipendi kubabaikiwa- ni katika kukufahamisha line of thought yangu imelalia wapi, kwamba ukitaka summary ya my line of thoughts angalia classic arguments za kumsaga mungu zinazokuwa associated na hayo majina.

  Mimi sina dini na niko openminded, make your case for a god in a convincing way and you will win me over, but not with one liners followed by a million and one nuktas, you gotta do your homework.

  Table of contents, by the very nature of its function, iko vague, inampa mtu a rather narrow window into the subject matter, sasa usitegemee mimi nielewe this incoherent table of content kama hujaweza kunyambulisha mambo.

  I'm ready, I don't know about you.

  Don't say that you haven't been warned by this mental Jujitsu master.
   
 16. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #16
  Mar 21, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Kuna desturi hii ya umoja, kushirikiana kwenye majanga(eg misiba) na kwenye Furaha( Harusi). Hii inaenda mbali zadi kwenye undugu extended family

  Mfanokulikuwa na desturi mtoto anakuwa ni wa jamii nzima akifanya kosa anaweza kukanywa au kuadhibiwa. Zipo mila na desturi nyingi.

  Kuna Desturi vijijini wachawi, vijana wakorofi walidhibitiwa na kuadhibiwa?( Mfano kutengwa, kufukuzwa) kwa sheria za kimila. Lakini leo hii tumevuruga hata mfumo wa sheria zilizokuwa zinafanya kazi vizuri vijijini.

  Matatizo kama ya ya Tarime( Mapanga shasha). Yametokea matatizo ndo serikali inawaita wazee. but wazee wakifanya maamuzi kwenye kijiji wanaambiwa wao sio mahakama.

  Mifano iko mingi
   
 17. N

  Ndjabu Da Dude JF-Expert Member

  #17
  Mar 21, 2010
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 3,648
  Likes Received: 408
  Trophy Points: 180
  Hizi mbona ni porojo tu?
   
 18. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #18
  Mar 21, 2010
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Ni porojo kivipi.

  Naomba unieleweshe ndugu nami niweze kutambua kuwa hizo ni porojo.
   
 19. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #19
  Mar 21, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,605
  Likes Received: 6,174
  Trophy Points: 280
  Kama unakusudia kusema maneno yuangu ni porojo, porojo zaidi ni kuzisema hizi porojo bila kuonyesha porojo ilipo.

  No research, no data, no right to speak.

  Tuonyeshe porojo iko wapi tuone.

  Ama sivyo maneno yako "Hizi mbona ni porojo tu" yanaweza kuwa ndiyo porojo kubwa kabisa katika thread hii.
   
 20. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #20
  Mar 21, 2010
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Ni porojo kwa sababu si kweli hizo ndizo zilikuwa sababu za maendeleo na kama causes of black death until the 19th century bado kulikuwa na common occurances ya vifo vya misimu in some areas.

  na kama ni dini italy and spain wana huge numbers in their population ambao ni waumini, bila ya hata kusema wa israel ambao unaweza sema kwa haraka haraka about 80% of the theorist today ni wao. therefore kusema mungu ni chanzo cha failure is just bunkum.
   
Loading...