BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,376
- 8,120
Mei 29, 2023, Taifa la #Nigeria, lenye utajiri wa Dola Bilioni 441 GDP na idadi kubwa ya Watu Barani #Afrika (Milioni 223), litashuhudia kuapishwa kwa Rais Mpya, #BolaTinubu na Makamu wake #KashimShettima
Pamoja na ukubwa wa Uchumi wake, bado Nchi hiyo imekosa utulivu katika maeneo mengi ikiwemo hali ya Usalama, mfumuko mkubwa wa bei na gharama kubwa za maisha, hali inayochangia kuzorota kwa Uchumi wake
Matarajio ya wengi hata wale ambao hawakumpigia Kura, watataka kuona mabadiliko ya mapema ya hali hizo. Hapa chini kuna baadhi ya vikwazo vikubwa vinavyomusbiri ofisini Rais Tinubu
MAMBO 5 YANAYOMSUBIRI OFISINI RAIS MPYA WA NIGERIA
1. Ruzuku ya Mafuta: Licha ya kuwa kati ya Nchi zinazozalisha Mafuta kwa wingi, Nigeria imekuwa ikikumbwa na uhaba wa Mafuta. Bola Tinubu ameahidi kuifuta Ruzuku hiyo, hali inayotajwa kuwa itasababisha kupanda zaidi kwa bei ya Mafuta
2. Uungwaji Mkono: Licha ya kushinda nafasi ya Urais kwa 37% ya Kura, Tinubu atakuwa na kibarua kigumu cha kuliunganisha Taifa hilo linalooneka kugawanyika kutokana na mambo Ukabila pamoja na Vijana wengi kutomuunga mkono
3. Kuimarisha Uchumi: Mtihani mwingine uko kwenye eneo la Uchumi ambapo takwimu zinaonesha Mtu 1 kati ya 3 Nchini humo hana Ajira, Mfumuko wa Bei umefikia 22%, Watu Milioni 96 wanaishi chini ya Mstari wa Umasikini
4. Hali Mbaya ya Usalama: Kwa muda mrefu taifa hilo limekuwa likisumbuliwa na Matukio ya Utekaji, Mauaji na Mashambulio ya Kigaidi. Hata hivyo, Tinubu aliahidi kuwa akishinda atatumia Vikosi Maalumu kupambana na vitendo hivyo
5. Afya Yake Kutetereka: Kiongozi huyo amekuwa akitajwa kutokuwa sawa Kiafya ikiwa ni pamoja kusambaa kwa picha zinaoonesha akitembea na Mfuko Maalumu wa kuhifadhia haja ndogo na kusafiri Nje ya Nchi mara kwa mara kwaajili ya Matibabu
============