Vijue vijitabia vya kujihami na kutojiamini

Vijue vijitabia vya kujihami na kutojiamini

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Posts
8,809
Reaction score
15,442
119.jpg


Kuna wakati huwa tunataka kujilinda dhidi ya hisia tusizozipenda za matukio au mambo yenye kututokea. Tunataka kukwepa, mawazo, hisia na matarajio fulani.

Kwenye nadharia za kisaikolojia, kuna kitu kinaitwa id, ego na superego. Hii id naweza kusema ni miito au utashi wa kimwili wa binadamu, ni kama choyo, matamanio na miito yote ya kibaolojia. Kwa mfano, kutaka kufanya mapenzi, kutaka kula, kutaka kupata heshima na mengine.

Ego, ni sauti za jamii, ni yale tuliyoambiwa kwamba, ni mabaya au mazuri katika jamii. Hivyo, kwa mfano, mtu anapotaka kuiba (id, sauti yenye kumwambia aache kwa sababu ni vibaya, hujitokeza (siyo sauti inayosikika kwa masikio, la hasha). Kwa hiyo, wakati mwingine mtu anajikuta amefungwa kwenye uhitaji, lakini kuna kitu kinamzuia kwa hofu ya kuharibu au kupata matatizo.

Kile kinachoitwa superego hutafuta suluhu, hali hiyo inapotokea. Hii superego, ina kawaida ya kutotaka kuiudhi id au ego. Katika hali kama hiyo, inatoa suluhu isiyo muafaka sana. Suluhu hii ndiyo ambayo tunaiita KUJIHAMI. Suluhu hii inatolewa ili mhusika ajisikie ahueni, asiumizwe na mtihani wa kushindwa/kuchagua ulioko mbele yake.


Aina za Kujihami:

1. Fidia: Kuhamisha udhaifu wa eneo moja kuupeleke kwenye uimara alionao mtu. Mfano mtoto asiyejiweza darasani, lakini anayejua mpira. Huyu atapeleka nguvu zake zote kwenye mpira ili kuziba/kufidia lile pengo la uwezo haba darasani. Mtu dhaifu wa mwili, anaweza kuwa mwongeaji mwenye ‘mkwara' mzito sana. Anafidia udhaifu wa mwili kwa sauti yake.

2. Kupinga: Hii ni hali ya kukataa ukweli/ hali halisi na kujifanya jambo halipo. Mfano mtu ameathirika kwa Ukimwi (kwa mujibu wa vipimo), lakini anajifanya walikosea vipimo. Anajifanya kwa njia hiyo hadi inafikia mahali anaamini, kwamba, vipimo vilikosewa.
shutterstock_demandrespect-378x334.jpg


3. Kuhamisha: Mtu anahamisha hisia zake chungu kutoka shabaha asiyoiweza hadi shabaha dhaifu. Kwa mfano, mume anafokewa na bosi wake kazini mchana. Hana ubavu wa kurudishia maudhi hayo kwa bosi wake, kwani ni shabaha imara. Kinachotokea ni mwanaume huyu kumfokea mkewe anaporudi nyumbani jioni. Hasira za kufokewa na bosi zinatupiwa kwa mke. Mke naye atamalizia hasira za kufokewa na mume, kwa mtoto wake. Huenda mtoto akamalizia hasira za kufokewa na mama, kwa paka anayefugwa pale nyumbani. Wengi sana tunatumia njia hii ya kujihami bila kujua. Ndio maana kwa Dar unaweza kukuta makondakta au ‘wapiga debe' ni shabaha dhaifu kwa abiria ambao huko walikotoka wamepambana na shabaha (watu wa hali) imara ambazo wasingeweza kuzirudishia maudhi au kero zilizowapata.

4. Ualinacha: mtu anakwepa ukweli wa kushindwa jambo kwa kujifurahisha kimawazo kwamba, limekuwa. Kwa mfano, aliyeshindwa masomo anajenga picha za kuwa amefanikiwa na ana kazi nzuri. Ni picha ambazo hatimaye humfanya aone na kuhisi kama kweli, jambo limekuwa na ni halisi. Kuna wakati hali hii ikizidi, mtu huchanganyikiwa.

man-looking-in-the-mirror-pf6.jpg


5. Kiwango: mtu hukataa kuukubali ukweli kwa kuangalia asilimia ya matokeo. Mfano, mtu ameambiwa ana kansa hatua ya nne. Anapeleka nguvu zake kwenye asilimia ya wanaoweza kupona kwenye hatua hiyo, siyo wanaokufa.

6. Urushaji: hii ni mtu kukataa udhaifu wake kwa kumsukumia mwingine. Mume mlevi anamlaumu mkewe kwamba, ujeuri wake ndio unamfanya awe mlevi. Inatokea kwamba, huyu anayemrushia mwenzake, anaamini kabisa katika kile anachosema.mwanasiasa anashindwa uchaguzi kwa kutokubalika, anasingizia rushwa.
unhappy-black-couple-pf.jpg

7. Sizitaki: hii huwa tunaaiita ‘sizitaki mbichi hizi', kwenye misemo ya Kiswahili. Mwanamke anamkataa mwanaume , na mwanaume huyu anasema, ‘kwanza mbaya', au ‘nilikuwa namtania, nani amtake yule Malaya.'

8. Kukandamiza: Ni kukataa hisia, mawazo machungu kwa kuyakandamiza. Hujasahau lakini unaamini umesahau. Hii hulipua sana mabomu ya hisia baadaye. Kwenye mawazo ya kawaida tunaweza kulisahau jambo husika, lakini siyo rahisi mawazo ya kina kulifuta. Hivyo unasahau bila kusamehe na kuondokana na maumivu fulani, halafu baadaye jambo hilo linalipuka likiwa katika sura tofauti.

9. Kukarabati: Kujaribu kurejesha tabia au mawazo ambayo hayakubaliki kwa wengine au jamii. Mfano, kumsifu sana mtu baada ya kumtukana huko nyuma. Bila shaka umeshaona au umeshawahi kufanya jambo hili. Unamnyanyasa mtoto wa kambo (hususan kwa wanawake) anapofanikiwa, unarejea kwake kwa kumsifu sana, kwamba, alikuwa na heshima na upendo sana kwa watu.
shutterstock_nicetomother-378x414.jpg


10. Kujifaragua: Kupunguza mashaka na hisia chungu kwa kuchukua tabia, hisia za upande wa pili. Mfano, mtu anajifanya anampenda mwingine kama rafiki kikwelikweli wakati anamchukia sana. Kuna idadi kubwa ya watu wa aina hii, ambao wanajifanya ni marafiki wa wengine, wakati kuna uadui mkubwa kati yao. Huku ni kujihami-ni kutaka kupunguza maumivu ya kihisia.

sioi.jpg


11. Kujifunganisha: Ni mtu kujaribu kujikimbia kwa kujifunganisha na anaodhani wana thamani zaidi. Mfano, kuona fahari kusema unajuana na Waziri fulani au kigogo fulani au hata mtoto wa kigogo fulani, wakati haikuwa inahitajiwa. Jikague ni wakati gani unajihami na kama kujihami huko kunakusaidia au hapana…..


Je inawezekana kuondokana na tatizo la kutojiamini?
Makala inayofuata itakuwa na majibu yote, ungana nami siku ya Ijumaa……..
 
Mtambuzi... Mada nzuri sana hii na ipo valid. Naomba niongeze kwa kuweka aina ya watu ambao Hawajiamini (Take note sijazingatia kujihami).

A]. Wale wasiojiamini Daima

Kuna watu hawajiamini no matter the circumstances. Inaweza ikawa kila kitu kipo according na matakwa yake or yakiwa yanam favor yeye but bado hajiamini. Huyu mtu karibu muda wote hajiamini kabisaa... Mtu asie jiamini wa namna hii ndio mbaya kuliko wote. Hakuna zuri kwao, kutafula lawama katika kila jambo (bila kujalisha hizo lawama anajipachika mwenyewe ama anapachika kwa wengine). Na siku zote hana amani or akiwa nayo ipo kwa muda mfupi sana.

B]. Wasiojiamini tokana na Watu waliomzunguka.

Kuna watu ambao kujiamini kwao sio tatizo. Ila huwa tatizo pale inapotokea yupo miongoni mwa kundi/watu ambao anahisi kwa namna moja ama nyingine wanamzidi kitu fulani, ama ni tishio kiasi fulani, ama wana qualities ambazo mhusika anahitaji awe nazo but bado hajafikia. In a way hii kutojiamini inakuwa intokana na kukumbana na watu ambao kwake kawaweka (kwa siri rohoni kwake) kama ngazi fulani ya juu.

C]. Wasiojiamini tokana na Mazingira.

Kama ilivyo wazi... Kila mtu ana maeneo yake ya kujidaia. Hasa wale ambao huwa vinara katika maeneo yao ya kujidaia. Mfano inapotokea mtu ambae ni star, lets say Bongo Celebrity (ambae hajabahatika kisomo); tokana na umaarufu na impact yake katika jamii akaalikwa kwenye masuala yanayohusu maslahi ya Taifa kwa vijana na akakutaniswa na Wasomi toka vitengo mbali mbali kujadili hoja muendelezo. Kwa kiasi kikubwa huyo Celebrity hataweza kujiamini to the extent ajiachie sana kwa kujua kuna wataalam pale ambao wapo wamesomea na kujua nini hasa wanawasilisha.
 
HorsePower, nimecheka mbaya, yaani alichosoma Madame B na kujifunza katika makala hii ni hiyo body ya huyo mwanaume hakuna kingine....

Ngoja niondoe hiyo picha niweke mwanaume kimbaumbau

Nafikiri baada ya kuona umbo la huyo kaka, darsa ulilolitoa la vijitabia vya kujihami na kutojiamini likamtoka ghafla!!! Mtambuzi inabidi sasa uwe mwangalifu na picha unazoweka maana zingine zinawathiri watu na unaweza kukuta lengo lako la kurusha mada yako hapa lisitimie, loh!
 
nimekukubali mwana asante sana kwa mada nzuri ambayo itatufanya tubadilike tulikokuwa nakuwa kivingine ila huyu man.jpg amenivutia zaiidi fanya mawasiliano naye basi ila yasitokee majanga bure na mentor akajua
 
Mtambuzi naunga mkono no 6 na 7, kwa kweli ni kweli tupu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom