Vijiji 11,313 vimeunganishiwa umeme kati ya vijiji 12,318 vya bara

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,502
9,281
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa REA ambaye pia ni Mkurugenzi wa Umeme Vijijini, Mhandisi Jones Olotu akizungumza na Jukwaa la Wahariri wa Habari Tanzania (Tanzania Editor's Forum - TEF) kuhusu hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini amesema hadi kufikia Novemba 23 mwaka huu, vijiji 11,313 vimeunganishiwa umeme kati ya vijiji 12,318 vya bara, huku vijiji 1,005 vilivyosalia vitakamilika Juni mwakani.

Amesema Serikali ipo mbioni kuhakikisha vitongoji 36,101 vinafikiwa na umeme na tayari imeandaa mipango madhubuti ili kufikia mwaka 2030 vitongoji vyote viunganishwe umeme.
 
Back
Top Bottom