Mbunge Sichalwe Aibana Wizara ya Nishati Kufikisha Umeme Kwenye Vijiji 20 Vilivyosalia

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,902
945

MBUNGE CONDENSTER SICHALWE AIBANA WIZARA YA NISHATI KUFIKISHA UMEME VIJIJI 20 VILIVYOSALIA JIMBO LA MOMBA

"Je, Serikali ina mpango gani wa kukamilisha zoezi la kuwasha umeme kwenye Vijiji vilivyosalia katika Jimbo la Momba" - Mhe. Condester Mundy Michael Sichalwe, Mbunge wa Jimbo la Momba

"Serikali inatekeleza mradi wa kusambaza umeme Vijijini Awamu III mzunguko wa pili ambapo Vijiji vyote visivyo na umeme vitafikiwa na huduma ya umeme. Mradi huu unahudumia Vijiji 42 vilivyosalia katika Jimbo la Momba ambapo kati ya Vijiji hivyo 22 vimekwelishawashiwa umeme na Vijiji 20 kazi mbalimbali zinaendelea. Mradi huu unatarajiwa kukamilika mwezi Disemba 202" - Mhe. Stephen Byabato, Naibu Waziri Nishati

"Katika Vijiji vilivyosalia nguzo zimepelekwa katika maeneo na zimeachwa kwa muda mrefu na wananchi wamechukulia nguzo zimetelekezwa, Je, ni lini shughuli itaendelea kwa ukamilifu kuona nguzo zinasimikwa an Vijiji vinawashwa umeme?" - Mhe. Condester Mundy Michael Sichalwe, Mbunge wa Jimbo la Momba

"Katika Vijiji ambavyo vimepatiwa umeme, umeme umekuwa siyo toshelevu hivyo wawekezaji kuvunjika Moyo kufanya shughuli zinazohitaji umeme mkubwa, Je, ni lini Serikali itaweka Capacitor au Busta kwenye Vijiji ikiwa ni sambamba na kujenga Kituo cha umeme mkubwa kwenye Kata ya Nkangama" - Mhe. Condester Mundy Michael Sichalwe, Mbunge wa Jimbo la Momba

"Kwenye Vijiji 20 ambavyo vimebaki kazi katika hatua mbalimbali zinaendelea. Mkandarasi anayefanya kazi katika Mkoa wa Songwe yuko zaidi ya asilimia 80. Kabla ya Mwezi Disemba 2023 maeneo yote yatakuwa yamepatiwa umeme. Vifaa vilivyowekwa kwenye maeneo hayo ni vile ambavyo vitakuja kutumika katika maeneo hayo na havijatelekezwa na vitatumika kufanya kazi inayostahili kufanyika" - Mhe. Stephen Byabato, Naibu Waziri wa Nishati

"Ni kweli kumekuwa na upungufu wa umeme katika maeneo mbalimbali na ni kwasababu ya Mahitaji kuwa makubwa. Wizara ya Nishati tunaendelea kufanya tathimini na katika awamu ya kwanza ya mradi wa Gridi Imara tumetenga vituo vya kupoza umeme 15 katika maeneo mbalimbali kulingana na mahitaji ya Umeme yalivyo. Nia ya Serikali ni kuhakikisha ifikapo 2023 kila Wilaya iwe imepata kituo cha kupoza umeme kulingana na uwezekano wa upatikanaji wa fedha kutoka Serikalini ili kuhakikisha kwamba tunafikisha umeme wa kutosheleza katika maeneo yetu" - Mhe. Stephen Byabato, Naibu Waziri wa Nishati.

 
Back
Top Bottom