GuDume
JF-Expert Member
- Jan 18, 2015
- 6,652
- 14,247
Nimewaza sana, wakati fulani nawaza nafika mbali sana. Hivi unajisikiaje unapoishi katikati ya wapuuzi halafu wewe tu ndo una akili? Inaumiza na inatesa sana. Ni mateso ambayo sisi wengine tunakumbana nayo kila siku.
Kila unachoandika watu hawakielewi hawaelewi ujumbe mzito katika lugha nyepesi unayotumia unashangaa vijana wengi wa siku hizi wanazaliwa akili wameziacha tumboni mwa mama zao.
Duniani wanakuja bila kitu kichwani empty kabisa, hawa ndo wanachafua tu mazingira na kufanya taifa lionekane lina watu wengi kumbe asilimia 80 ni magarasa.
Umewahi kucheza karata? Mtu anaweza lamba magarasa mengi sana ila wewe ukawa na mali au madume machache tu ukamshinda ndo maisha yalivyo kwa vijana wa kitanzania.
Wengi walishaacha kufikiri na hawataki kabisa kusumbua bongo zao hivyo zimeota kutu na kufunikwa na ukungu wa ule uchafu wa kutu ya maji akili zimefubaa.
Kuna kipindi unajikuta wewe peke yako ndo unawaza na kuwazua, waliokuzunguka wanasikilizia sauti ya tumbo wanakula, wanavimbiwa wanaanza kutoa gesi na wengine kuharisha.
Wewe peke yako ndo unaumiza kichwa, wewe ndo unajiuliza tumetoka wapi, tupo wapi na tunaelekea wapi, imagine huu si ni mzigo mzito kwa mtu mmoja? Unajiangalia umebeba watu zaidi ya milioni moja unafikiria kwa niaba yao wao wapo nje wanacheza kombolela wakisubiria shujaa aje abutue.
Wewe tu ndo unajua kuwa michezo yao ni mauti yao unawaza huko wanakojificha kuna nyoka, nge, tandu na kila aina ya hatari wao hawajali hii hali, hawaoni hatari na hawana habari unatumia akili kufikiri wao wanatumia matumbo kufikiri.
Wakati mwingine unawaza mbali sana hawa miaka ile ya gharika waliponaje? Ilikuaje wakapona? Hata wakati wa Sodoma na Gomora si wangechomwa moto wawe mbolea? Unawaza hata hivyo kama wangekuwa mbolea ingeota miti yenye majani na matunda sumu.
Hapo ndo mtu unawaza tu why me? Ni usiku wa kiza kinene tunatembea bila taa watu wanapapasa hawaoni vyema.
Huwa siku zote najiuliza katika kundi kubwa la vichaa. Je kiongozi wao anakuwa na afadhali kidogo au kichaa zaidi? Hali kadhalika katika kundi la wenye akili kiongozi wao anakuwa na akili zaidi au akili hamna kabisa? Hapa ndipo ilipo tafakuri.
Hamjui mnavyotutesa sisi wenye akili hamjui tu mateso mnayotupa ni makubwa ni bora ya kutwangwa kwenye kinu kuliko mnavyotufanyia ninyi ndugu zetu ndiyo mtabaki kuwa ndugu zetu tu maana unaweza chagua rafiki lakini huwezi chagua ndugu ndugu ni ndugu yako hata kama ni taahira.
Bora tu nife, nimechoka kuwa mimi na wengine wachache ndo tunakuwa tunatumia akili inachosha sana na kuumiza kichwa inatesa moyo na akili.
Wasalaam.