Vijana walikaririshwa kwamba tatizo ni Mfumo!!!

Uloi nga mâché68

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2013
Posts
486
Reaction score
153
Wakati wa Uchaguzi Vijana na kundi fulani waliaminishwa kwamba tatizo la Nchi yetu ni Mfumo mbovu na siyo viongozi. Waliaminishwa kwamba Mgombea wao ambaye kakulia kwenye huo wanaoita mfumo mbovu ndiye ataleta mabadiliko!!! Aidha waliaminishwa mpiga kampeni mmoja ambaye naye aliongoza Nchi kwa miaka mingi na kuchangia hicho walichokiita mfumo mbovu eti naye angeleta mabadiliko!!
Wakati ule akili zao ziliganda kabisa kushindwa kuelewa kuwa mgombea wao alikuwa na UCHU uliopitiliza kwenda Magogoni kiasi cha kuamini kwamba ni yeye tu anayefaa kuwa RAIS na siyo mtu mwingine!!
Ajabu hao washabiki wake ukiwauliza watabadilije mfumo watu waliokulia na kuzoea Mfumo wanaouita mbovu waliishia kuwa na jazba na kusema ni bora kuchagua jiwe au shetani kuliko CCM!!
Mpaka wakati huu wamepata fundisho kuwa UKAWA hawakuwa na lengo la kuleta mabadiliko maana hata Sera yao walishaiacha kwa kusafisha UFISADI wa Mgombea wao kwa maelezo mepesi na ya kitoto eti mwenye ushahidi ampeleke Mahakamani! KUMBE TATIZO SIYO MFUMO NI DHAMIRA TU YA WALIOPEWA DHAMANA BILA KUJALI NI UKAWA AU CCM.
 
Hakika in bora juchagua jiwe kuliko CCM, hata Leo uchaguzi ukirudiwa sitampigia kura Magufuli, me siyo mtoto wa kunidanganya kwa peremende,
 
CCM imefanya maamuzi sahihi kumteua Magufuli kuwa mgombea Urais. Sasa matunda ya uamuzi huo tumeyaona
 
Sijakuelewa vizuri unaongelea nini, hebu jipange uandike vizuri ni nini unachotaka tujadili.
 
Hakika in bora juchagua jiwe kuliko CCM, hata Leo uchaguzi ukirudiwa sitampigia kura Magufuli, me siyo mtoto wa kunidanganya kwa peremende,

Wewe una chuki ya ukanda na ukabila. Kampe huyo mgombea wako uongozi wa familia yako maana wa Nchi wenye akili tumekataa!
 
Miaka mitano ya Magufuli ni mingi sana kwann usifunge mdomo wako km huna cha kuongea,
 
ccm imefanya maamuzi sahihi kumteua magufuli kuwa mgombea urais. Sasa matunda ya uamuzi huo tumeyaona
hayo matunda yako kwenye tv za ccm, magazeti ya ccm, na redio za ccm.! Siyo kwenye maisha ya watanZania.
 
Uloi nga mâché68;14821949 said:
Wewe una chuki ya ukanda na ukabila. Kampe huyo mgombea wako uongozi wa familia yako maana wa Nchi wenye akili tumekataa!

Chuki, ukanda na ukabila wangu watoka wapi hapa??? ww ndo zao LA huo ukanda na ukabila, halafu hii nchi ingekuwa na watu wenye akili Leo yangekuwa yanaongelewa mengine na sio kusafisha mitaro na barabara, kwakuwa hatuna akili na akili zimedumaa hazifanyi kazi ndo maana tupo hivi tulivyo
 
We mtoa mada we hujasikia juzi kwenye kikao cha ccm wamemuonya Pombe asiwe na kasi sana eti taarifa zingine analetewa majungu!!? Hivi hujui kuwa mfumo ccm kwa kauli hiyo tayari wanamdhibiti rais!? Pombe hataweza ndani ya mfumo ccm asilani, muda utaongea wenyewe.
 
Kama ww ni mzee unaona unaona vijana walidanganywa jas sababu ya huu mwanzo,nyie ndio aina ya wazee tusiowataka kabisa,binafsi nadhan anchokifanya mkuu ni kuwashtua watu kwanza wakat akiwa anajipanga aje na strategy ipi,huwezi kuniaminisha kuwa miaka kumi viongozi watakuwa wanashtukiza kila ofis na makaratasi kufukuza watu, hiyo sio akili ya ccm wala sio akili ya kiongoz yoyote ni akili yako ww binafsi kwa ajili ya kujipendekeza tu.
 
Chuki, ukanda na ukabila wangu watoka wapi hapa??? ww ndo zao LA huo ukanda na ukabila, halafu hii nchi ingekuwa na watu wenye akili Leo yangekuwa yanaongelewa mengine na sio kusafisha mitaro na barabara, kwakuwa hatuna akili na akili zimedumaa hazifanyi kazi ndo maana tupo hivi tulivyo

Akili finyu ni kudeki barabara na kupoteza fahamu kwa ajili ya FISADI!
 
Hahaha yaani mpaka sasa kuna watu akili mgando wanaamini kuwa mamvi na yule mwenzake eti wangewafaa
 
Weka akiba ya maneno, mapema mno.

Magufuli anafanya kazi nje ya mfumo wenu na ndio maana saa hii uko hapa unashangilia. Kwa kawaida ya CCM saa hizi mmngekuwa uwanja wa taifa mnatapanya fedha, sasa wewe kwa akili yako huoni ni mfumo ndio tatizo letu?

Mfumo wa kuchekacheka na kusafiri umepita, SASA KAZI TU
 
Uloi nga mâché68;14821886 said:
Wakati wa Uchaguzi Vijana na kundi fulani waliaminishwa kwamba tatizo la Nchi yetu ni Mfumo mbovu na siyo viongozi. Waliaminishwa kwamba Mgombea wao ambaye kakulia kwenye huo wanaoita mfumo mbovu ndiye ataleta mabadiliko!!! Aidha waliaminishwa mpiga kampeni mmoja ambaye naye aliongoza Nchi kwa miaka mingi na kuchangia hicho walichokiita mfumo mbovu eti naye angeleta mabadiliko!!
Wakati ule akili zao ziliganda kabisa kushindwa kuelewa kuwa mgombea wao alikuwa na UCHU uliopitiliza kwenda Magogoni kiasi cha kuamini kwamba ni yeye tu anayefaa kuwa RAIS na siyo mtu mwingine!!
Ajabu hao washabiki wake ukiwauliza watabadilije mfumo watu waliokulia na kuzoea Mfumo wanaouita mbovu waliishia kuwa na jazba na kusema ni bora kuchagua jiwe au shetani kuliko CCM!!
Mpaka wakati huu wamepata fundisho kuwa UKAWA hawakuwa na lengo la kuleta mabadiliko maana hata Sera yao walishaiacha kwa kusafisha UFISADI wa Mgombea wao kwa maelezo mepesi na ya kitoto eti mwenye ushahidi ampeleke Mahakamani! KUMBE TATIZO SIYO MFUMO NI DHAMIRA TU YA WALIOPEWA DHAMANA BILA KUJALI NI UKAWA AU CCM.
kwa ufupi tu tuna hitaji la kubadili mfumo kuliko kumtegemea mtu kama ilivyo sasa, lazina uwepo utaratibu wa kumlazimisha kiongozi kufanya matakwa yetu. mfumo unao mlazimisha kiongozi asiye na dhamira awe na dhamira.
 
Tatizo ni mfumo wa ccm umejaa wezi,, Magufuli akitaka mafanikio asichague mtu yoyote kutoka CCM.. Huko hakuna msafi wote wameoza
 
Uloi nga mâché68;14821886 said:
Wakati wa Uchaguzi Vijana na kundi fulani waliaminishwa kwamba tatizo la Nchi yetu ni Mfumo mbovu na siyo viongozi. Waliaminishwa kwamba Mgombea wao ambaye kakulia kwenye huo wanaoita mfumo mbovu ndiye ataleta mabadiliko!!! Aidha waliaminishwa mpiga kampeni mmoja ambaye naye aliongoza Nchi kwa miaka mingi na kuchangia hicho walichokiita mfumo mbovu eti naye angeleta mabadiliko!!
Wakati ule akili zao ziliganda kabisa kushindwa kuelewa kuwa mgombea wao alikuwa na UCHU uliopitiliza kwenda Magogoni kiasi cha kuamini kwamba ni yeye tu anayefaa kuwa RAIS na siyo mtu mwingine!!
Ajabu hao washabiki wake ukiwauliza watabadilije mfumo watu waliokulia na kuzoea Mfumo wanaouita mbovu waliishia kuwa na jazba na kusema ni bora kuchagua jiwe au shetani kuliko CCM!!
Mpaka wakati huu wamepata fundisho kuwa UKAWA hawakuwa na lengo la kuleta mabadiliko maana hata Sera yao walishaiacha kwa kusafisha UFISADI wa Mgombea wao kwa maelezo mepesi na ya kitoto eti mwenye ushahidi ampeleke Mahakamani! KUMBE TATIZO SIYO MFUMO NI DHAMIRA TU YA WALIOPEWA DHAMANA BILA KUJALI NI UKAWA AU CCM.

CCM imefanya maamuzi sahihi kumteua Magufuli kuwa mgombea Urais. Sasa matunda ya uamuzi huo tumeyaona

Tatizo la wana-ccm ni kujisahau kwamba hao wote wanaotolewa kafara si wa-ccm wenzao.
Je? kabla ya utawala huu ilikuwepo chadema madarakani?
 
Ila LOWASSA angeweza ndani ya Mfumo ambao ni MBOWE pekee ana uwezo wa kumteua Mgombea bila ushindani wowote ndani ya Chama??? Wewe kumbe ndio miongoni mwa waliopewa jina zuri la Mh MKAPA pale jangwani!!!
 
Back
Top Bottom