Vijana wa leo mnafahamu maana ya rangi za bendera ya CHADEMA?

Ileje

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
8,793
12,238
  1. Bendera ya CHADEMA ina rangi nne: Nyeusi, Bluu isiyokoza (light blue), nyeupe na nyekundu.
  2. Bendera ya CHADEMA ina nembo ya kiganya cha mkono kilichonyoosha vidole viwili katika mfumo wa V kama ishara ya USHINDI. CHADEMA ni chama kinacholenga kushinda kidemokrasia na hatimaye kuleta ushindi wa maendeleo ya taifa.
  3. Rangi ya BLUU ISIYOKOZA iko juu ya rangi NYEKUNDU kama ishara kwamba kama taifa tumevushwa na mashujaa kuelekea katika jamii yenye haki, na wakati wote CHADEMA imevuka hatua kama chama cha siasa na sasa inasimamia haki.
  4. Rangi nyeupe iko mbele ya rangi zote kama ishara kwamba chama kinatanguliza UKWELI NA UWAZI katika nyanja zote. Pia rangi nyeupi imebeba nembo ya chama kwa kuwa UKWELI NA UWAZI ni misingi muhimu sana kwa chama. Nembo ya chama iko mbele kama kama ishara ya CHADEMA kuwa chama kiongozi katika kuchochea misingi muhimu katika kuleta mabadiliko na maendeleo katika Taifa.
  5. Rangi zingine zinatenganishwa na ufito mweusi ambao unaumbo la "T" ikiwasilisha kifupi cha jina la taifa la Tanzania.
Rangi za Bendera
NYEUSI

Rangi hii inawakilisha WATU WA TANZANIA. Hii ni rangi ya wazawa asili wa nchi yetu. Ni rangi ambayo inabeba pia falsafa ya NGUVU YA UMMA.
BLUU ISIYOKOZA (LIGHT BLUE)
Hii ni rangi ya asili ya CHADEMA. Ni rangi ambayo inawasilisha HAKI. Lakini pia rangi hiyo inawakilisha BAHARI kama ishara ya maliasili/raslimaji na Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar.
NYEUPE
Rangi nyeupe inawasilisha UKWELI, UWAZI na AMANI. Huu ni msingi muhimu wa CHADEMA. CHADEMA ni chama ambacho kitasimamia uadilifu kwa njia ya demokrasia.
NYEKUNDU
Rangi nyekundu inawakilisha MASHUJAA. CHADEMA inathamini historia ya nchi yetu ambayo inawasilisha kumbukumbu ya mashujaa waliotupitisha katika michakato ya mbalimbali ya demokrasia na maendeleo ikiwemo harakati za kuondoa ukoloni. Rangi hii ni chimbuko la uzalendo wetu.
 
Asante kwa ufafanuzi mzr ndg yangu wa Ileje... yaani umenyoosha vilivyo... hongera sana japo cjui Kama ww ni team mabadiliko au lah
 
Hii hapa
Mawe%20Rashidi%2C%20profile%20picture_20200607_2.jpeg
 
Rangi nyekundu inaashiria umwagaji wa damu. Ndio maana akina Lema na Mbowe wanapenda sana kutishia umwagaji wa damu kila mara wanapoongea.
 
Back
Top Bottom