Tatizo kubwa lipo kwenye jamii sio vijana.. yani kijana akimaliza chuo akaendesha bodaboda au kufanya Kazi ya saidia fundi watu wengi huanza kusema vibaya kumchukulia kama kitendo cha kwenda shule alipoteza muda.. na hakuna maarifa aliyo yapata ya ziada tofauti na walio baki mtaani hii kitu sio kizuri kwenye jamii yetu, na ndo kimefanya vijana wengi wajifungie majumbani.
Yani ili nchi iendelee inatakiwa tujifunze kuwasifia watu wanao kujituma kufanya Kazi kwa bidii hata kama ikiwa ni Kazi ya kuzibua choo.. na kingine pia tujifunze kwa nchi zilizo endelea.
Jamii yetu inaona kama mtu ukimaliza kusomea Uhandisi ukaenda kulima au kujiajiri katika fani tofauti unakuwa umepotea.. kwa mtazamo wangu kitu kikubwa kinacho kwamisha vijana ni majungu kutoka kwenye jamii.
Mfano niulize tu.. ni wazazi wangapi wataruhu mwanao aliesomeshwa kwa gharama mpaka chuo akawe bodaboda,saidia fundi, au hata kuwa mpishi mgahawani?? Wazazi kama mpo humu naomba mjibu kwa uwazi kabisa