Mimi nimekaa naangalia wazee wenzangu na vijana wa kileoAiseee, Mkuu asante kwa kuanzisha huu uzi, umenikumbusha mbali sana, wakati huu mziki ulikua mtamu sana.
Niliangalia dicumentary ya maisha yao wakiwa ABBA. Walikuwa couples na kazi ya wanaume ilikuwa kutunga nyimbo na wanawake kucheza na kuimba. Wanaume waliitikia vibwagizo na kupiga piano. It was the real meaning of team work.i am reliably informed that ABBA have been re-united and they expect to release their first song by december 2018. tusubiri kuviona vibibi (Agnetha na Anni-Frid) na vibabu (Bjorn na Benny)
Wale Wa enzi hizo tuliopenda miziki ya Zaire aka Bolingo ,Cavasha unatusaidiaje tukumbuke enzi. Kiingereza nakijua kiasi ila frankly speaking wazungu wakiimba sisikii maneno yao isipokuwa wachache kama Celine Dion, Shakira na wengine wachache. Lingala siielewli lakini nyimbo zao ziliniteka miaka hiyo. Kulikuwa na imani miziki ya kizungu ilikuwa ya wachaga ,sababu take sijui labda ndio wasomi Wa enzi hizo. Lakini nadhani ni matter of interest , tulivyochukia ubepari hadi utamaduni wao tukauchukia, hatukutofautisha. Weka na Bolingo nzuri za enzi hizo if you don't mind.
Dada huu wimbo unanikumbusha DJ Rujual kwenye harusi ya vijana fulanibTanga bwana harusi alikuwa uhamiaji na bibie alikuwa posta ndio ulikuwa wimbo wa kuwaingiza ukumbini duuh