Yona F. Maro
R I P
- Nov 2, 2006
- 4,202
- 218
Miezi Michache iliyopita nilianzisha Blogu ya kutangaza na fasi za kazi East African Career and Job-Hunting Blog imekuwa hewani kwa muda mfupi kidogo na imepata mafanikio makubwa haswa katika matangazo na secta zingine zinazohusu mtandao huo nashukuru wote kwa wale ambao kwa namna moja au nyingine walinipa moyo wakati ule nakumbuka wa kwanza ni Jackson mbogela ( mwaka huu sijamsikia sijui yuko wapi )
Wakati nimeanzisha na kuendeleza vitu kadhaa nilifikiri watanzania wanahitaji sana ajira , wanahitaji sana nafasi hizi pamoja na mengine mengi yaliyokatika blogu hiyo , muda ulivyozidi kwenda nikagundua mawazo yangu sio sawa kabisa kuna vitu zaidi watanzania hawajui , au labda hawajafundishwa au sijui kuna tatizo gani
Blogu hiyo niliiunganisha katika mtandao wa blogu za kiafrika katika afrigator pia nikaunganisha katika mtandao wa blogu za Kenya katika kenyaunlimited , kila siku Napata email karibu 200 na zaidi kutoka kwa wakazi wa afrika mashariki asilimia 90 kati yao ni wakenya wengine ni Rwanda huko , na wengine walio katika nchi za mbali ila wanapenda kuja kufanya kazi nchini Tanzania
Inasikitisha sana pamoja na kwamba magazeti na idara za serikali zinatoa nafasi nyingi za kazi na kuzitangaza muamko wa Tanzania haswa vijana umekuwa mdogo sana katika kuchangamkia nafasi hizi wengi wanaochangamkia ni wa nchi za jirani haswa Kenya wako shap sana na waelewa sana mtu yuko radhi kuagiza gazeti kutoka dar kwenda Nairobi kupata nafasi hizo za kazi .
Watanzania haswa vijana wanatakiwa waelewe nafasi waliyonayo sasa na huko mbeleni haswa tunapoingia katika mambo ya afrika ya mashariki soko letu la ajira linajaa watu wengine badala ya sisi , wajukuu zetu sijui watakimbilia wapi
Naamini katika ajira hakuna kupendeleana kama wengi wanavyodhani na kuaminishwa hivyo na baadhi ya makundi ya jamii .
Mchana mwema