Vijana tusing'ang'anie Dar

Vijana tusing'ang'anie Dar

Mm sjawahi ielewa Du salaam yale maisha ya kugombania kila kitu sio wazee wala vijana
 
Hodi wadau, mimi ni mgeni kiuanachama ila ni mwenyeji kiusomaji. Leo Nina hoja yangu. Kama takuwa nimewakwaza watu samahanini sana, hoja yangu ni hii,

Kuna maisha nje ya Dar, huku mikoani kuna fursa za kutosha kwa mfano ukibahatika kufika Mpanda unaweza kushangaa vijana wadogo wanavyovuna mahindi na mazao engine.

Dar maisha magumu sana hasa kwa wale hali ya chini. Huko hewa yenyewe ya kugombania.

Watu hawalali wanakesha kwenye magari. Yani mtu saa kumi lazima uwe umeamka.

Joto, foleni, kelele yani watu wanastress balaa ukimgusa hata kwa bahati mbaya atawaka balaa.

Kwa leo naishia hapa karibuni Mpanda Kalila tulime mpunga.
Kilimo ni kamari
 
Mwisho wa siku tukubaliane tu, pesa inavyopatikana Dar ni tofauti mno na upatikanaji wa pesa kwa sehemu nyingi za nchi hii. Mfano, kwa sasa mihogo Dar es Salaam imekuwa ni biashara kubwa mno inayolipa vizuri kuanzia kwa wauzaji sokoni mpaka kwa wanaoichoma sasa nipe mrejesho wa mkoani katika ufanano huo.

Wacha tutafute mitaji kwanza hapa mjini, huko tutakuja tukiwa na mitaji ya kueleweka ila Dar wacha pawe hivyo hivyo tu.
 
Hodi wadau, mimi ni mgeni kiuanachama ila ni mwenyeji kiusomaji. Leo Nina hoja yangu. Kama takuwa nimewakwaza watu samahanini sana, hoja yangu ni hii,

Kuna maisha nje ya Dar, huku mikoani kuna fursa za kutosha kwa mfano ukibahatika kufika Mpanda unaweza kushangaa vijana wadogo wanavyovuna mahindi na mazao engine.

Dar maisha magumu sana hasa kwa wale hali ya chini. Huko hewa yenyewe ya kugombania.

Watu hawalali wanakesha kwenye magari. Yani mtu saa kumi lazima uwe umeamka.

Joto, foleni, kelele yani watu wanastress balaa ukimgusa hata kwa bahati mbaya atawaka balaa.

Kwa leo naishia hapa karibuni Mpanda Kalila tulime mpunga.
Dar vijana wengi wanapoteza muda sana wakija kushtuka umri umeenda!...akiwa na kigeto na friji basi maana bia za bure dar zipo sana!...

Sent from my SM-A037F using JamiiForums mobile app
 
Sasa kuna vijiji hata hicho chumba tu cha kupanga hupati! Bei za vitu vidogoo kama viberiti/chumvi zipo juu! Huduma muhimu za jamii hakuna! Vyakula hakuna, vikiwepo ni aina moja tu mnagombania kijiji kizima! Ulevi wa pombe ni vijana wote kijiji kizima tena mnalewa na kuongea kilugha kabisa! Hiyo tv ya 32' na sabufa ya sundar unaikuta kwa mwenyekiti wa kijiji au mwalimu mkuu tu, yaani hao ndio madon wa kijiji. Huduma zinatolewa kwa kujuana.. Hapana tutang'ang'ana mjini mwanzo mwisho!
 
Vijana wote vijijini wamepambana na wametoboa? Hawahawa ambao tukishuka stendi kuwasalimia wazazi na bibi zetu wanaitana na kupigiana simu kujulishana.

Hawahawa ambao msimu wa sikukuu ndio wanafurahia maana wageni kutoka Dar ndio watakuja kukarabati nyumba za wazazi wao, kujenga, kununua mifugo yao kuchinja na kuongeza mzunguko wa hela?

Meanwhile hapa Dar kuna stendi ya Magufuli inamwaga makumi ya maelfu jijini kila siku lini uliwahi sikia watu wa Dar wanashangilia kwamba watu wa Kinampanda ya Singida wamekuja.

Mnavyosema vijijini watu wana hela utadhani Dar nzima maskini, kwa taarifa yenu kila mtaa wa Dar una angalau billionaire mmoja labda nje ya mji ambapo mtaa hauna kaya hata 50. Hakuna mtaa Dar unakosa walau jengo la thamani ya 200M, uko Kinyala, Mbeya nako ni hivyo .

Dar inalipa kodi kama 80% ya nchi nzima, Dar ina 10% ya population ya nchi nzima wakati inazidiwa ukubwa na wilaya kibao za mikoa. Yaani tuondoke mkoa unaolipa zaidi ya trilioni 11 kwa mwaka kama kodi, tuje Katavi mkoa ambao hata bilioni 10 kwa mwaka haifikishi?
Ukie da Kijijini kwa mtu ulie kaa dar lazima utaona fulsa labda kama utakua kijana wa ovyo na ukipambana lazima utoke lakini hapa vijana wengi hawajajipata wapo wapo tu wachache ndo wamejipata
 
Aikoooooooo! wa taarifa yako waliopo dar ni Staff wa JF tu wengine tupo live mikoani, karibu Kabanga, Ngara 🤣
Huko kabanga ndio naambiwa ni kitovu cha parachichi mzee?
 
Bila shaka umeleta uzi baada ya vijana kadhaa wa daslam kulalamika hali ngumu.

Sio hawataki kuja ila kuja bila kitu nacho kipengele.
Ngoja watafute nauli, watakuja.
 
umeongea jambo la maana sana na la msingi mno 🐒

jamaa mwaka wa 14 kang'ag'ana dar kazini mshahara la5 kwanza kabisaa haumtoshi, kodi kachumba kamoja kadogo kichizi, hawez nunua kiwanja wala boda boda akati vijana wadogo tu kijijini kwa kilimo na biashara wana mijumba na mahekalu ya hatari huko kijijini ana watoto wa kuzaa kama wote 🐒

town ni kupigwa jua tu na kujipoaza na kahawa baadae jioni 🐒
Nimeingia Njombe Jana Usiku nikitokea huko "mikoani". Nitakuwepo kwa siku kadhaa kwa shughuli fulani ya kikazi.

Leo nimepata nafasi ya kutembelea maeneo kadhaa yanakolimwa maparachichi. Nilijikuta nahisi kama nataka kulia, si kwa huzuni, bali furaha. Hii nchi imebarikiwa sana. Hali ya hewa ni nzuri sana kwa kilimo. Nimekutana na watu kadhaa wanafanya kilimo cha parachichi, wengine ni mamilionea wanaolekea kuwa mabilionea.

Jamani nchi hii ina utajiri mkubwa sana.

Inawezekana kuwa bilionea Tanzania.

Hii nchi ni tajiri mno. Ukijipanga vizuri, na ukaamua kuwekeza kwenye kilimo biashara, ni suala la muda tu, unajikita umeshakuwa bilionea.

Nitaondoka Njombe hivi karibuni, lakini nitarudi tena. Ni sehemu sahihi kuwekeza kilimo cha parachichi.
 
👊 for sure kua tajiri au maskini ni uchaguzi na uamuzi wa mtu tu, fursa zipo nyingi na zipo wazi kabisaaaa kama ivo yaani 🐒
 
👊 for sure kua tajiri au maskini ni uchaguzi na uamuzi wa mtu tu, fursa zipo nyingi na zipo wazi kabisaaaa kama ivo yaani 🐒
Nimefika maeneo mengi Tanzania. Ni mikoa miwili tu, Lindi na Mtwara ndiyo bado sijatia miguu yangu. Huenda nikaenda huko wiki ijayo.

Lakini kwa niliyoyashuhudia Njombe, nakuhakikishia sihami Tanzania ng'o. Bilioni yangu ya kwanza nitaipata nikiwa Tanzania.

Nitaondoka Njombe siku chache zijazo, lakini nitarudi tena kuja kuwekeza kwenye kilimo cha parachichi na mifugo.

Nikiwa na alau ekari 50 za parachichi, ng'ombe 20 wa maziwa, na mbuzi 100, ni mwanzo mzuri. Lakini lengo ni kuwa na ekari 200 za Parachichi aina ya Hass.

Njombe, nitarudi kuja kuwekeza!

Tanzania ni nchi nzuri sana. Si bure ndugu zetu Wakenya wanapatamani!

It's possible kuwa bilionea Tanzania!
 
Hayo magunia utawaona wenzio wakivuna tu.kalime wewe uone
 
Hayo magunia utawaona wenzio wakivuna tu.kalime wewe uone
Mkuu, unazungumza nami?

Sijayaona magunia, nimeyaona matokea ya yanayofanyika Njombe kwenye kilimo cha parachichi. Kwa sababu hiyo basi, na mimi nitawekeza, siyo kwa ajili ya kuyaona magunia, bali kupata matokea mazuri.

Nitalima, na nikianza kuvuna, nayapaki kwenye vifungashio stahiki na kuyasafirisha kwenda "ng'ambo"

Nitayanunua pia na kuyafanyia packaging kabla ya kuyaexport.

Mkuu, wewe hutaki kuwa bilionea?

Fursa za ubilionea zipo nyingi sana Tanzania.

Tembea ukifikiri, utaligundua hilo.
 
Kila la kheri
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom