Vijana tusing'ang'anie Dar

Vijana tusing'ang'anie Dar

Sehemu kubwa ya mada yako umeishia kuponda Dar badala ya kueleza hizo fursa unasema vijana wanavuna mahindi!
Mimi nimezaliwa Dar na kukulia DSM maisha yangu yapo hapa japo kuna muda niliwahi kutoka nje ya mkoa ila mpaka sasa hakuna mkoa unaosegelea DSM kwa fursa. Pia ukiishi DSM una asilimia zaidi ya 70 kufaulu tofauti na mikoani ambapo ili angalau uingize elfu 10 tu kwa siku utamenyeka vibaya sana. Ukishindwa kufanikiwa DSM basi jua mikoani ni unaenda kucheza bahati nasibu labda uwe umezaliwa huko.

Nimewahi kuishi mikoa hii

1.Songea
2.Mtwara
3.Iringa
4.Njombe
5.Mbeya
 
Ila ki ukweli watu wa dar wanaponda mda tu sasa mtu unakuta anakimbiza miaka 40 anakaa chumba kimoja na ka tv nchi 32 na subwoofa basi anajionaa katoboaaaa bank hana hata mia tigo pesa ama mpesa ana buku 20000.Jamani twendeni vijijini kuna vijana wamepambana na wako njema sana.
Sasa kuna vijiji hata hicho chumba tu cha kupanga hupati! Bei za vitu vidogoo kama viberiti/chumvi zipo juu! Huduma muhimu za jamii hakuna! Vyakula hakuna, vikiwepo ni aina moja tu mnagombania kijiji kizima! Ulevi wa pombe ni vijana wote kijiji kizima tena mnalewa na kuongea kilugha kabisa! Hiyo tv ya 32' na sabufa ya sundar unaikuta kwa mwenyekiti wa kijiji au mwalimu mkuu tu, yaani hao ndio madon wa kijiji. Huduma zinatolewa kwa kujuana.. Hapana tutang'ang'ana mjini mwanzo mwisho!
 
Saa 10 uamke uende wapi? Acha kukariri maisha!
 
Ila ki ukweli watu wa dar wanaponda mda tu sasa mtu unakuta anakimbiza miaka 40 anakaa chumba kimoja na ka tv nchi 32 na subwoofa basi anajionaa katoboaaaa bank hana hata mia tigo pesa ama mpesa ana buku 20000.Jamani twendeni vijijini kuna vijana wamepambana na wako njema sana.
Vijana wote vijijini wamepambana na wametoboa? Hawahawa ambao tukishuka stendi kuwasalimia wazazi na bibi zetu wanaitana na kupigiana simu kujulishana.

Hawahawa ambao msimu wa sikukuu ndio wanafurahia maana wageni kutoka Dar ndio watakuja kukarabati nyumba za wazazi wao, kujenga, kununua mifugo yao kuchinja na kuongeza mzunguko wa hela?

Meanwhile hapa Dar kuna stendi ya Magufuli inamwaga makumi ya maelfu jijini kila siku lini uliwahi sikia watu wa Dar wanashangilia kwamba watu wa Kinampanda ya Singida wamekuja.

Mnavyosema vijijini watu wana hela utadhani Dar nzima maskini, kwa taarifa yenu kila mtaa wa Dar una angalau billionaire mmoja labda nje ya mji ambapo mtaa hauna kaya hata 50. Hakuna mtaa Dar unakosa walau jengo la thamani ya 200M, uko Kinyala, Mbeya nako ni hivyo 😂.

Dar inalipa kodi kama 80% ya nchi nzima, Dar ina 10% ya population ya nchi nzima wakati inazidiwa ukubwa na wilaya kibao za mikoa. Yaani tuondoke mkoa unaolipa zaidi ya trilioni 11 kwa mwaka kama kodi, tuje Katavi mkoa ambao hata bilioni 10 kwa mwaka haifikishi?
 
Maisha ya Watu wa Dar ajabu wa Mikoani ndo wanaumia, kila siku nyuzi za Dar hivi, Dar vile, sema mnatamani kuja Dar ila pa kufikia ndio hamna, pyeeeeeeeeee!
 
Kwa Mtu Ambaye Amekaa Dar Es Salaam Pekee Hawezi Kuelewa.

Ila Kama Unatoka Na Kurudi Dar Es Salaam Kuna Time Unaona Kabisa Dar Es Salaam Si Mji Wa Kuishi.

Watu Wanaoishi Nje Ya Mji Huu Kiukweli Ndio Wanaishi.
Kuweni serious wakuu, Dsm na changamoto zake huwezi kulinganisha na sehemu nyingi za mikoani

Hivi ukitoka kibaha Hadi Morogoro mjini, Morogoro mjini hadi Dodoma; sehemu nyingi ni za ovyo na sehemu nzuri ni chache mno


Watu mnaosifia mikoani mnakaa sehemu zilizo za mjini



ila huwezi ukakaa ndani ndani uanze kusifia mkoani
 
Maisha ya Watu wa Dar ajabu wa Mikoani ndo wanaumia, kila siku nyuzi za Dar hivi, Dar vile, sema mnatamani kuja Dar ila pa kufikia ndio hamna, pyeeeeeeeeee!
Mikoani kule kwenye vibanda vya nyasi kibao?

Gari la kwenda mjini ni moja tu tena linapiga route moja tu Kwa siku


Wanadhani watu waliopo Dsm hawayajui maisha ya huko wakati wametokea huko huko
 
Mnadhani watu hatujawahi kuishi huko vijijini?

Acheni uongo hakuna hayo maekalu mnayoyasema, hao hao wa vijijini ndio wanaoongoza kukimbilia Dsm.

Hao watu wa kijijini ndio Kila siku wanatupiga virungu wakiaminj huku tumetoboa

Mafanikio ya vijana wachache usifanye yawe ya vijiji vyote


Hata huku Dsm Kuna vijana Wana maisha mazuri
unaona aibu kurudi kijijini na mvi, kipara na stress za ajira na maisha kama zote, umri umeenda huku huna mke, huna mtoto wala kaploti 🐒

na digrii yako jamaa wa darasa la saba ulo waacha kijijini ndio vibopa wana pesa chafu, mahekalu ya nguvu we unapiga myayo hujui ata pa kuanzia 🐒

uskate tamaa, fursa bado unayo.
Ni kuamua na kujipanga tu 🐒

kwa Neema na Baraka za Mungu yote yanawezekana wakati wowote 🐒
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom