Vijana tunakosea wapi siku hizi?

Captain mopao

Senior Member
Feb 25, 2021
134
500
Habari ndugu wananchi,

Kidumu Chama cha Mapimduzi😎

Kuna jambo moja hua nalifikilia sipati jibu.

Kipindi nazaliwa namkuta maza tayari ana mashamba makubwa ana viwanja ana mifugo ana asset kibao.

Mzee alikua kaoa mitara so home kwetu hakua ana deal napo sana.

Mama yetu ni mkulima, yaan akisimama shambani mvua ije itanyesha itakatika haachi jembe sisi wanae hatuna kipaji cha kulima saana
Ijapo katuachia spirit ya kupambana katika mazingira magumu maana kuna kipindi alikua anaponda kokoto tupo naye kwenye kuchunga ng'ombe ingawa tulikua tunamsaidia kipindi cha likizo na weekend.

Kuna siku nilikaa nikatafakali nikajiona sipo serious na maisha nikamuuliza mama, umri gani wewe ulianza kua na mifugo, mashamba na kununua viwanja?

Akanitajia umri ambao nipo nao sasa mimi hapa nikijitathimini kiwanja ninacho kimoja tu, nilichonunua kwa pesa yangu kitu kingine nachomiliki ni tv subwoofer vyombo na kitanda.

Hili jambo liliniumiza sana kichwa but nikipiga mahesabu hapa mtaani wapo vijana walionizidi umri wanakaa kwao hawawazi maisha ya kuijtegemea.

Sana sana wanangoja urithi. Unakuta mtu kaoa kbsa anapishana chumba na baba yake.

Kwanini zama zetu ipo hvyo maana ukifatilia ata kwa familia nyingine utakuta baba yako alivoku na umri wako alikua ameshaanza kujitegemea na alikua na ngombe na mbuz still wewe unachomiliki ni smartphones tu.

Sijui vijana wa zama zetu tunakwama wapi au tunachelewa shule au uvivu umetutawala hiki kitu kwangu mimi hua kinaniuma sana.

Hiv shida gani ipo hapa kwetu vijana.

Asaaanteni
 
Captain mopao

Senior Member
Feb 25, 2021
134
500
Wao miaka hiyo walikuwa wanaingia polini tu na kujichagulia maeneo sio sasa hiv.
Ni kweli lakini ata vijijini kwenye mapori ambako vijana wanaweza kufyeka hawafanyi ivo nimelima manyara kijiji flan iv lakini cha ajab wanaolima kule mashamba makubwa ni watu kutoka mjini vijana hawajishughulish kbsa nikakuta kuna jamaa kaweka pool table, unajua wanakesha hapo mpka asubuh wanacheza
 
SN.BARRY

JF-Expert Member
Oct 12, 2012
3,532
2,000
Ukiona mtu anakaa kwao au hana kazi unaweza kumuona au kumhisi mvivu asiyependa kujituma. Fursa zikifungwa hata ufanye nini hutoboi.

Zamani ukija Dar hata ukisema ukaange mihogo au ufungue goli la chipsi au kitimoto unatusua maisha. Sasa hivi haiko hivyo watu hawana hela. Fungua banda la chipsi utakula mwenyewe.

HALI NI NGUMU HATA KAZI ZA VIBARUA TU HAMNA AU ZIPO CHACHE KULINGANISHA NA IDADI YA WATU WASIO NA KAZI.
 
ProMagufuli

Senior Member
Apr 6, 2021
135
250
Kwa upande wangu naona si suala la kulaumu vijana. Nyakati zinatofautiana.

Now days gharama za maisha ziko juu sana. Kama huna pesa ya kutosha ni vigumu kujiwekeza. Even kijijini bei za mashamba sasa ziko juu na pesa yenyewe kuipata ni taabu tu.
 
Captain mopao

Senior Member
Feb 25, 2021
134
500
Kwa upande wangu naona si suala la kulaumu vijana. Nyakati zinatofautiana.
Now days gharama za maisha ziko juu sana. Kama huna pesa ya kutosha ni vigumu kujiwekeza. Even kijijini bei za mashamba sasa ziko juu na pesa yenyewe kuipata ni taabu tu.
Sawa kaka
 
Kiti Chema

JF-Expert Member
Oct 18, 2017
1,098
2,000
Ukiona mtu anakaa kwao au hana kazi unaweza kumuona au kumhisi mvivu asiyependa kujituma. Fursa zikifungwa hata ufanye nini hutoboi.

Zamani ukija Dar hata ukisema ukaange mihogo au ufungue goli la chipsi au kitimoto unatusua maisha. Sasa hivi haiko hivyo watu hawana hela. Fungua banda la chipsi utakula mwenyewe.

HALI NI NGUMU HATA KAZI ZA VIBARUA TU HAMNA AU ZIPO CHACHE KULINGANISHA NA IDADI YA WATU WASIO NA KAZI.
Nakubariana na mawazo yako mkuu, unajuwa sometime mtu anawaza aanzie wapi anashindwa, unaweza kuwa na mtaji wa kuanzisha biashara lakini ukitazama TRA watakavyo kufuata hata kabla hauja anza jumlisha na ukosefu wa pesa, inauma na umri unaenda bado upo home, unabaki kuchanganyikiwa tu hata huna la kuamua
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom