Vijana tuache huu ujinga

Wazazi wapo wapweke inabidi wachangamshwe...mfn mm bibi yangu anapenda wajukuu kuliko wanawe!

Eish man! Bibi wote kama sio wengi wanapenda sana wajukuu na hilo sio tatizo.

Kinachoongelewa hapa ni ile kwenda kuwaachia na kutelekeza watoto kwao.
Mbaya zaidi hata matunzo na matumizi hauwakumbuki.
 
Sawa lakini hao hao wazee ndio wanaosumbua kuwa wanataka wajukuu wao wawaone kabla hawajafa
 
Acha tuu mkuu ukikuta bibi anaishi mjini hata magimbi ya shambani hawezi kupata ni balaa..
Ninapo ishi hapa mjini, kuna jirani yangu ambaye ni Bibi na babu mmoja..pia wanaishi na binti yao.huyo binti hajaolewa ila kazaa watoto watano hapo nyumbani kwao.Mazingira wanayo ishi ni magumu mnoo,nyumba ni ile ya kizamani mnoo.ina vyumba viwili,kula yao ni ya shida mnoo.huyo mtoto wao hafanyi kazi yoyote,yaan huyo bibi ndo muhangaikaji wa kuwalisha wajukuu.huyo dada ni kuzaa tu yaani.Inaniumiza mnooo
 
Hilo lidada si mlireport walifunge kizazi jamani???? Itakuwa ana matatizo ya akili aisee
 
Zamani vijana walikua wanazaa ili wajenge familia..

siku hizi vijana wanazaa ili watest mbegu kama zina uwezo, vijana wa kike wanazaa ili watest matumbo ya uzazi.

wakishapata majibu ya test zao majukumu ya kulea wanahamishia kwa wengine..

ndo tumefikia hapo.
 
I think people should take responsibilities of choices they make.
Tatizo jamii inawapa sana vijana pressure kwa maswali kama
1. Utaoa lini ?
2. Utaolewa lini ?
3. Una watoto wangapi ?
4. Utazaa lini ?

Kwa maswali ya kifaler kama hayo unakuta watu wanafanya maamuzi yaliyo nje ya uwezo wao ili kuiridhisha jamii inayowazunguka.
 
Kabisa mkuu
 
Oraita!Ombi;Rudisha avatar ya bibie anamnywesha baharia mvinyo kwa gubu.Naipenda sana ile avatar.
Aisee, hujui ni kiasi gani nimehangaika kuipata ile picha....yaani nimeitafuta mnoo, kama unajua sehemu ninayoweza kuipata naomba unisaidie
 

Nakubaliana na wewe kabisa mkuu na sina tatizo na unachokisema.

Sasa ukishafanya maamuzi kwa kusikiliza presha za watu wa nje, jitahidi basi kuwajibikia maamuzi yako mkuu!!!

Watu watapiga kelele tu lakini hawatakusaidia kwa chochote! Mzigo wote unabaki kuwa kwako. Lakini ukilea wanao, nani atakusumbua kwa masimango?
 
Yani mtu usikilize maneno ya watu alafu uje kumtesa mama yako
Too bad.
 
Watu wanatekeleza ushauri wa kufyatua watoto sasa wewe utaka kusema nini na wewe fyatua tu
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…