Vijana na mawazo potofu juu ya CHADEMA

Vijana na mawazo potofu juu ya CHADEMA

Tegemeo Sambili

New Member
Joined
Oct 29, 2013
Posts
4
Reaction score
5
Wapo Vijana Wachache sana Wenye Matumaini Makubwa na Chadema,Wanaamini Kabisa ya Kwamba Kama Chadema Ikichukuwa Nchi,Watanzania Tunaweza Kuishi Kama Marekani au Ulaya Magharibi, Wanaamini Hakutakuwa na Njaa wala shida,Wanaamini Ajira Zitakuwa Nyingi Kama Mchanga wa Bahari,Kutakuwa na Barabara Sitasita Juu na Chini,Wanaamini Tanzania Nzima Inaweza Ikapigwa Cement Hivyo Watanzania Kutokanyaga Vumbi wala Matope,Wanaamini Chadema ndio Chama Pekee Kinachoweza Kupambana na Ufisadi na Ukiukwaji wa Democrasia ndani ya Nchi Hii.Wanaamini Chadema Inawapenda sana Vijana Kuliko CCM na Vyama Vingine vya Upinzani.

Wanaamini Kabisa Kama Chadema Ikipewa Dolla Basi Tutashuhudia Kasi Kubwa ya Maendeleo,Uboreshwaji wa Elimu,Hospitari,Miundo Mbinu ya Maji,Barabara,Reli,Viwanja vya Ndege,Makazi.

Lakini Kabla ya Kuwaunga Mkono Chadema ni Vema Tutafakari Baadhi ya Mambo ya Msingi 1. 1. Hivi ni kwa Kiasi Gani Democrasia Imekuwa na kukomaa ndani ya Chadema?

Maana Kama Zitto Kabwe Anataka Kugombea Uenyekiti,Anaitwa MUHAINI,MSALITI,Anaonekana ni kikwazo cha Maendeleo ya Chadema….na Baadhi ya Viongozi kama Said Arfi,Dr Kitila Mkumbo…Wanalalamika Chadema Kuchaguliwa Viongozi na Mzee Edwin Mtei.

Hivi ni Maendeleo yapi Yamefanywa na Chadema,Ndani ya Chadema Kama Taasisi na Tanzania Kama Nchi yetu Sote?

Maana Chadema Ina Miaka 21 sasa Tangu Kuanziswa Kwake 1993,Licha ya Ruzuku Kubwa na Misaada Lukuki Inayopata Chadema, Viongozi wa Chadema Wameshindwa Kujenga Hata Ofisi ya Makao Makuu ya Chama Chao.Sasa Watawezaje Kuiletea Tanzania Maendeleo?

Chadema Haijawahi Kutoa Hata Msaada wa Madawati kwenye Shule zetu za Kata,Wao Wamekalia Kulalamika na Kushinikiza Kuing'oa CCM Madarakani. 3. 3.Hivi ni Upendo Upi Chadema IInao kwa Vijana Hata Tuiamini na Kuiunga Mkono?

Maana Chadema Haina Utofauti na Wilaya Mpya(Wilaya Isio na Ofisi,Watu wachache sana&#8230😉,Vijana Wanapewa Nafasi za Kugombea Ubunge ndani ya Chadema kwa Sababu Nafasi Hizo Zipo Wazi,Bado Chama Hakina Wanachama wengi, Nafasi nyingi za Kugombea Zipo wazi Kutokana na Uchanga wa Chama Chenyewe.

Lakini na Uchanga Kilionao Tunashuhudia Baadhi ya Viongozi Waking'ang'ania Madaraka,Je Kama Chadema Ikikomaao na Kuwa Kama Ilivyo CCM Kutakuwa na Nafasi ya Vijana Tena??Maana Vijana Kama Zitto Kabwe Wanaotaka Kugombea Uenyekiti Wanaitwa WAHAINI, WASALITI.

Acha Niiunge Mkono CCM,Maana WAMETHUBUTU.

Ng'ara CCM Ng'araaa.
 
Ametumwa huyo mwacheni jamani, ila sijui yuko upande wa mishikaki au maneno ya khanga(matamko)?
 
Na kama akili yako ni matope namna hii utakaa sana.

Tumekaa na ccm sasa miaka 37 kila walichokikuta wamekiua kuanzia vya kwae vyenyewe mfano sukita,jengo la kitega uchimi la umoja wa vijana nk.

Pia wametafuna reli,atc,viwanda vyote,mashamba ya umma,vyama vya ushirika,azimio la arusha,miiko ya uongozi,nyumba za srikali wameuziana viongozi,deni la taifa kulilipa mpaka tuuuze mkoa wa kigoma nk.

Sasa kwa akili yako tunapoiona chadema ni kama mkombozi na ni kama kuanza chekechea yenye matumaini ili kuelekea primary,o level,a level na hatimaye tupate digree ya maendeleo sisi ni wajinga?

Ccm tuliiamini nayo ikatuaminisha inaweza kutupa digree tukiwa darasa la kwanza lakini miaka 37 imeisha wamekula mpaka ubao wa kuandikia wamelamba chaki na hata viboko vya kuwaadhibia watukutu(miiko ya uongozi)wamekula tuwaeleweje?

Kama ingekuwa jeshini wewe ungekela risasi maana tumeingia aruwa wewe unataka kuturudiasha mutukula.
 
umeandika vizuri sana. mawazo yako yanashabihiana na mawazo ya wanachadema wengi
 
CCm badilisheni jina mkitaka kuendelea kutunyonya.

Tunataka jina jipya ndo mana tunaitaka CDM, hata kama watakua wanyonyaji zaidi yenu, kwani baada ya miaka 5, tunaipiga chini.

Sasa nyie ccm mnataka mtutawale miaka mia moja na ngapi ndo mridhike?
 
Nikweli wamethubutu kuuza nchi wameweza na sasa wanasonga mbele kuuza gesi mafuta uranium na kudidimiza elimu
 
Nani kakwambia watu wanawaza hayo uliyowaza ww, yani akiliyako mgando enye ukakasi unajifanya kuhisi watu ndo wanafikiri hivyo, kwanini usiulize malengo ya CDM n nini na mipangoyake ni nn. acha kutumia akili ya m.su.k.u.le
 
Mkitukanwa mnalalamika wakati mnataka kutukanwa mda wote ma ccm bwana
 
tatizo lako maccm wakikulambisha mifupa ndo shida. naomba ubadilike la sivyo utakuwa maskini wakutupwa
 
W

Lakini Kabla ya Kuwaunga Mkono Chadema ni Vema Tutafakari Baadhi ya Mambo ya Msingi 1. 1. Hivi ni kwa Kiasi Gani Democrasia Imekuwa na kukomaa ndani ya Chadema?

Maana Kama Zitto Kabwe Anataka Kugombea Uenyekiti,Anaitwa MUHAINI,MSALITI,Anaonekana ni kikwazo cha Maendeleo ya Chadema….na Baadhi ya Viongozi kama Said Arfi,Dr Kitila Mkumbo…Wanalalamika Chadema Kuchaguliwa Viongozi na Mzee Edwin Mtei.

Hivi ni Maendeleo yapi Yamefanywa na Chadema,Ndani ya Chadema Kama Taasisi na Tanzania Kama Nchi yetu Sote?

Chadema Haijawahi Kutoa Hata Msaada wa Madawati kwenye Shule zetu za Kata,Wao Wamekalia Kulalamika na Kushinikiza Kuing'oa CCM Madarakani. 3. 3.Hivi ni Upendo Upi Chadema IInao kwa Vijana Hata Tuiamini na Kuiunga Mkono?

Acha Niiunge Mkono CCM,Maana WAMETHUBUTU.

Ng'ara CCM Ng'araaa.
Tegemeo Sambili

1. Ni kweli kabisa Zitto ameitw amajina hayo, Je unaweza kuniambiwa Shibuda aliitwa majina gani? je Lowassa, Sumaye, Membe leo wanitwa majina gani huko ndani ya CCM ?

2. Hivi kweli kabisa chama cha siasa kimesajiliwa kwa msajili wa vyama kwa kazi ya kutoa misaada na kugawa madawati?

Hivi chama cha siasa kimekuwa ni NGO ? kusema kuwa kifanye kazi ya kuleta madawati na madawa Hospitali?

Je CCM miaka 37 sasa unaweza kuniambia wamegawa MADAWATI au hata Bomba la SINDANO wapi?
 
Last edited by a moderator:
Tunachotaka ni mabadiliko no matter what! Hata kama tukianza upya sawa! Hatuwezi kutoka analogy kwenda digital tukabaki na chama analogia, hatuwezi kutoka katiba ya zamani kwenda katiba mpya tukabaki na chama cha zamani!
 
Umetumwa ine kuturubuni, kamwe hutoweza shame on you kibaraka
 
Tegemeo Sambili

1. Ni kweli kabisa Zitto ameitw amajina hayo, Je unaweza kuniambiwa Shibuda aliitwa majina gani? je Lowassa, Sumaye, Membe leo wanitwa majina gani huko ndani ya CCM ?

2. Hivi kweli kabisa chama cha siasa kimesajiliwa kwa msajili wa vyama kwa kazi ya kutoa misaada na kugawa madawati?

Hivi chama cha siasa kimekuwa ni NGO ? kusema kuwa kifanye kazi ya kuleta madawati na madawa Hospitali?

Je CCM miaka 37 sasa unaweza kuniambia wamegawa MADAWATI au hata Bomba la SINDANO wapi?

Hivi taasisi kama tamwa, makanisa na misikiti wanaotoa misaada kama hayo madawati ni NGo? Usiwe shabiki wa chama kupitiliza wakati mwaingine ilazimishe akili yako kufikiri
 
Last edited by a moderator:
wapi ulikaa na vijana wakasema hivyo,walikua wangapi,walikua na umri gani,wakutoka maeneo gani,na hadidu rejea zako zilikua ni zipi?
 
Back
Top Bottom