Vijana na mawazo potofu juu ya CHADEMA

Vijana na mawazo potofu juu ya CHADEMA

Endelea kujifariji tu.lakini lakini ukweli ni kwamba ccm ni sawa na mgonjwa anayeishi kwa msaada wa mashine soon CDM itaiondoa.
 
"Kama ningepewa kuongoza nchi ya Tanzania,kwa kutumia BANDARI tu,Tanzania ingekuwa nchi tajiri kuliko nchi zote za Afrika mashariki,na hapo sijaongelea RELI,UTALII na MALIASILI nyingine nyingi zinazopatikana katika nchi hiyo!Nafikiri nchi hiyo inakosa UONGOZI MAKINI tu!"

Paul KAGAME-Rais wa Rwanda
 
wapi ulikaa na vijana wakasema hivyo,walikua wangapi,walikua na umri gani,wakutoka maeneo gani,na hadidu rejea zako zilikua ni zipi?

huku ni kukosa hoja za msingi,kama huna la kuchangia sio lazima utie neno.mmeguswa pabaya enhee?
 
"kama ningepewa kuongoza nchi ya tanzania,kwa kutumia bandari tu,tanzania ingekuwa nchi tajiri kuliko nchi zote za afrika mashariki,na hapo sijaongelea reli,utalii na maliasili nyingine nyingi zinazopatikana katika nchi hiyo!nafikiri nchi hiyo inakosa uongozi makini tu!"

paul kagame-rais wa rwanda

haya maneno hata kwenye khanga yapo,suala ni utekelezaji na si kuongea.kwa kutumia fursa zilizopo nchini mwake tukiondoa hiyo bandari amezitumiaje? Hako kanchi kake si kangekuwa mbali sana kiuchumi? Nenda kafie mbali na muuaji wako kagame.
 
Wewe ni mmoja kati ya vijana wenye weledi mkubwa na kujitambua,una mawazo mapana,unaona mbali na unastahili kabisa kuwa political analyst wa dunia.

Hawataki kuona Misri walikuwa na mawazo mgando kama ya vijana wetu,kuwa Morsi na chama chake cha Muslim brotherhood wangeleta mabadiliko makubwa lakini muda si mrefu wamemuondoa Morsi madarakani na chama chenyewe wakakiita cha kigaidi.

UPINZANI BADO KUONGOZA NCHI. ASANTE MTOA MAADA.
 
Mimi Nafikiri tunahitaji mbadala wa ccm na cdm. Miaka 37 ya ccm wapenda mabadiliko wanasema hakuna kilichofanywa. Miaka 21 ya cdm wameshindwa hata kujenga ofisi ya makao makuu tu ya chama.

Bila shaka tunahitaji majibu stahiki ya hoja za msingi bila kujali imetoka wapi.

Hii biashara ya kuitana majina ya ajabu huku tukiacha hoja za msingi wa maisha yetu zikielea hewani bila majibu sidhani kama ni faida kwetu.

Maoni yangu huyu mtoa mada hajibiwe kama hayo yamefanyika cdm ili watu wawe na uelewa mpana kuhusu vyama vyetu.

Niweke nukta hapa ili niangalie upepo wa wenzangu unaendeleaje.
 
Elimu kwanza. Cdm kimeonyesha kinaweza ndani ya wiki 2 kutoa elimu juu ya mchakato na katiba mpya, wapiga kura na kupiga kura. Kabla ya kugmbea uenyekiti bila kuweka uhuru wa kila mwenyehaki kupiga kura anapiga ni upofu. Hili ndio msingi wa kuelekea kutengeneza tz ya maziwa na asali.

Ccm hata mara 1 haijawawi toa mafunzo hata ya choo bora kwa raia walau kitongoji 1 kwa tz yenye vitongoji maelfu, si bahati mbaya bali kutojua kwa watu kwao ni mtaji. Angalia ni wabunge wa chama gani wanaminywa mawazo yao bungeni? Wanaitwa ndiyooo! Au hujui tofauti kati ya demokrasia na uendeshaji wa kidikteta? Wtz tunaona ni wanani wana uhuru halisia kuwajali na sio wale wenye kudai wanawajali kumbe wanajijali wao na familia zao.

Hakuna demokrasia ijayo bila utaratibu, nidhamu, nk na Zitto anajua. Vinginevyo kila mtu anautashi tofauti na mwingine, ukitimiza utashi wa kila mtz hiyo vurugu huwezi zuia. Cdm kinaonyesha seriousness kinawapa matumaini watz kuliko chama chochote tz. Na wapenzi wa vyama vingine wanakionea inda.
 
Kwa hiyo kipimo chako kikubwa cha kutaka mbadala ni ujenzi wa ofisi ya chama tu?
 
Yani kampeni zote kuhusu katiba mpya tunaelimishwa na tume ya katiba kupitia redio na magazeti na mizandao wewe unatuwaminisha kuwa mi cdm ndio wanaotowa elimu. Sasa hiyo tume ya katiba ya nini iindwe?

Wewe viongozi wa cdm waliona ilitule hela ya cdm tuwandae mikutano kwa kutumia chopa kwa sababu wanajuwa hawaulizwi matumizi wala mapato na mtu ni ndio mzee cdm itakombowa nchi hii si kwakupitia viongozi hawa wakina mbowe na slaa matapeli wakubwa nyambafu
 
Ili kujua mwanao wa kiume kama anauwezo wa kuzalisha mpe mke baada ya hapo utamhukumu. CDM tukiwapa nchi ndiyo tutawahukumu. By the way kama ni kula acha nao tuwape wakale kwani CCM nao si wanakula tu?
 
Semeni yote muwezavyo lkn sisi tumesha amua ni CDM tu. Hata waweke jiwe tutachagua hilo jiwe. Kifupi ni kwamba tumeichoka ccm.
 
Yani kampeni zote kuhusu katiba mpya tunaelimishwa na tume ya katiba kupitia redio na magazeti na mizandao wewe unatuwaminisha kuwa mi cdm ndio wanaotowa elimu. Sasa hiyo tume ya katiba ya nini iindwe?

Wewe viongozi wa cdm waliona ilitule hela ya cdm tuwandae mikutano kwa kutumia chopa kwa sababu wanajuwa hawaulizwi matumizi wala mapato na mtu ni ndio mzee cdm itakombowa nchi hii si kwakupitia viongozi hawa wakina mbowe na slaa matapeli wakubwa nyambafu

Kumbuka katiba mpya ilikuwa ktk ilani ya ccm! Na kuboresha kitabu champiga kura je? Gharama ya demokrasia ni kubwa na demokrasia sio pale kuchagua na kuchaguliwa tu. Demokrasia ipo kila siku na ni mchakato. Kuchagua ni sehemu ndogo tu. Hamna kibaya ktk demokrasia kama kununua kadi ya wapiga kura na kura inapigwa na wachache km 27%. Kwingine mtu kuchaguliwa na wachache hivyo anakataa hiyo post.
 
Mbona mijiccm inajihami sana? Na bado
 
Binafsi sipendi kuongozwa kwa mazoea....CCM must go Nmewachoka hamna mawazo mapya....
 
Wapo Vijana Wachache sana Wenye Matumaini Makubwa na Chadema,Wanaamini Kabisa ya Kwamba Kama Chadema Ikichukuwa Nchi,Watanzania Tunaweza Kuishi Kama Marekani au Ulaya Magharibi, Wanaamini Hakutakuwa na Njaa wala shida,Wanaamini Ajira Zitakuwa Nyingi Kama Mchanga wa Bahari,Kutakuwa na Barabara Sitasita Juu na Chini,Wanaamini Tanzania Nzima Inaweza Ikapigwa Cement Hivyo Watanzania Kutokanyaga Vumbi wala Matope,Wanaamini Chadema ndio Chama Pekee Kinachoweza Kupambana na Ufisadi na Ukiukwaji wa Democrasia ndani ya Nchi Hii.Wanaamini Chadema Inawapenda sana Vijana Kuliko CCM na Vyama Vingine vya Upinzani.

Wanaamini Kabisa Kama Chadema Ikipewa Dolla Basi Tutashuhudia Kasi Kubwa ya Maendeleo,Uboreshwaji wa Elimu,Hospitari,Miundo Mbinu ya Maji,Barabara,Reli,Viwanja vya Ndege,Makazi.

Lakini Kabla ya Kuwaunga Mkono Chadema ni Vema Tutafakari Baadhi ya Mambo ya Msingi 1. 1. Hivi ni kwa Kiasi Gani Democrasia Imekuwa na kukomaa ndani ya Chadema?

Maana Kama Zitto Kabwe Anataka Kugombea Uenyekiti,Anaitwa MUHAINI,MSALITI,Anaonekana ni kikwazo cha Maendeleo ya Chadema….na Baadhi ya Viongozi kama Said Arfi,Dr Kitila Mkumbo…Wanalalamika Chadema Kuchaguliwa Viongozi na Mzee Edwin Mtei.

Hivi ni Maendeleo yapi Yamefanywa na Chadema,Ndani ya Chadema Kama Taasisi na Tanzania Kama Nchi yetu Sote?

Maana Chadema Ina Miaka 21 sasa Tangu Kuanziswa Kwake 1993,Licha ya Ruzuku Kubwa na Misaada Lukuki Inayopata Chadema, Viongozi wa Chadema Wameshindwa Kujenga Hata Ofisi ya Makao Makuu ya Chama Chao.Sasa Watawezaje Kuiletea Tanzania Maendeleo?

Chadema Haijawahi Kutoa Hata Msaada wa Madawati kwenye Shule zetu za Kata,Wao Wamekalia Kulalamika na Kushinikiza Kuing’oa CCM Madarakani. 3. 3.Hivi ni Upendo Upi Chadema IInao kwa Vijana Hata Tuiamini na Kuiunga Mkono?

Maana Chadema Haina Utofauti na Wilaya Mpya(Wilaya Isio na Ofisi,Watu wachache sana…),Vijana Wanapewa Nafasi za Kugombea Ubunge ndani ya Chadema kwa Sababu Nafasi Hizo Zipo Wazi,Bado Chama Hakina Wanachama wengi, Nafasi nyingi za Kugombea Zipo wazi Kutokana na Uchanga wa Chama Chenyewe.

Lakini na Uchanga Kilionao Tunashuhudia Baadhi ya Viongozi Waking’ang’ania Madaraka,Je Kama Chadema Ikikomaao na Kuwa Kama Ilivyo CCM Kutakuwa na Nafasi ya Vijana Tena??Maana Vijana Kama Zitto Kabwe Wanaotaka Kugombea Uenyekiti Wanaitwa WAHAINI, WASALITI.

Acha Niiunge Mkono CCM,Maana WAMETHUBUTU.

Ng’ara CCM Ng’araaa.

Vijana wanaoamini CHADEMA kama mkombozi wao na mkombozi wa Watanzania ni wale wanaliojitoa ufahamu na kubakia kama mtaji wa wapiga pesa, wazee wa fursa.

Wanatakiwa kujua kuwa Mbowe ataendelea kuwatumia katika kutengeneza pesa tu, mwisho atawatupa na kuwaacha kama scrapers.

Viongozi wa CHADEMA hawajawahi kuwa na nia na lengo moja la kumkomboa masikini kutoka katika ugumu wa maisha ya mtanzania. CHADEMA ni sawasawa na CCM.
 
Ccm haikujenga ofisi bali ilijimilikisha majengo yaliyo jengwa kwa nguvu za wananchi enzi za chama kimoja. Hata hivyo ofisi ni majengo tu hayana ishu kwetu CDM inajenga kwenye mioyo ya watu, nyie kaeni na majengo yenu.
 
Back
Top Bottom