Hili Taifa Vijana wangetumia ⅓ ya Akili zao leo hii tungekuwa Taifa kubwa kiuchumi zaidi ya Taifa la Marekani!

UMUGHAKA

JF-Expert Member
Sep 1, 2021
1,881
9,518
Nsikuchoshe na Usinchoshe,tusichoshane!

Ukiona viongozi wa Serikali wana wang'ang'ania wazee kwenye nafasi nyeti tambua ya kwamba vijana watakuwa na matatizo ya kiakili,Vijana wengi waliopewa nafasi ili waonyeshe uwezo wao wamekuwa wapumbavu kuliko hata wazee waliochokaa!.

Hili Taifa la Tanzania ndilo Taifa linaloongoza duniani kwakuwa na Vijana wapumbavu kuliko Mataifa yote yanayotambulika na Umoja wa Mataifa (UN).

Hebu fikiria kijana anatoka nyumbani au kibaruani kwake kuelekea Airport (JKNIA) kumpokea msanii wa muziki wa kizazi kipya kisa kachukua tuzo huko Marekani,na kibaya zaidi huyo kijana anakimbiza gari lililombeba huyo msanii kitokea Airport hadi Kawe!.

Zaidi ya Km 22 huyu kijana anakimbiza gari kutoka JULIUS KAMBARAGE NYERERE INTERNATIONAL AIRPOT (JKNIA) hadi Kawe huku akitokwa jasho na kunuka kama mbuzi wakati huo huo huyo msanii akiwa anapigwa na AC (Air Condition)!.

Nimetafakari sana namna vijana wa nchi hii (Wengi) walivyo wapumbavu hadi nimekosa majibu!.

Hebu fikiria muda ambao huyo kijana kapoteza katika shughuli za uzalishaji mali!.

Kwanini vijana wasitumie muda kama walioutumia leo wakaandamana kuihoji serikali kuhusu ripoti ya CAG? Nilitamani kuona vijana wanahoji wezi wa mali na
wafuja rasilimali zilizotajwa kwenye ripoti ya CAG lakini hakuna anayehoji.
 
Sheria na kanuni za kipambavu zinazoruhusu upigaji kama masilahi ya wabunge, katiba mbovu, matumizi ya anasa ya viongozi n.k zimetungwa kipindi ambacho hao vijana walikua watoto au hawajazaliwa kabisa.

Nyie wazee/wababa mlikua wapi kuandamana zisipitishwe from the first place mpaka mnataka kumrushia kijana mzigo wa kuzipinga?

Mlikua wajinga kuona ubovu? Mliogopa kukinukisha? Hayo maandamano unayotaka vijana tufanye mngeyafanya nyie mliotutangulia leo hii usingekuwepo hapa unalalamika.

Wazee/wababa mmeshindwa kuzuia chanzo cha tatizo kwaiyo hamna uhalali wa kulaumu vijana kwa kushindwa kupambania hayo matatizo yaishe. Actually youths suffer consequences of your ignorance, selfish and cowardness.
 
Hao wazee unao wasemea ndio hawa hawa washenzi wezi na majambazi wanaofilisi nchi Kila kukicha au kuna wengine 🤔🤔🤔 vijana wanao pewa nafasi ni vijana wa mboga mboga ambao wamepikwa na kuandaliwa kua mazuzu na waimba mapambio kwa watawala usilinganishe vijana wote na hao wapumbavu wachache, kua na adabu
 
Nsikuchoshe na Usinchoshe,tusichoshane!

Ukiona viongozi wa Serikali wana wang'ang'ania wazee kwenye nafasi nyeti tambua ya kwamba vijana watakuwa ...
Tanzania izidi nchi ya Marekani kiuchumi?

Hakuna taifa lolote la kiarabu ambalo linaizidi Marekani kiuchumi.

Sasa utakuwa nchi yako ambayo umeme ni wa mgao?

Hao wazee wamefanya nini zaidi ya kuuza nchi?

Tatizo umeandika huu uzi ukiwa na mhemuko sana. Kaa kwa kutulia kisha andika upya
 
Mbona yanga day au simba day sioni threads kama hizi

Mbona sijawahi kuona watu wakiponda watu wanaokesha kuangalia ligi za mpira za ulaya

Au tu watu wakiponda bar kujaa weekdays

Kwa nini ikija sekta ya burudani huwa kuna stigma ilhali hata michezo hususani mpira inapoteza muda vile vile

By the way, pamoja na libya kuwa na rasilimali pamoja na uongozi thabiti wa Ghadafi lakini haikuikaribia marekani zaidi ya kuboresha maisha ya wanachi wake. Hapo bado China na teknolojia, productive population na strong government institutions lakini bado haijafikia. Ndio iwe Tz, umekuza vitu mkuu
 
Tanzania izidi nchi ya Marekani kiuchumi?

Hakuna taifa lolote la kiarabu ambalo linaizidi Marekani kiuchumi.

Sasa utakuwa nchi yako ambayo umeme ni wa mgao?

Hao wazee wamefanya nini zaidi ya kuuza nchi?

Tatizo umeandika huu uzi ukiwa na mhemuko sana. Kaa kwa kutulia kisha andika upya


Hili taifa Vijana wangejitambua wakasimamia Rasilimali Tulizonazo ingewezekana kabisa mkuu!
 
37 Reactions
Reply
Back
Top Bottom