80% ya wazee wetu walishindwa kujitafuta na kujipata

Mwizukulu mgikuru

JF-Expert Member
Oct 21, 2021
4,737
11,096
Ndiyo wakuu, hii ni nyingine tena kutoka kwa Mwizukulu mgikuru ni ukweli usiopingika kuwa kwa sasa vijana wengi tunapitia joto ya jiwe, moja ya mambo yanayotufanya dunia tuione chungu ni hili la wazee wetu, unakuta kijana anahangaika kujijenga lakini bado pia ajenge na kule alipotoka.

Kama haitoshi yeye mwenyewe ajitengenezee vitega uchumi vitakavyo mpa chochote kitu kama nyongeza zaidi ya mapato yake lakini pia wapo wazee wanaoomba nao pia wajengewe miradi au biashara ili wasikae bure, huu wote ni msalaba wa kijana wa sasa na hii inadhihirisha kuwa wazee au wazazi asilimia kubwa walishindwa kujitafuta na kujipata leo wamekuwa mizigo kwa vijana wao.
 
Sasa vijana nanyi mjipange, kwa, ufupi kijana inabidi uandae miradi ya kukupa kipato ili uishi vzr maana kuna uwezekano wa kuishi mpaka miaka 70+, nawaona wazee waliostaafu baada ya kufika 60, bado wanaonekana wana nguvu kama vijana wa 40yrs!! Sasa fikiria, una 60, umestasfu, unategemea pensheni! Haikidhi mahitaji, lazima, utadata tu
 
Wazee hawakuwa na competition.
Ujamaa uliwapumbaza.
Sera ya nyerere iliwatia uoga wa uhujumu uchumi. Hakukuwa na globalization.
Miundo mbinu ilikuwa mibovu hata ukilima huna pa kupeleka, vijiji vilijifungia havikuwa connected kama sasa.
Elimu haikuwa open kama sasa. Sasa ukishindwa maisha huna cha kujitetea.
Wazee wetu walipitia changamoto nyingi sana japo mazingira yalichangia zaidi kufeli kwao.
Vijana wa sasa mna ilaumu sana CCM na serikali na wazee ila wamejitahidi kuwawekea mazingira mazuri kuliko zamani.
Kijana wa mwaka 80 alikuwa anachangamoto nyingi kuliko kijana wa sasa.
 
Ndiyo wakuu, hii ni nyingine tena kutoka kwa Mwizukulu mgikuru ni ukweli usiopingika kuwa kwa sasa vijana wengi tunapitia joto ya jiwe, moja ya mambo yanayotufanya dunia tuione chungu ni hili la wazee wetu, unakuta kijana anahangaika kujijenga lakini bado pia ajenge na kule alipotoka.

Kama haitoshi yeye mwenyewe ajitengenezee vitega uchumi vitakavyo mpa chochote kitu kama nyongeza zaidi ya mapato yake lakini pia wapo wazee wanaoomba nao pia wajengewe miradi au biashara ili wasikae bure, huu wote ni msalaba wa kijana wa sasa na hii inadhihirisha kuwa wazee au wazazi asilimia kubwa walishindwa kujitafuta na kujipata leo wamekuwa mizigo kwa vijana wao.
Saidia wazazi wako acha kutafuta uhalali wa kukacha majukumu

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Kumbuka kuwa, Hao unaodai kuwa walishindwa kujitafuta na kujipata, ndio hao walijinyima na kujibana sana ili wakutunze na kuhakikisha unapata elimu bora. Leo unawaona wamekuwa mzigo. Ama kweli shukrani ya punda ni mateke.
 
Back
Top Bottom