Vijana msidanganywe, ukiwa na pesa utapata mwanamke umtakaye

SEASON 5

JF-Expert Member
Sep 28, 2020
481
1,000
Nimekua nikisoma thread tofauti humu JF za wanaume wakilalamika kuhusu kutendwa na wanawake zao kisa hawana pesa kisa hawana uwezo wakuwahudumia hao wenza wao, nk

Nimeona wengi kwenye comment wakishauri watu watafute pesa sana na kwa bidiii ili kuepuka hayo yote, kila ushauri mzuri ni vyema ukautendea kazi na katika mashauri mengi watu wanayoyatoa mimi niliamuaga kuchukua ule ushauri wa "tafuta pesa kwanza" mengine yote yatakuja.

Vijana wenzangu niwahakikishie muda mzuri wa wewe kutafuta mpenzi/mke/mwenza/mchumba ni kipindi hiki ambacho huna mbele wala huna nyuma huelewi mchana utakula nini wala kesho utatokaje kwenda barabarani, hiki ndio kipindi muafaka kwa jambo lako hilo la kutafuta mwenza wa maisha yako.

Usije ukaacha kunisikiliza mimi mwenzako nasema nina uthibitisho wa asilimia 99.9% kama unataka mke wife material mtafute sasa ukiwa na hali hiyo ngumu hivyo hivyo, wakati unaumiza kichwa usiku ukifika ule nini naomba usisahau kuwaza wapi utapata mke mzuri kwahiyo endelea kutafuta kama ni kutongoza tongoza kama ni kuimbisha imbisha usisubiri upate pesa kama unataka kweli "mke wa maisha yako"

Nyie mnaowaambia wenzenu watafute pesa kwanza kisha mke atafata, mnawadanganya nawahakikishia, wenye pesa hupata wanawake wa kuwachezea na kuwaacha hao wapo wengi, lakini kumpata mke kweli kweli ndugu zangu pesa hai hitajiki.

KWANINI NASEMA HIVI?

Mke kweli hashawishiki na wingi wa pesa zako na tena ukiwa na pesa kumshawishi mwanamke wa kweli kuwa ni kweli unampenda mjomba kibarua chake sio kidogo mama angu mi nawambia.

Real wife material Hashawishiki na magari bro, hashawishiki na hayo mabiashara my brother nawambia hivi kama kweli unataka mke na unataka usije kuchelewa kuoa watu tukakunyooshea kidole, huu muda ambao uko hovyo usisahau msaka wa ubani wako, achana na pesa we msake ataeweza kuishi na wewe ktk hali yako hiyo mbovu kisha msimame pamoja.

Ila ukisimama peke yako, ukawa na pesa ukakamilika kila idara Ishu ya kumpata MKE BORA ni kipengele kitakachokuchukua si chini ya 5yrs, we endelea kuwasikiliza hao wanaokwambia saivi, Tafuta pesa.
 
Haya Mambo yanachanganya Sana, vijana waliobahatika kupata pesa mapema huficha kuonekana Wana fedha ili kupata Mke (mwenye true love) atakaemkubali sio kwa sababu ya fedha zake.

Na wewe unawashauri watafute mke wakiwa hivyohivyo hawana hela. Ili kumpata Mke(mwenye true love) atakaependa bila kushawishika kwa nguvu ya hela.

Yoooote haya Ni katika kumpata mke Mwema.(mwenye true love). Aisee wanawake jitathminini, yaani mnaogopwa hatari.
Kila mbinu inatumika ili kumpata mke mwenye true love.
 
tunapokwambia tafuta pesa hatumaanishi ukipata ndo utafute mke.
Tunakwambia tafuta pesa ili iwe fimbo ya kuwachakata hawa maslei kwini, sio kuoa.
kama unatafuta pesa ili ukizipata ndo uoe, kwa heshima na taadhima nakupa "Pole" maana hisia zako lazima zitapigwa "Dole".

Tuendelee kutafuta pesa ili tukizipata tuwachakate sana..

Anaetaka kuoa, anatakiwa atafute mke pale ambapo anahitaji mke, na sisi tusio na mpango wa kuoa tunasema wacha tuendeleee kutafuta chapaaa ili tuwachape nazo vizuri..
 
20210124_171040.jpg
 
Chini ya Jua ,Pesa inaweza kuletea mwanamke yoyote unayemtaka, ila Haitakaa kukuletea mwanamke mwema.

Lkn pia Bado chin ya Jua, Umasikin utakuletea Mwanamke yoyote unayemtaka lkn hautakaa kukuletea Mwanamke mwema.

Kwann nayesema haya ??


Kwa sababu ,Sio kweli kua Ukiwa na Pesa basi huwezi kupendwa kwa dhati , na sio kweli kua Ukiwa masikin basi ndio utapendwa kwa dhati.


Kuna JAMBO MOJA NALOHITAJI MLIELEWE KWA WANAWAKE..

Hawa viumbe ,hawajawah na hawatokaa kamwee Kujua ni kwann wameamua kua na mtu fulani Kwa dhati !! ... Haraka haraka Jibu lao linabaki kua moja "Ilitokea tu"


Hawa wanawake ni viumbe wanaoishi KIHISIA SANA ...

Unaweza kua Una Pesa, Au ni Masikin ila kwakua wee ni "NICE GUY".. kumpata mwanamke akavutiwa nawewe unabaki kua mtihan kama ilivyo mitihan mingine, nahapi ndo utabaki unajiuliza

Nina gari, nina pesa, nina maisha lkn mbona Yule demu ananikwepa sana????

Au maneno kama, Sawa tu ,unanikataa sababu ya umasikini wangu ,haina shida....n.k ni laana ambazo utaishia kujilaani mwenyewe sababu mwanamke hakutaki.


Hapo hapo ukawa Una Pesa zako au ni masikin tu lkn ukawa na sifa ya "ALPHA MALE A.K.A BAD BOY" , Nakuambia ivi, unaweza wapanga wanawake , Unaweza liliwa na wanawake, yaan unao uwezo wa kuwafanya wakukimbilie na kukuliaaaaaa .


Why??? Kwa sababu ndani ya Alpha/Bad boy kuna Mvuto ambao huwa unatikisa mind ya mwanamke yoyote chin ya jua nakumfanya aamin kua wewe ndio mwanaume unayemuweza.



Hujawah Ona, mwanamke akaamuacha Tajiri nakwenda kwa masikin???

Lkn pia, kuna mwanamke alimuacha masikin na kwenda kwa Tajiri fulan???


Hapa inshu inakua sio Utajiri au umasikin wako,

UKWELI UNABAKI PALEPALE kua ili umuwin mwanamke, ili umfanye akupende kwa dhati, ni lazima uhakikishe umemvutia kihisia nahapa haijalishi una Pesa au Masikin.


HAMNA PESA INAYOMTOSHA MWANAMKE /BINADAMU , NA KWA MAANA HIYO, KAMA MWANAMKE ANGEMPENDA MTU SABABU YA PESA, BASI MKE WA MO DEWJ, ANGEMUACHA NAKWENDA KWA DANGOTE N.K...

VIVYOIVO KAMA UMASIKIN UNGEKUA SABABU YA MWANAMKE KUMPENDA MWANAUME, BASI MASIKIN WASINGEKUA WANAUMIZWA NA MAPENZI

lkn maajabu ni kwamba Wote tunalia. Ama uisikie saut yangu au usiisikie Utalia tuu....


Sasa swali ni Je ,Mwanamke anapenda nini??????.Pesa au Masikin???.



Faida ya Pesa... Pesa inasaidia kutatua changamoto tu za huduma n.k ....

Hii inaamana kua, unaweza mjali kwa upendo wa nje yaa vitu lkn km kwa upendo wa ndan unamfanya ajione Sio mwanamke basi amin nakuambia, wewe na mavitu yako sio bure na atakuliza tu.

Pia, Unaweza kua masikin mzuri tu, akaamua kua nawee, lkn kwakua wee ni masikin jeuri , kakorofi n.k ATAKUACHA TU JOMBA .

Kwahiyo wote mnalizwa na mwanamke.


Kuna jambo najaribu kulifikisha hapa ingawa nmeandika bila mpangilio , ILA KIKUBWA NIKWAMBA, KUA MASIKIN AU KUA TAJIRI, HAKUMFANYI MWANAMKE AVUTIKE NAWEE KWA UPENDO WA DHATI.. ILA, KWA KUA WAO WAMEUMBWA "KUFANYWA WAPENDE" ,BASI WOTE TAJIRI NA MASIKIN WANAYO HAKI SAWA YA KUMPATA MWANAMKE .

Changamoto inakuja hapa,... Wee kapuku utampata wapi mtoto wakishua wakati mtoto wakishua ana sehem zake zakutembelea.
Nawee mwenye Pesa, utampata wapi mtoto wa kimasikin wakati pisi ya kimasikin inasehem zake pia za kutembelea???.

Ndo hapo sasa, inapotokea mmekutana basi chakuamin ni kua unayo nafasi ya kumfanya Hata binti wa JPM awe demu wako bila kujalisha wee una Pesa sana, au ni Masikin sana.


SUALA LA MWANAMKE MWEMA KAMA MKE MWEMA LINABAKI PALEPALE, MKE MWEMA ANATOKA KWA BWANA..... Ndio maana kuna masikin wana mademu namademu zao wanachepuka sanaaaaaaaaaaa... na bado Kuna matajiri pia ,wake zao wanachepuka sanaaaaaaaaaaaaaaa.
 
Hii yote ni kwasababu ya Wanawake hawaeleweki wanahitaji nini. Ukikosa pesa pia unaweza tafuta weee mpaka uchoke,kila kazi unakuta inakutolea nje.
Pia bado ukizipata wanakukataa eti kisa una kisu kikali (Pesa )so wanahisi utakua unakula sana watoto wazuri.
Daah ni asee!
 
Mkuu umenena
Kua na pesa haina maana utampata mtu unaempenda
Ni never never never!!!!!!!
Aise kuna wanadada wanajielewa sana
Ukiwa na pesa utapata haya makuruga kuruga tu yanauopaka mekapu sijui 24hrs
Ila kuna watu pesa ni something else kabisa kwao
Yaani haiwapi shida!

Ukiona umempata kwa pesa basi jua yeye ndio pesa!
 
Hamna kila kitu ni kujifariji kulingana na na Hali ya maisha uliyo nayo , Mwenyezi Mungu amebarki kila level inakuwa satisfied , Kama huna hela kuna type ya wanawake utawapata na ni wife material Kwa level hyo ya kutokuwa na hela, kama Una hela za Kati pia kuna wanawake level hyo na Ni wife material Kwa level hyo ya kipato cha Kati.

Kama Una pesa nzuri pia kuna wanawake level hyo na still ni wife material Kwa level hiyo ya pesa nzur.... Na kila level ina changamoto ya kumpata mwanamke sahihi , (Mapenzi ni chuo Kwa maskini na tajiri pia)

Cha Msingi kila mtu aangalie level yake ,....

NB: Tangu Hawa pale Edeni aliposhawishiwa Kwa kuona tunda lapendeza Kwa macho na linavutia. Tangia hapo wanawake wote wanaathiriwa na kupenda vitu vzuri , wana uvumilivu wa kiwango tofaut hata hvo ikitokea chance ya kupata Jambo zuri analolitaka atashawishika tu.

Hata mke uliye naye pengine kwel ni wife material lakn akitokea mwamba mwenye pesa akataka atumie pesa yake kukuchapia anakuchapia Tu Tena easy , pengne hupat changamoto hyo cse mke wako sio attractive.... Hana mvuto wa kumfanya mwamba mmoja to waste his money...na hvyo mke wako anakuwa special Kwa level ya mwanaume maskini
 
Hamna kila kitu , umeandika utopolo mtupu ,na ni kujifariji kulingana na na Hali ya maisha uliyo nayo , Mwenyezi Mungu amebarki kila level inakuwa satisfied , Kama huna hela kuna type ya wanawake utawapata na ni wife material Kwa level hyo ya kutokuwa na hela, kama Una hela za Kati pia kuna wanawake level hyo na..
kweli umendika point sana
 
Back
Top Bottom