Vijana mnaooa na kufunga ndoa miaka hii, mnakera sana

Vijana mnaooa na kufunga ndoa miaka hii, mnakera sana

Nikioa Mungu akinipa uhai na uzima pamoja na uthubutu nitatoa taarifa ya harusi tu kwa kwel michango now days imekua ni kero na wengine wamefanya ni vitega uchumi,kama hujiwezi unamuolea nani??mwisho wa siku uje kugongewa uanze kuhaha!
 
Ukristo ndio kunachangamoto sn ya hili jambo. .imekua miradi ckuhizi yaani usipotoa unatengwa kabisa bilakuzingatia uchumi waunaemuomba. ..nabaada ya muda flani wanakutafuta ukawatatulie ugomvi wao
 
Unakuta wadau umewachangia kwenye harusi zao fresh tu, halafu ikifika zamu yako hawakuchangii wanakuja na visingizio kibao mara ooooh! Hali ngumu.
Hii inauma sana, mimi nilikuwa hodari kuwachangia marafiki, lakini mtu unampa taarifa ya ndoa hastuki hata kidogo

naenda kuoa mkoani hadi narudi hata kunijulia hali na kunijulia safari na sherehe iliendahe hataki

yaani mchango hatoi na hata kuwasiliana hataki

NIMEJIFUNZA, NDUGU NITAWACHANGIA ILA MARAFIKI WATANISAMEHE
 
Nikioa Mungu akinipa uhai na uzima pamoja na uthubutu nitatoa taarifa ya harusi tu kwa kwel michango now days imekua ni kero na wengine wamefanya ni vitega uchumi,kama hujiwezi unamuolea nani??mwisho wa siku uje kugongewa uanze kuhaha!
Naam kila la heri.Ndoa ni Jambo jema lkn lisigeuzwe kitega Uchumi.
 
Hii inauma sana, mimi nilikuwa hodari kuwachangia marafiki, lakini mtu unampa taarifa ya ndoa hastuki hata kidogo

naenda kuoa mkoani hadi narudi hata kunijulia hali na kunijulia safari na sherehe iliendahe hataki

yaani mchango hatoi na hata kuwasiliana hataki

NIMEJIFUNZA, NDUGU NITAWACHANGIA ILA MARAFIKI WATANISAMEHE
Pole sana mkuu.Hao ndio Walimwengu.
 
Ukristo ndio kunachangamoto sn ya hili jambo. .imekua miradi ckuhizi yaani usipotoa unatengwa kabisa bilakuzingatia uchumi waunaemuomba. ..nabaada ya muda flani wanakutafuta ukawatatulie ugomvi wao
Umesema Kweli mkuu.Mimi Kuna Classmate aliniomba Mchango wa harusi Kipindi nauguza mke wangu nikashindwa kumchangia,aisee Yule Jamaa alikata mawasiliano na mimi hadi leo hii hatuwasiliani.
 
Unakuta lijitu mmesoma nae na wala hakua rafiki Yako Kisa anataka kuoa linakuunga kwenye group SAA zngne ukute hata hakua na namba yako
Hiyo ipo sana,kuna Njemba km tatu hivi zimeniunga Kwenye magroup ya Whatsapp ya Harusi ilihali sikuwahi kuwa na mazoea nao wala kuwa na Namba zao za,simu,Nimewapotezea sitachanga.
 
Ndio maana nimesema si lazima
Unaongea kirahisi ila mchango ya harusi siku hizi imekuwa ni lazima, unasumbuliwa na kudaiwa mchango kama deni vile.

Juzi kati hapa kulikuwa na harusi ya ndugu yangu mmoja wakaweka amount double 100k single 70k.
Kuna ndugu mmoja ambae hayupo vizuri financially, hana kazi yupo hivyo siku zote. Akatafuta 50,000 achangie.. Huwezi amini mchango ulikataliwa.. Na ni ndugu wa karibu sana.
Nilipatwa na mshangao hadi sasa sijaelewa.

Ni kweli sio lazima kuchanga lakini lazima watu waambiwe ili waache tabia mbaya.
 
Wapendwa hbr za jioni?,Poleni kwa majukumu ya siku nzima.Bila kupoteza Muda nianze kwanza kwa ku declare interest kuwa mimi ni Muumini wa dini ya Kikristo,Kanisa Katoliki.Hivyo ninapenda sana Vijana wanaooana kwa kufunga kwanza Ndoa Kanisani au Msikitini,Maana wanatimiza kile Mungu anataka,hivyo ni Jambo la Baraka.

Lakini Kuna Jambo huwa sipendezwi nalo;Unakuta Kijana hajajipanga,Badala yake anategemea watu Wengine ndio wampige jeki, hii si sawa.

Mimi Wakati nafunga Ndoa sikuwasumbua watu,Watu wa Karibu yangu nilipokuwa naishi na kufanyia Kazi walijikusanya wenyewe wakaunda Kamati nami nikaweka Kiasi cha pesa mezani nao wakachangia kuongezea, kimsingi niliwashirikisha tu wale wa Karibu yangu mahali nilipo,wale wa mbali sikutaka kuwasumbua Kwasababu niliona sio fair.

Sasa siku hizi unakuta mtu yupo Mwanza anaomba mchango wa harusi kwa mtu yupo Mtwara,huu ni usumbufu Kwasababu yule wa Mtwara ataombwa Mchango pia na watu wa pale anapoishi.

Jambo la pili linalonikera,unakuta Kijana huyo hakuwahi kukutafuta siku za nyuma ili kujuliana hali,lkn Harusi yake ikishakaribia anakutafuta kukuomba Mchango wa Harusi yake,Hapa na pale utachangia,Sherehe zikiisha,anakata tena mawasiliano unakuta hana muda na wewe Kabisa,hata akisikia unaumwa hawezi kukumbuka angalau hata salamu za pole tu.Kiufupi unakuwa wa Muhimu tu wakati anataka kufanikisha sherehe yake.Huu ni Uchuro mnakatisha sana tamaa.

Tatu ni ishu ya Viwango vya Mchango, Mtu yupo Dar anakutumia Mchango mtu upo Songea kuwa ni Tshs.100,000/=,ili hali anajua fika kuwa hutashiriki na ukijitahidi ukalipa hata nusu yake ataendelea kudai utadhani ni deni, huu ni upuuzi, nikikuchangia Kiasi chochote kwa vile sitashiriki Kwenye sherehe yako,basi tosheka nacho.

Jambo la mwisho linalonikera,utakuta mtu anakuunga Kwenye kamati ilihali upo mikoa ya mbali Kabisa,sasa hivyo vikao vya Kamati utahudhuriaje?,Siku ya sherehe watakupanga Kwenye sekta ipi Wakati hautakuwa eneo husika? Halafu kwanini unipange Kwenye Kamati pasipo ridhaa yangu?.Huu ni ujeuri.

Rai yangu kwa Vijana; Ndoa ni Jambo Takatifu,Sherehe za Ndoa zisigeuzwe kitega Uchumi.Pili Waheshimuni sana wanaowachangia kufanikisha Sherehe zenu za Harusi,msigeuze watu tissue paper Kwamba ikishatumika unaitupa Kwenye dustbin, hii inavunja sana moyo.

Yangu ni hayo tu kwa leo, kama kuna Mwingine amewahi kukerwa km mimi Fall Army Worm Karibu,tuwaonye Vijana.
Utanyooka
 
Back
Top Bottom