The-unknown
JF-Expert Member
- Feb 26, 2014
- 1,702
- 1,980
Na siku hizi hadi ubarikio wanaomba mchango,
Akili ziko kalioni
Akili ziko kalioni
Sawa,jipange kwanza ili kutosumbua watu kwa michango ya Harusi.Hii kitu ya kuoa nitakua wa mwisho kabsa kwa rika langu.
Si ndio hapo!!!.Nilishasema sichangii mtu,matatizo na Raha zao wale wenyewe
Kaamua yeye kuoa Mimi nahusikaje hapo
Badilika sasaKama mimi vile wanisema ndugu
Uzi umejaa ukweli mchungu alafu huyo mke au mume unaempata ni wako sio wetu ujue ....sasa kama uchumi wenu ni wa harusi ndogo sasa mnataka makubwa ya nini?Wapendwa hbr za jioni?,Poleni kwa majukumu ya siku nzima.Bila kupoteza Muda nianze kwanza kwa ku declare interest kuwa mimi ni Muumini wa dini ya Kikristo,Kanisa Katoliki.Hivyo ninapenda sana Vijana wanaooana kwa kufunga kwanza Ndoa Kanisani au Msikitini,Maana wanatimiza kile Mungu anataka,hivyo ni Jambo la Baraka.
Lakini Kuna Jambo huwa sipendezwi nalo;Unakuta Kijana hajajipanga,Badala yake anategemea watu Wengine ndio wampige jeki, hii si sawa.
Mimi Wakati nafunga Ndoa sikuwasumbua watu,Watu wa Karibu yangu nilipokuwa naishi na kufanyia Kazi walijikusanya wenyewe wakaunda Kamati nami nikaweka Kiasi cha pesa mezani nao wakachangia kuongezea, kimsingi niliwashirikisha tu wale wa Karibu yangu mahali nilipo,wale wa mbali sikutaka kuwasumbua Kwasababu niliona sio fair.
Sasa siku hizi unakuta mtu yupo Mwanza anaomba mchango wa harusi kwa mtu yupo Mtwara,huu ni usumbufu Kwasababu yule wa Mtwara ataombwa Mchango pia na watu wa pale anapoishi.
Jambo la pili linalonikera,unakuta Kijana huyo hakuwahi kukutafuta siku za nyuma ili kujuliana hali,lkn Harusi yake ikishakaribia anakutafuta kukuomba Mchango wa Harusi yake,Hapa na pale utachangia,Sherehe zikiisha,anakata tena mawasiliano unakuta hana muda na wewe Kabisa,hata akisikia unaumwa hawezi kukumbuka angalau hata salamu za pole tu.Kiufupi unakuwa wa Muhimu tu wakati anataka kufanikisha sherehe yake.Huu ni Uchuro mnakatisha sana tamaa.
Tatu ni ishu ya Viwango vya Mchango, Mtu yupo Dar anakutumia Mchango mtu upo Songea kuwa ni Tshs.100,000/=,ili hali anajua fika kuwa hutashiriki na ukijitahidi ukalipa hata nusu yake ataendelea kudai utadhani ni deni, huu ni upuuzi, nikikuchangia Kiasi chochote kwa vile sitashiriki Kwenye sherehe yako,basi tosheka nacho.
Jambo la mwisho linalonikera,utakuta mtu anakuunga Kwenye kamati ilihali upo mikoa ya mbali Kabisa,sasa hivyo vikao vya Kamati utahudhuriaje?,Siku ya sherehe watakupanga Kwenye sekta ipi Wakati hautakuwa eneo husika? Halafu kwanini unipange Kwenye Kamati pasipo ridhaa yangu?.Huu ni ujeuri.
Rai yangu kwa Vijana; Ndoa ni Jambo Takatifu,Sherehe za Ndoa zisigeuzwe kitega Uchumi.Pili Waheshimuni sana wanaowachangia kufanikisha Sherehe zenu za Harusi,msigeuze watu tissue paper Kwamba ikishatumika unaitupa Kwenye dustbin, hii inavunja sana moyo.
Yangu ni hayo tu kwa leo, kama kuna Mwingine amewahi kukerwa km mimi Fall Army Worm Karibu,tuwaonye Vijana.
Vijana wanapenda sana kufake Maisha,hawataki kuishi uhalisia wao,mwisho wa siku ni kuwabebesha Wengine mizigo,na kuishia kuwalaumu wale watakaoshindwa kuwasaport.Uzi umejaa ukweli mchungu alafu huyo mke au mume unaempata ni wako sio wetu ujue ....sasa kama uchumi wenu ni wa harusi ndogo sasa mnataka makubwa ya nini?
[emoji16][emoji16][emoji16] hakuna cha harusi mkuu navuta tuishi tuSawa,jipange kwanza ili kutosumbua watu kwa michango ya Harusi.
Hao ukute,wamewachangia sana Wengine kwa hiyo wanaamua kutafuta Sababu ili kufidia michango yao.Halafu siku hizi hadi wazee ( walioko kwenye ndoa) nao wanapita kuomba michango ya harusi zao! Wewe unamiaka 15 au hata mmoja na watoto harusi ya Nini kama sio kugeuza wengine vitega uchumi!
Huo sio mpango wa Mungu.[emoji16][emoji16][emoji16] hakuna cha harusi mkuu navuta tuishi tu
Hao mimi huwa nawapotezea na kuwatupilia mbali.Wengine hawasemi unashtuka umeungwa group la michango whatsaap unsbaki unashangaa tu [emoji23]
Safi,hiyo Nzuri.Maisha magumu bhana.Tena harusi hapan kwa kwel kila mtu ajikune pale mkono wake unaishia Sitoi hela kamwe ikitokea naolewa ntafunga ile ya kwenda kuapa na kwenda geton kwisha habar
Kweli Kabisa,Ushauri Mzuri.vijana wakumbuke kuna maisha baada ya kufunga ndoa anatumia pesa nyingi kwenye harusi anabakiwa hana kitu kwenye akaunti yake ,sa maisha utaya anza vipi na wakati huna kianzio? matokeo yake baada ya ndoa una anza kuwasumbua watu kwa kuwapiga mwiba, mikopo mingi,utapeli mwingi!!?,n.b. fanya sherehe kwa kuangalia balance yako ya pesa na akiba inasomaje itatosha kukuongoza baada ya ndoa!!?