Vijana mnakwama wapi?

Vijana mnakwama wapi?

Vijana wengi wanapishana na magari ya mishahara wenyewe halafu wanawalaumu watu wengine
Ndiyo hapo sasa! Mtu ambaye haoni umuhimu wa kununua hata vocha ya buku ili aombe kazi kesho ndiyo umtegemee aje kazini tena kwa wakati?
 
Vijana wengi wana Utoto mwingi na Umama..hawako serious na Maisha..ile Nidhamu ya maisha hawana..hawajui kutofautisha mazungumzo bila kujali unaongea na nani..Lugha unayotumia kwa vijana wenzako huwezi kuitumia kwa Mzazi,Boss,Kiongozi or yoyote aliekuzidi umri..wacha maisha yawachape kwanza ili akili ikae sawa ndio watabadilika..

Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Ibariki Chakwale
Mungu Ibariki Morogoro
Mkuu nifanyie mpango nipate kazi.
 
Kwa lugha hizi hata kama ulidhamiria kumdhamini lazima uingiwe ubaridi.tatizo linakuja hawajui kuandika kulingana na mazingira text seriously wanaandika kama wapo kwenye magrup ya shule za msingi.
Mnatuonea aisee. Sio wote tupo hivyo mkuu
 
Unakuta kijana anakupigia simu kuomba kazi au msaada fulani. Simu yake inakatika baada ya dakika moja kabla hamjamaliza kuzungumza. Anakutumia ujumbe, "Aisee dakika zimeisha, nitumie namba ya Tigo!". Nani atakuajiri kwa usawa huo?

Au mwingine alikupigia mmezungumza mara moja kuhusu fursa fulani ambayo unaweza kumsaidia au kufanya pamoja, baadae akiwa anakupa mrejesho anaanza kukutumia SMS akitumia lugha kama anazungumza na mshkaji wake tu.

Kwa nini vijana wanachukulia mambo simple sana bila umakini? Halafu mkipigwa chini kwenye interviews na michongo ya pesa mnalalamika hampewi ajira na fursa.
Wamekuxoma xabaxeven
 
Nyie wazee mnaotufanyia mambo hayo mkizeeka wakati sisi tupo kwenye system tunarudisha kikokotoo ili mpate 25% dadadeq.
Sasa hivi si mnaona mmetoboa sababu mliwahi kuzaliwa.. sasa mtazeeka tu na sisi tutaingia kwenye system na yote mnayotufanyia tutalipa..
 
Vijana wengi wanapishana na magari ya mishahara wenyewe halafu wanawalaumu watu wengine
Unakuta kijana anakupigia simu kuomba kazi au msaada fulani. Simu yake inakatika baada ya dakika moja kabla hamjamaliza kuzungumza. Anakutumia ujumbe, "Aisee dakika zimeisha, nitumie namba ya Tigo!". Nani atakuajiri kwa usawa huo?

Au mwingine alikupigia mmezungumza mara moja kuhusu fursa fulani ambayo unaweza kumsaidia au kufanya pamoja, baadae akiwa anakupa mrejesho anaanza kukutumia SMS akitumia lugha kama anazungumza na mshkaji wake tu.

Kwa nini vijana wanachukulia mambo simple sana bila umakini? Halafu mkipigwa chini kwenye interviews na michongo ya pesa mnalalamika hampewi ajira na fursa.
Hayo mambo tulifundishwa kidato cha pili lakini hatuzingatii
 
Acha kuwalaumu vijana kiasi hicho, hata wewe kumbuka kuna watu wanakuona una zingua ila tu wanakustahi/wanakuwa waelewa kwani lawama hazisaidii.

Note: Jifunze kuelewa hali na tabia za watu wa rika tofauti tofauti ndani ya nyakati tofauti. Kunyooshea kidole mapungufu ya rika fulani/mtu fulani hakukufanyi uonekane wewe uko perfect.

Wewe hutowasaidia hao vijana ila tupo tutakao wasaidia kwasababu tunaelewa hali halisi ya hawa vijana wetu.

Acheni complications za ajabu ajabu!
 
Back
Top Bottom