Vijana mnakwama wapi?

Vijana mnakwama wapi?

Kwenu wasomi wa Kiingereza.. unaandikaje "leading" badala ya "reading"? CV inasomeka fluent in both leading, writting and speaking..
We ndo umeandika apo

Alafu kiswahili chenyewe tunakitumia kuongea tu

Kwenye maandishi labda uku JF
 
Vitu gani ivyo
Kiswahili fasaha kwani tunaandika vitabu apa
Mchukue mtu uone ana material gani sio kukosoa uandishii
Wengine tumesoma mavitu hata kwa kiswahili hayatafsiriki alaf unataka niandike kiswahili fasaha kwani ni fasihi andishi hii
 
Wengine tumesoma mavitu hata kwa kiswahili hayatafsiriki alaf unataka niandike kiswahili fasaha kwani ni fasihi andishi hii

Huu ni ujuha ambao majuha wengi hujaribu kujificha wakibanwa, eti oooh mimi sayansi bwana mwandiko kitu gani mara Kiswahili fasaha cha nini.... unavyoandika au kuongea ndio utambulisho wako kwa asiyekujua.
 
Relax mkuu

Naona kama umepanic ilaa kiswahili fasaha tunaongea ila hakina mahali kwenye utambulisho wangu kazini tukija kwenye swala la kuandika

Labda nyie walimu wakiswahili
 
Mother Confessor.. Daaah!! Haujadanganya. Watu tuna wadogo zetu University graduates.. Unakuta maneno kama uxafil "usafiri", uncle nirikuwa tu nakuxarimia, nitajilekebisha, kuangaria, leading "reading".... mtu unaona aibu kuwaunganisha na maboss cz this is a very close reflection of their understanding and attitude which is a true reflection of their performances.
Halafu wakiambiwa ukweli wananuna,.
 
Unakuta kijana anakupigia simu kuomba kazi au msaada fulani. Simu yake inakatika baada ya dakika moja kabla hamjamaliza kuzungumza. Anakutumia ujumbe, "Aisee dakika zimeisha, nitumie namba ya Tigo!". Nani atakuajiri kwa usawa huo?
Au mwingine alikupigia mmezungumza mara moja kuhusu fursa fulani ambayo unaweza kumsaidia au kufanya pamoja, baadae akiwa anakupa mrejesho anaanza kukutumia SMS akitumia lugha kama anazungumza na mshkaji wake tu.
Kwa nini vijana wanachukulia mambo simple sana bila umakini? Halafu mkipigwa chini kwenye interviews na michongo ya pesa mnalalamika hampewi ajira na fursa.
Mkuu ni kweli kuna mwingine alipeleka barua,vyeti na CV kwa ajili ya kuomba kazi alipofika akamkuta boss wa ile ofisi akamwambia "oya boss inakuaje" boss akawa mpole tu akaitikia "poa" baada ya mazungumzo ya hapa na pale boss akachukua zile documents akaziangalia akasema tu poa acha mawasiliano tutakuita hadi leo anasubili kuitwa.
Baada ya kijana kuondoka boss akasema vijana wa siku hizi wana hatari sana lugha za mtaani wamezirasmisha wanazitumia popote bila kujali wanazungumza na nani wala muktadha waliopo.
 
Halafu uandishi wao sasa,."xamahani c* una nmbar ya tigo" "ctoweza kuja nimecherewa uxafili" jumbe za namna hiyo huwa sipotezi muda wangu kujibu,na huyo ndio msomi wa chuo kikuu...mfyuuu!!!
kuna mmoja alinitumia sms "Bos kama hunawezanihunganisha ile diri,fanyahivyo nitakuhachia chochote rife tahiti kitaha" nikasema kweli mwisho wa dunia umekaribia😁
 
Mfumo wa elimu yetu ni janga kubwa.
 
kuna mmoja alinitumia sms "Bos kama hunawezanihunganisha ile diri,fanyahivyo nitakuhachia chochote rife tahiti kitaha" nikasema kweli mwisho wa dunia umekaribia😁

Wengi wenu mmeandika vilevile jinsi hawa mayanki wanavyoandikaga. Itakuwa mnajuana nyie, hahahahha!
 
Halafu uandishi wao sasa,."xamahani c* una nmbar ya tigo" "ctoweza kuja nimecherewa uxafili" jumbe za namna hiyo huwa sipotezi muda wangu kujibu,na huyo ndio msomi wa chuo kikuu...mfyuuu!!!
C* naomba uni push buku 2 kama unayo ya karibu hapo.
 
Halafu uandishi wao sasa,."xamahani c* una nmbar ya tigo" "ctoweza kuja nimecherewa uxafili" jumbe za namna hiyo huwa sipotezi muda wangu kujibu,na huyo ndio msomi wa chuo kikuu...mfyuuu!!!
Hivi Mu....wewe wa rika gani...?? Nadhani natamani nikujue.
 
Yaani shida ya kwake halafu apigiwe? Anakosa hata vocha ya elfu moja?

Ndiyo hapo sasa! Mtu ambaye haoni umuhimu wa kununua hata vocha ya buku ili aombe kazi kesho ndiyo umtegemee aje kazini tena kwa wakati?
 
Back
Top Bottom