Vijana mnakwama wapi?

Vijana mnakwama wapi?

DELETED ACCOUNT

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2010
Posts
9,805
Reaction score
15,470
Unakuta kijana anakupigia simu kuomba kazi au msaada fulani. Simu yake inakatika baada ya dakika moja kabla hamjamaliza kuzungumza. Anakutumia ujumbe, "Aisee dakika zimeisha, nitumie namba ya Tigo!". Nani atakuajiri kwa usawa huo?

Au mwingine alikupigia mmezungumza mara moja kuhusu fursa fulani ambayo unaweza kumsaidia au kufanya pamoja, baadae akiwa anakupa mrejesho anaanza kukutumia SMS akitumia lugha kama anazungumza na mshkaji wake tu.

Kwa nini vijana wanachukulia mambo simple sana bila umakini? Halafu mkipigwa chini kwenye interviews na michongo ya pesa mnalalamika hampewi ajira na fursa.
 
Hii ndio ilinipata majuzi kati kuna bonge job nawatonya vijana wachangamkie naanza kupata sms zao " oyo bloo nimckia kuja kijob au nini mzee wangu nipigishie msele basi nipate pa kujibanza au vp bloo ' hapo mtu ana degree ya computer science
 
Ilibidi uumpe siku nne atengeneze simple ya app ya android alafu akiweza una muunganishia... Alafu usubiri ujionee maajabu wa musa...
 
Vijana wengi wana Utoto mwingi na Umama..hawako serious na Maisha..ile Nidhamu ya maisha hawana..hawajui kutofautisha mazungumzo bila kujali unaongea na nani..Lugha unayotumia kwa vijana wenzako huwezi kuitumia kwa Mzazi,Boss,Kiongozi or yoyote aliekuzidi umri..wacha maisha yawachape kwanza ili akili ikae sawa ndio watabadilika..

Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Ibariki Chakwale
Mungu Ibariki Morogoro
 
Hii ndio ilinipata majuzi kati kuna bonge job nawatonya vijana wachangamkie naanza kupata sms zao " oyo bloo nimckia kuja kijob au nini mzee wangu nipigishie msele basi nipate pa kujibanza au vp bloo ' hapo mtu ana degree ya computer science

Bloo wasaidie wenzako
 
Halafu uandishi wao sasa,."xamahani c* una nmbar ya tigo" "ctoweza kuja nimecherewa uxafili" jumbe za namna hiyo huwa sipotezi muda wangu kujibu,na huyo ndio msomi wa chuo kikuu...mfyuuu!!!
Hii ndio ilinipata majuzi kati kuna bonge job nawatonya vijana wachangamkie naanza kupata sms zao " oyo bloo nimckia kuja kijob au nini mzee wangu nipigishie msele basi nipate pa kujibanza au vp bloo ' hapo mtu ana degree ya computer science
Kwa lugha hizi hata kama ulidhamiria kumdhamini lazima uingiwe ubaridi.tatizo linakuja hawajui kuandika kulingana na mazingira text seriously wanaandika kama wapo kwenye magrup ya shule za msingi.
 
Back
Top Bottom