Vijana; leo nawaibia siri kidogo kuhusu ugumu wa maisha mnaopitia

Vijana; leo nawaibia siri kidogo kuhusu ugumu wa maisha mnaopitia

kalisheshe

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2020
Posts
2,280
Reaction score
4,579
Leo siwapi kila kitu ila nitaendelea kutoa kila nikipata muda

1. Zinaa ( kula/ kuliwa mzigo) ni chanzo no1 kinachokwamisha harakati zako. Kubali, kataa, pinga au andamana ila huo ndio ukweli. Zile hisia za kujilaumu unazozipata baada ya kufanya ngono ni Taarifa ya kukuonesha kuwa kuna kitu cha Thamani kimeondoka kwako.

2. Historia ya familia/ ukoo wenu.
Historia ina nafasi kubwa ya kukuamulia hatima ya maisha yako. Tegemea kuwa vizuri kama historia yenu iko vizuri na Tegemea kuwa vibaya kama historia yenu iko vibaya.

3. Kama historia( background ) iko vibaya. Hutakiwi kufuata njia zilezile ambazo watangulizi wako walizitumia, kuwa wa tofauti, utafutaji wako ufanye kuwa wa aina nyingine kabisa, ingawa hautaeleweka na wengi ila utafanikiwa.

4. Hutakiwi kuiga maisha ya mtu mwingine.
Nasema hivi kwa sababu tumetofautiana kwa kiasi kikubwa mno, na kila mtu kapewa misheni yake tofauti ili aifanye kabla hajaondoka hapa duniani.
Kuna mtu kapewa misheni ya kupitia shida na matatizo ya kila aina ili wangine wajifunze kupitia yeye na kuna mwingine kapewa misheni ya kuishi maisha ya anasa ili wengine wajifunze kupitia yeye.

5. Usihisi uko peke yako katika kundi la wanaogalagazwa na Dunia, mko wengi sana, wapo unaowafahamu na kuwaheshimu, wengine unatamani maisha wanayoyaishi na wengine unahisi wamepata kila kitu ila sio kweli
Wengi wameamua kutulia na kupambana na matatizo yao kimyakimya.

6. Pambana usikate tamaa
7. Usiinue mdomo kuwaambia watu progress yako yoyote labda wawe ni wanaoisaidia hiyo progress.

Kijana mwenzenu
 
Haya
Asante mwana kwetu
20250811_143606.jpg
 
Ile hofu tuliyo pandikiziwa tukiwa wadogo dhidi ya ngono imeleta athari Sana kwenye mitazamo yetu .
Pamoja na kwamba ilikuwa ni busara kupandikiza hofu hio kwa sababu ya athari zake, lakini pia upande wa pili wa athari ni ndio hili ngono kusingiziwa mengi mabaya kila wakati.
 
Mbona wengine wanafanya sana zinas na ndo kwanza wanazid kuwa matajiri hatarii haya mambo ya kufikirika tu kama ww tajiri n tajiri tu na kama ww umeumbwa kuwa maskini utakuwa maskini hata kama hutozini hata siku moja
 
W
Mbona wengine wanafanya sana zinas na ndo kwanza wanazid kuwa matajiri hatarii haya mambo ya kufikirika tu kama ww tajiri n tajiri tu na kama ww umeumbwa kuwa maskini utakuwa maskini hata kama hutozini hata siku moja
Wenzako wanaifanya ngono wakiwa na kinga za kuwalinda au wanaifanya ili wachukue thamani ya wengine shtuka
 
Vijana kuleni mzigo maisha ni haya haya! Watu wanafanya umalayer na wanatoboa vizuri tu wengine wanajinyima na mpaka kesho ngoma ngumu.
 
Back
Top Bottom