Vijana hawanyanyuki kiuchumi sababu wanawake ni ombaomba

Ni mwanaume mjinga tu atakaeshindwa kupiga hatua kimaendeleo kwa sababu ya mwanamke.
Kuna mambo yana options ni uamuzi wako kufanya/kutokufanya.

Kuna mambo ya muhimu na ya lazima kufanya, ukishayajua hautopata shida.

Weka vipaumbele vyako na ishi kwa kuviheshimu na kuvipambani.
 
Fanyeni kazi nyie acheni ujinga wa kusingizia wanawake ni chanzo cha maisha yenu magumu. Kama ni hivyo ungekuta wanaume wote ni maskini, ila mbona wanaume wengine wana maisha mazuri tu wanahonga hadi magari?

Halafu wakati mnafanya kazi mjitahidi pia kutumia akili. Hauna hela badala ujitume kwenye kazi unahangaika na mapaja na makalio ya wadada halafu mnakuja kutupigia nduru huku utadhani hizo hela mliporwa
Kajala 1&2 tena zote ni Range
 
Ewe slay kwini kamuombe baba ako au mzazi mwenzio 🙄

20240306_094151.jpg
 
Wanawake muda mwingine mnawaandama tu bure, kwani huwa wanawaforce kuwapa pesa au mnawapatiaga wenyewe?
 
Ndugu zangu.

Sipo hapa kukashifu wanawake ila ukweli usemwe vijana wapone, vijana wengi wanafanya kazi ila ni masikini sana kwasababu wanadate na ombaomba.

Wanawake wamekua ombaomba sana kutwa kucha kuchezea simu , kupiga umbea saloon huku akimtumia baby wake picha kabinua makalio na kuachia kiuno wazi ili akitoka kutafuta hela ampe hicho kidogo alichopata.

Vijaa wanadate na ombaomba wanapigwa mizinga ya kila namna pasi na kuonewa huruma, vijana wanaamka saa kumi alfajiri kutafuta riziki siku inaisha wamepata elfu 5 na bado mwanamke huyo anaejiita mpenzi wake anae ishi kwao ana mlilia njaa, mara hela za kusuka, gesi imeisha, mara akanunue air force pamoja na ndugu zake vans avae apendeze huku mwanaume wake akizidi kusagika na kuhangamia kiuchumi

Vijana wanajibana sana ili kuwapa hela omba omba ambao hawamsaidii chochote zaidi ya kumpa utelezi unao mkamua nguvu zake zote na kukuacha akiwa amelegea sana, mchovu wa mwili na hela hana.

Vijana wamekua na maisha magumu sana , hawawekezi , hawana akiba kwasababu hawa madumadu, parara na nzige wamewachuna na kuwakamua kila mahali kwa kisingizio cha mwanamke matunzo. Mwaka mzima vijana wanakimbizana kutafuta hela ila huoni cha maana wanachofanya, utakuta kijana anakoma kusaka hela alafu hata kiwanja cha 10*15 hana, kitanda hakuna, hata radio hana ila anafanya kazi na hela anamalizia zote kwa mpenzi wake ambaye hana msaada wowote zaidi ya kumpa kikojoleo chake.

Vijana uchumi wao una yumba, wanaishi kwa tabu sana sababu maisha yao yamezungukwa na wanawake omba omba wasio na msaada wowote kwenye maisha yao, vijana wengine wanajitosa kusomesha wapenzi wao, kuwafungulia biashara na kuwapendezesha huku wakijisahau wao kujiendeleza kiuchumi na mwishowe wanaachika na kubaki masikini

Vijana wanateketea sana kiuchumi, wana hali mbaya mno, wanaishi kwa tabu, wanaugua hela hawana akiba hata kidogo kwa sababu wanadate na wanawake omba omba


Ndugu zangu vijana wanahangamia sana.
Zinaa ndio chanzo cha umasikini.
 
Back
Top Bottom