Kamata rais wa vijana Nyosho Elsaadati.....Hajawahi kufika kwao miaka 12 sasa...na wengi ukuw anatamani kuwa wakimbizi ...risasi mbili zikilia washavuka mpaka kwenda kuwa wakimbizi.
Wengine watatumia mwanya huu huu wamakelele ya kimataifa kwenda kuwa wakimbizi....
Mkuu nilipokuwa mtoto mdogo nilifikili Congo ni nchi ya wacheza mziki tu, sikuamini kama kuna vyuo vikuu au ma Profesa mpaka nilipokuja kumsikia Profesa Wamba Dia Wamba akiwa Chuo Kikuu Dar - hizo zilikuwa akili za kitoto si unajuwa TENA!
Utani mbali, lakini baada ya kuwachunguza kwa muda mrefu ndugu zetu hawa naona mawazo yangu ya utotoni yalikuwa na ukweli wa aina fulani ndani yake. Wacongo walio kuwa wanajali ustawi wa TAIFA lao kwa dhati walikuwa ni Patrice Lumumba na Pierre Mulele ndio maana hawakuishi muda mrefu! Tangu kutoweka kwa kwa mashujaa hao nchi hiyo aijawahi kuwa na amani ya kudumu by 100%, wala ukubwa wa nchi hiyo sio sababu ya kukosa uzalendo na amani, mbona walipo kuwa chini ya Wabelijiji nchi ilikuwa imetulia kabisa.
Tatizo la wenzetu hawa ni kutukuza starehe za mziki, mavazi
(wenyewe wanaita sijuhi PAMBA) na wanawake kuliko kitu chochote kile hapa duniani; sijawahi kuona wako overy concern na hatma ya TAIFA lao, sijawahi kusikia wimbo wowote unao husu matatizo ya nchi yao, maoni au kuonyesha kwamba mambo yanayo endelea nchini mwao yanawatia simanzi ya kweli, sijawahi kuwasikia wakihitisha mikutano au upigaji wa miziki ya hisani kwa ajili ya wakimbizi au raia wenzao walio kosa makazi nchini mwao kutokana na vita! Vijana wenye nguvu wanakimbia nchi yao kwenda kupiga miziki na kunengua kwenye nchi za nje wanasahau kabisa kushikamana na kuikomboa nchi yao yenye utajiri wa kila aina, leo hii wanataka vijana wa mataifa mengine waende Congo kupigana a proxy WAR, wenyewe wakiendelea na ndombolo ya SOLO ughaibuni, as far as they are concern
"MOKILI YAO NI MAMBO YA BORINGO BORINGO na MWASI bana kitoko akiwa karibu naye ndio BASI TENA" - mambo ya kukomboa nchi yao hayana priority yoyote katika mawazo yao!!
Mimi huwa nashindwa kuelewa kama traits zao hizo za kupenda miziki na starehe kipindukia ziko
inborn au
acquired? Niliwahi kusoma kitabu kimoja kilicho husu mpigania uhuru wa kimataifa Mr.
Che Guevara alikuwa anasimulia visanga alivyo wahi kukutana navyo alipo kuja Africa kuwasaidia Wacongo katika vita vya misituni dhidi ya Mobutu, mwenyeji wake walikuwa ni
Kabila Sr na Serikali ya TANZANIA,
Kabila Sr. na
Che waliodoka kwenda misitu ya Congo wakipitia Kigoma,
Che anasema alipo fika katika kambi ya wapiganaji alikuta wako kwenye mambo ya starehe tu hawa kuwa-commited na ukombozi wa nchi yao, nafikili
Che alikaa zaidi ya miezi sita (
kama nakumbuka vizuri) msituni Congo akiwanoa na kupigana bega kwa bega na jamaa hawa na alikuwa na tatizo la ugonjwa wa PUMU masikini,
Che katika mapigano yake nchini Congo alipoteza askali sita kati ya kumi na mbili aliokuja nao kutoka CUBA, kumbuka
Che wakati huo alikuwa bado ni Waziri katika Serikali ya Cuba na alikuwa na shahada ya chuo kikuu ya udaktari wa binadamu!!
Ndugu
Che kilicho mshangaza kuhusu hulka za ndugu zetu hawa ni kupenda kwao
STAREHE! Anasema walipo rudi Dar nadhani walifikia tena Hotel Continental
(kama nakumbuka vizuri) anasema baada ya siku mbili hivi,
Kabila Sr alianza kuendesha gari aina ya
mercedes mpya
, Kabila Sr alipo mwambia
Che Guevara kwamba gari hiyo ameinunua alimshangaa sana; funga kazi ni pale
Che na
Kabila Sr walipo ahidiana kukutana saa mbili jioni kuzungumzia mambo nyeti -
Kabila Sr alisahau ahadi yao hivyo
Che Guevara kahamua kumfata Kabila Hotel Continental na kwa kuwa
Che alikuwa anajuwa namba ya chumba alicho fikia
Kabila Sr aliamuwa kumfuata chumbani, kwa bahati mbaya Kabila alisahau kuweka komeo kwenye mlango wa chumba chake,
Che kufungua mlango tu-la ahula kamkuta
Kabila Sr akiwa na
wanawake watatu kitanda kimoja!! Kitendo hicho kilimkifu vibaya sana
Che Guevara, na toka siku hiyo alihapa hatarudi tena Africa (Congo) kusadia lolote, ingawa Che aliendelea kubaki hapa Dar kwa miezi kama saba hivi akiandika kitabu cha kumbukumbu za vita hivyo kabla ya kurudi CUBA.
Labda sasa cha kujihuliza hapa ni: Vituko hivyo vilitokea zaidi ya miaka karibu arobaini na saba iliyo pita, Je; kuna kitu chochote kilicho badirika muda wote huo kuhusu mind set za majirani zetu hawa kuhusu kutoweka maanani ukombozi wa kweli wa nchi yao, je mambo ya kupenda starehe kupindukia wameachana nayo?? Jibu ni hapana!
Labda hapa niongozee kwamba si
Wacongo wote wana tatizo hili, lakini tukiwa wakweli wengi wao wako hivyo; kama wangekuwa
wamoja na
majasiri nchi kama Rwanda isigeweza kuendesha Congo katika mwendo wa
FANGA FANGA na kuigeuza
Congo kuwa shamba la
BIBI.