Vijana chukueni mchongo wa soya

nzalendo

JF-Expert Member
May 26, 2009
10,815
10,100
Nawashauri vijana WANYAKE MASOKO MAWILI TU MAKUUUBWA SANA NA YOTE YATAMEZA VIJANA WOOTE WAKIACHA UVIVU.

1. CHINA WAMETUPA SOKO LA SOYA BEANS la ukubwa wa tani 400,000 kila mwaka Tanzania kwa sasa as we speak inazalisha tani 15,000 tu za soya.

Ina maana kunatakiwa tani 400,000 za soya kuzalishwa kubeba soko hilo la China.

UKULIMA WA KUZALISHA TANI 400,000 ZENYE SOKO la wazi ungeajiri vijana 75% ya wasio na kazi sasa hivi na wanaoulishwa ugali na wazazi wao waliomaliza la 7

#TUACHE UVIVU TULIME SOYA.

2. Tangu mwaka 2017 China walitupa soko la muhogo lenye thamani ya $377 milioni maana wao wanauhitaji kutengenezea wanga na sweeteners,Tapioca na bidhaa nyingine 12 kutoka huo hadi sasa Hatujapeleka hata 10% ya hilo soko na muhogo unastawi Mtwara,Lindi,Pwani,Morogoro na Tanga lakini watu tunalima vishamba vile vile vya kuuza muhogo kariakoo ndio maana hata ukiiutafuta muhogo kupeleka China himuwezi kuupata kama soya tu ..

HIVYO VIJANA TUACHE UVIVU pesa ziko KWENYE KILIMO HASA MASOKO HAYO YA WAZI KABISA NA YAKO MENGI sana

Kuna mwarabu alikuwa anataka bamia tani tano kila wiki kupeleka Dubai alikosa wapi atapata tani 20 za bamia kwa mwezi Tanzania hii.

Tan trade pana soko tangu 2018 la kuku 200,000 kila wiki kupeleka Bahrain lakini hata BAKHRESA haliwezi sio kwakua hana pesa bali hakuna utapata kukusanya kuku 200,000 Tanzania hii kwa wiki.

Ndio maana supermarket zinaingiza kuku wa nyama kutoka South Africa Zambia na malawi Zimbabwe kumekufa siku hizi.

Tanzania hii kuna watu wanaagiza samaki kutoka Thailand kuingiza Nchini hapo ndio ujiulize kwanini watu ni wavivu saana namna hii.

Masoko yapo vijana waache kulia lia tu wanyake masoko kwa kuzalisha bidhaa za kilimo.
 
Nyongeza.....kuna mTanzania amepata soko la korosho katika maduka ya Walmart Marekani,,,,,,kwa kipimo alichopewa angalau kontena za futi 40 ziwe 50 kwa kila baada ya miezi mitatu,,,,,,,,
Hata wakulima wote wa korosho Tanzania waungane kuwe na chombo cha kuwawezesha hawatamudu.......
 
Nyongeza.....kuna mTanzania amepata soko la korosho katika maduka ya Walmart Marekani,,,,,,kwa kipimo alichopewa angalau kontena za futi 40 ziwe 50 kwa kila baada ya miezi mitatu,,,,,,,,
Hata wakulima wote wa korosho Tanzania waungane kuwe na chombo cha kuwawezesha hawatamudu.......
Kontena 50 TANZANIA ishindwe?
Tufanye kontena moja ni tani 30

Tani30xkontena50 unapata Tani 1500 kila miezi 3.

KWA mwaka 1500x4=Tani 6000

Sasa jamaa ameambiwa apeleke Tani 6000.

UWEZO WA NCHI KUZALISHA KOROSHO

Nchi inazalisha tani 200,000 na zaidi KWA mwaka kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali ikiwemo website ya Statista


Kwanini Unasema nchi inayozalisha tani 200,000 inashindwa kutuma USA Tani 6000?
 
Back
Top Bottom