Ukweli kuhusu pombe kali na sigara

BUMIJA

JF-Expert Member
Oct 19, 2011
5,818
11,001
Pombe na Sigara ni bidhaa muhimu sana kwa uchumi wa Taifa. Lakini je ubora wa hizi pombe za vichupa za 2000 zinaenda kumaliza vijana wetu kwa namna mbili.

Vijana wanazianza mapema asubuhi kabla hawajala chochote. Hii pombe inaenda kusaga maini moja kwa moja. Bia ni Pombe nzuri sana ila ina gharama kubwa na vijana hawamudu walio wengi. Wanapendelea Jet Fuel ili walewe mapema.

Huchaguliwi namna ya kuishi,ila kila kitu kifanyike kwa kipimo.Sigara nazo tusiwafiche zinaozesha mapafu.Mtu mmoja anavuta zaidi ya Sigara 20 kwa siku.

Hizi pombe vijana wanaziparamia sana. Pombe ni starehe inayotaka maandalizi hasa suala la lishe.
Konyagi na Kvant hizi ni Congo za kizungu nazo. Zikifika tumboni zinataka zikute kitu chochote.
Vijana wengi lishe ni duni na tunakunywa ili tupunguze stress za maisha.Pombe ni starehe ya kuburudisha ubongo na sio stress zetu za kila Sikh.

Vijana wanasema unatunza maini ili umtunzie nani? Liver Curosis huathiri maini yako na mwisho huleta kifo.
Siwatishi vijana ila tunywe kwa vipimo na Sigara vuta kiasi.

Nawatakia weekendi njema na mnywe Kistaarabu.

The best hang over is the promise of never drinking again
 
Dah ukweli mi mwenyewe napenda sana Pombe hasa Weekend.

Shida sasa ukianza kumwagilia Moyo kutoka kwenye hicho kiti na kwendelea na ratiba zingine ndio changamoto.

Mungu atusaidie sisi vijana.

Kweli hapa naandika hii thread huku navaa nielekee kiwanja nikanywe Bia na Nyama kama nitawahi kurudi basi sa Saba Usiku.Yaan dah.

Na imenifanya siwezi oa wala kuishi na mwanamke.

But all in all BIA TAM
 
Hatuwezi kuongea bila mwanasheria wetu...

FB_IMG_16910896836581588.jpg
 
Pombe na Sigara ni bidhaa muhimu sana kwa uchumi wa Taifa. Lakini je ubora wa hizi pombe za vichupa za 2000 zinaenda kumaliza vijana wetu kwa namna mbili.

Vijana wanazianza mapema asubuhi kabla hawajala chochote. Hii pombe inaenda kusaga maini moja kwa moja. Bia ni Pombe nzuri sana ila ina gharama kubwa na vijana hawamudu walio wengi. Wanapendelea Jet Fuel ili walewe mapema.

Huchaguliwi namna ya kuishi,ila kila kitu kifanyike kwa kipimo.Sigara nazo tusiwafiche zinaozesha mapafu.Mtu mmoja anavuta zaidi ya Sigara 20 kwa siku.

Hizi pombe vijana wanaziparamia sana. Pombe ni starehe inayotaka maandalizi hasa suala la lishe.
Konyagi na Kvant hizi ni Congo za kizungu nazo. Zikifika tumboni zinataka zikute kitu chochote.
Vijana wengi lishe ni duni na tunakunywa ili tupunguze stress za maisha.Pombe ni starehe ya kuburudisha ubongo na sio stress zetu za kila Sikh.

Vijana wanasema unatunza maini ili umtunzie nani? Liver Curosis huathiri maini yako na mwisho huleta kifo.
Siwatishi vijana ila tunywe kwa vipimo na Sigara vuta kiasi.

Nawatakia weekendi njema na mnywe Kistaarabu.

The best hang over is the promise of never drinking again
Nadhani ni liver cirrhosis na si liver curosis
 
Back
Top Bottom