Vigogo wa CHADEMA wahamia CCM - Morogoro

majira ishanunuliwa ka jambo leo" kajanja kasife njaa
.
Mwananchi ,tz daima,itv hazijanunuliwa na cdm????..... Cdm kitakufa kwa sababu moja tu viongozi na wanachama wake wote hawapendi kusikia mabaya juu ya chama chao , wanapenda kupakwa maji ya mchele kila mara.... Hongera majira kwa kuwa sawa kwa pande zote ....
 
Wakihamia cdm toka ccm ni makamanda wapiganaji ..wakihama toka cdm kwenda ccm wachumia tumbo,mafisadi... Cdm endelea na mtazamo huo huo kuelekea 2015.
 
wanao ondoka waondoke tu ni bora kuwa na kikundi kidogo na wapiganaji maana ni heli nusu shari kuliko shari kamili ondokeni mamuruki njia nyeupe
 
Poor souls..........hivi kumbe kabla ya kupanda basi ni lazima ukague injini? Mimi nilikuwa sijui hilo.......halafu wamejidanganya sana kuwa viongozi wa CCMnia yao sio kujinufaisha.......Labda kwa vile wako Morogoro wangekuwa huko Bongo wasingesema hayo
safi sana ,sahani ya supu *HAIOSHWI KWA MAJI BARIDI* kiboko yake maji moto na sabuni,magamba mpaka yaishe.walifikiri chama cha manufaa hicho*CDM*WAKAUNGANE NA CHICHIDODO

 
Huyu si Shibuda John kweli?

Ukiwa shushushu wa chama hizo ndo kazi wanazopewa. Namfahamu kiongozi mmoja alikuwa chama pinzani baadaye nikamuona anawakilisha ccm kwenye shughuri maalum ya kitaifa. Wala wapinzani wa kweli wasitishike na hilo jambo, huo ni mpango wa ccm wa muda mrefu wa kuonesha watanzania wasivo penda vyama vya upinzani kama mbinu za kudhoofisha wapinzani.

ccm wanapotea kutumia njia hizo. Wao wangekuwa wanatenda mambo yaliyo sawa then watu wanaipenda ccm kwa kazi nzuri sio wanajifanya kuua upinzani ili wao waendelee kuibia nchi.
 
Na Severin Blasio, Morogoro

ALIYEKUWA Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), mkoani Morogoro, Bw. Abeli Ruanda pamoja na Mwenyekiti wa chama hicho wilayani Morogoro Bw. Rajabu Ally ’Kiselengo’, wametangaza rasmi kuhamia CCM.

Wakizungumzia na gazeti hili kwa nyakati tofauti, viongozi hao walidai kujiunga upinzani kwa bahati mbaya kama abilia awapo barabarani ambapo linapotekea gari lenye umbo na rangi nzuri hulazimika kuingia ukiamini ni chombo imara wakati mashine yake ni mbovu na haiwezi kuwafikisha popote.

Mbali na kuipongeza CCM kwa uimara wake, viongozi hao walisema vyama vya upinzani havina sera ya kuwakomboa Watanzania bali viongozi wake wanataka kujinufaisha.


Chanzo: Gazeti la Majira, Dec 4, 2012
Safiiii. Mhe Silaha fuata nyayo!
 
Na Severin Blasio, Morogoro

ALIYEKUWA Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), mkoani Morogoro, Bw. Abeli Ruanda pamoja na Mwenyekiti wa chama hicho wilayani Morogoro Bw. Rajabu Ally 'Kiselengo', wametangaza rasmi kuhamia CCM.

Wakizungumzia na gazeti hili kwa nyakati tofauti, viongozi hao walidai kujiunga upinzani kwa bahati mbaya kama abilia awapo barabarani ambapo linapotekea gari lenye umbo na rangi nzuri hulazimika kuingia ukiamini ni chombo imara wakati mashine yake ni mbovu na haiwezi kuwafikisha popote.

Mbali na kuipongeza CCM kwa uimara wake, viongozi hao walisema vyama vya upinzani havina sera ya kuwakomboa Watanzania bali viongozi wake wanataka kujinufaisha.


Chanzo: Gazeti la Majira, Dec 4, 2012

Very interesting...imekuwa vyema kutambua na kuchukuwa maamuzi mapema ila sina uhakika kama hilo gari walilokimbilia mashine yake iko salama. Kama viongozi walipaswa kutumia busara kukimbilia gari ambalo walidhani liko salama (CHADEMA) lakini wakagundua baadaye gari hilo haliko salama baada ya kuona mwendo kasi na umakini wa kondakta ambaye hatoi misaada tutani.
 
Nimeona kamanda Sugu ameingiza wanachama zaidi ya 200 wapya na ni wananchi wa kawaida kabisa ambao maisha yao yamefanywa magumu na ccm.. Tunawahitaji wananchi wa kawaida kwenye kwenye ukombozi.. Sio hawa ambao walikuwa ni viongozi kabla ya kutoka ccm.. Wanapokuja wanaishia kuitisha mikutano na kutangaza kuhama kwa kashfa..
Hata pale Morogoro waliandamana wengi tu lakini hawa Viongozi walikuwa wapi mpaka kijana wa watu AKALA CHUMA CHENHYE NCHA KALI
Kwa hiyo hao wanaoandamana kwanza wangewauliza hao madreva wanaoendesha hilo Basi lenye rangi nzuri ni zima kweli au ni sifa kujaza tu watu.
Baada ya Dreva na konda kushuka nani anakuwa Dreva ni swala la abiria kujiuliza,
AMA KUSHUKA KUPANDA BASI LINGINE
AU KUTEMBEA KWA MIGUU

Kitendo cha kufuata mkumbo wakati uko nyuma km Kobe hutajua km Safari ni Safari bora niwe mbele kiherehere km mbwamwitu katika Msafara wa wanyama nitajionea mengi hata kitu chenye Ncha kali nitakikwepa
 
Last edited by a moderator:
MKUU VYEO VIPI TENA unamaanisha? si tayari walikuwa navyo huko chadema lakini wameamua kuvitema? labda utoe sababu nyingine.
yeo naaamnisha kuwa kwa CCM kuwa na cheo ni Ulaji, CDM kuwa na cheo ni utendaji, see the difference
 
alijiunga kwa bahati mbaya kumbe na sio dhamira na nia ya kupambana na udhalimu.....kaona njaa kali anasepa,huku harakati kwenda mbele posho hamna nenda wakina mwigulu kama hawaja ***** kule igunga alaivyofanyiwa mwenzako sababu ya njaa kama hizo
 
Unafahamu hata huko walipokwenda nako watapakimbia kwa sababu za njaa zao,unapohitaji madaraka lazima ujipange na watambue kuwa wasiichukulie chadema kama sehemu ya kujipatia madaraka,ukitaka madaraka lazima ujipange,hivyo hata huko wanakotaka. Kwenda wajue kuwa nako huko panahitaji gharama kwani kule rushwa ndo mahala pake tumeona rushwa kila kona hivyo kama hawajajipanga wajipange.CHADEMA MZIKI MKUBWA
 
kwani kuihama chadema dhambi?????,aya na uyo katibu wa chama nae arudi alikotoka ambapo anaonekana bado anapatamani,na ye mtamuita ananjaa au mta zip midomo iyo!
 
Hawa walikuwa ni mapandikizi ya CCM,sasa walishindwa kufanya walichotumwa!.Ni bora wamejitoa mapema.
 
Udini na ukabila unaaitafuna cdm ingawa wenyewe wanajifanya hamna kasoro yeyote.walahi watabaki wenye chama chao wachaggggigikoko
 
Back
Top Bottom