Vigogo wa CHADEMA wahamia CCM - Morogoro

KIBE

JF-Expert Member
Nov 23, 2010
943
184
Na Severin Blasio, Morogoro

ALIYEKUWA Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), mkoani Morogoro, Bw. Abeli Ruanda pamoja na Mwenyekiti wa chama hicho wilayani Morogoro Bw. Rajabu Ally 'Kiselengo', wametangaza rasmi kuhamia CCM.

Wakizungumzia na gazeti hili kwa nyakati tofauti, viongozi hao walidai kujiunga upinzani kwa bahati mbaya kama abilia awapo barabarani ambapo linapotekea gari lenye umbo na rangi nzuri hulazimika kuingia ukiamini ni chombo imara wakati mashine yake ni mbovu na haiwezi kuwafikisha popote.

Mbali na kuipongeza CCM kwa uimara wake, viongozi hao walisema vyama vya upinzani havina sera ya kuwakomboa Watanzania bali viongozi wake wanataka kujinufaisha.

Chanzo: Gazeti la Majira, Dec 4, 2012
 
walitegemea kupata posho, kwa hiyo anaona sera nzuri morogoro Abood kutoa basi kupeleka watu kwenye mazishi? njaa mbaya sana
 
Walikimbilia vyeo...haooo waende kwa wachumia njaa wenzao
 
Hao ni losers ni wachungaji wa mshahara tena bora wamewahi kuondoka wafike salama waendako."Kuvuja kwa pakacha nafuu ya mchukuzi"
 
Siyo vibaya..siasa ni kazi kama kazi nyingine...kama ukiona hailipi tafuta kazi sehemu (chama) nyingine. Tusidanganyane wanasiasa wote wapo walipo kwasababu ya njaa zao na tamaa ya madaraka. Haya ya kusema kwamba fulani alikuwa mzigo ndani ya chama au fulani alipotea njia ni porojo tuu........wakati mwingine tuwe wakweli
 
Pesa za pembe za ndovu za kinana zinafanya kazi!tunawatakia kila la kheri!hata askari vitani kuna mamluki.
 
Na Severin Blasio, Morogoro

ALIYEKUWA Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), mkoani Morogoro, Bw. Abeli Ruanda pamoja na Mwenyekiti wa chama hicho wilayani Morogoro Bw. Rajabu Ally 'Kiselengo', wametangaza rasmi kuhamia CCM.

Wakizungumzia na gazeti hili kwa nyakati tofauti, viongozi hao walidai kujiunga upinzani kwa bahati mbaya kama abilia awapo barabarani ambapo linapotekea gari lenye umbo na rangi nzuri hulazimika kuingia ukiamini ni chombo imara wakati mashine yake ni mbovu na haiwezi kuwafikisha popote.

Mbali na kuipongeza CCM kwa uimara wake, viongozi hao walisema vyama vya upinzani havina sera ya kuwakomboa Watanzania bali viongozi wake wanataka kujinufaisha.

Chanzo: Gazeti la Majira, Dec 4, 2012

Poor souls..........hivi kumbe kabla ya kupanda basi ni lazima ukague injini? Mimi nilikuwa sijui hilo.......halafu wamejidanganya sana kuwa viongozi wa CCMnia yao sio kujinufaisha.......Labda kwa vile wako Morogoro wangekuwa huko Bongo wasingesema hayo
 
kitu ambacho sielewi ni mabinti wadogo kuparamia vibabu, sijui mnataka kumuulia kifuani?

hivi kule kwenu buruguni kwa mnyamani hakuna vitoweo vingine zaid ya vichwa na miguu ya kuku??

Hivi unaona athari uliyoipata kutokana na kutumia chakula hiko??
 
ni bora tunaanza kuwajua mapema,naomba majina yao yaandikwe kwa ajili ya historia ya vizazi vijavyo kama wasaliti wa taifa...
 
Gazeti la Majira siku hizi linaripoti habari za CCM tu kishabiki na tena kwa upande mmoja.
 
Ukiwa shushushu wa chama hizo ndo kazi wanazopewa. Namfahamu kiongozi mmoja alikuwa chama pinzani baadaye nikamuona anawakilisha ccm kwenye shughuri maalum ya kitaifa. Wala wapinzani wa kweli wasitishike na hilo jambo, huo ni mpango wa ccm wa muda mrefu wa kuonesha watanzania wasivo penda vyama vya upinzani kama mbinu za kudhoofisha wapinzani.

ccm wanapotea kutumia njia hizo. Wao wangekuwa wanatenda mambo yaliyo sawa then watu wanaipenda ccm kwa kazi nzuri sio wanajifanya kuua upinzani ili wao waendelee kuibia nchi.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Wakizungumzia na gazeti hili kwa nyakati tofauti, viongozi hao walidai kujiunga upinzani kwa bahati mbaya kama abilia awapo barabarani ambapo linapotekea gari lenye umbo na rangi nzuri hulazimika kuingia ukiamini ni chombo imara wakati mashine yake ni mbovu na haiwezi kuwafikisha popote.

Thats explain everything....kila heri kwa 'bahati nzuri' huko CCM!
 
Habembelezwi mtu mzima kama yai huku CHADEMA. Kama ulikuja kwa malengo binafsi na ukaona hakuna nafasi, just show us your back.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom