Vigogo wa CHADEMA wahamia CCM - Morogoro

Kwa taarifa CDM ni chama cha kizazi kipya. Kuna mikikimiki mingi ya ukombozi kwa mfano operation sangara, mara M4C, mara vua gamba vaa gwanda n.k. Hakuna kulala mpaka kieleweke. Wazee wenye makovu ya CCM na wachumia tumbo hawawezi kudumu CDM. Wataingia na kutoka. Waacheni waende zao. Akitoka mzee moja moja huingia vijana kumi. 2015 mabadiliko ni lazima! Hiyo ni kauli mbiu ya kizazi kipya.
 
Nimemkumbuka kiongozi huyo ni Ndimara Tegambwage. Wapinzani wakweli msitishike na hao wanaoandaliwa na ccm kujifanya wapinzani then wanajifanya kurudi ccm kwa visingizio visivo na mishiko. Uozo unao fanywa na viongozi ndani ya ccm na hatuoni wanavyo wajibishwa, kwa akili ya mtu wa kawaida unawezaje ukarudi ccm wakati wanaoaibika kwa rushwa, kuibia taifa hawafanywi lolote, ni usanii kwenda mbele, ukiona watu kama hao ni mbumbumbu na hawakupaswa kuitwa wapinzani.

Swali la kujiuliza ni mazuri yapi yamefanywa na ccm watu wakatamani kurudi ccm? Mi nawaita mazezeta waacha hizo ni njaa.
 
Kwa taarifa CDM ni chama cha kizazi kipya. Kuna mikikimiki mingi ya ukombozi kara vile operation sangara, mara M4C, mara vua gamba vaa gwanda. Hakuna kulala mpaka kieleweke. Wazee wenye makovu ya CCM hawaiwezi. Wataingia na kutoka. Waacheni waende zao. Akitoka moja huingia kumi. 2015 mabadiliko ni lazima! Hiyo ni kauli mbiu ya kizazi kipya.
nisichokijua ni kiasi gani ccm wametenga kufanya kazi hii ambayo lengu lake kubwa ni kuchelewesha ukombozi wa mnyonge wa Tanzania
 
Hatushangai kwenye msululu wa mamba na kenge wamo. Bora mmejitambua mapema mkaondoka make sisi tuko na mungu
 
Na Severin Blasio, Morogoro

ALIYEKUWA Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), mkoani Morogoro, Bw. Abeli Ruanda pamoja na Mwenyekiti wa chama hicho wilayani Morogoro Bw. Rajabu Ally ’Kiselengo’, wametangaza rasmi kuhamia CCM.

Wakizungumzia na gazeti hili kwa nyakati tofauti, viongozi hao walidai kujiunga upinzani kwa bahati mbaya kama abilia awapo barabarani ambapo linapotekea gari lenye umbo na rangi nzuri hulazimika kuingia ukiamini ni chombo imara wakati mashine yake ni mbovu na haiwezi kuwafikisha popote.

Mbali na kuipongeza CCM kwa uimara wake, viongozi hao walisema vyama vya upinzani havina sera ya kuwakomboa Watanzania bali viongozi wake wanataka kujinufaisha.

Chanzo: Gazeti la Majira, Dec 4, 2012

Hao ni WAZANDIKI. Kwani walipoingia hawakupima? Au malengo yao ya kukifisadi chama hayakufikiwa? Au (MCHURO) MZEE WA KUZIKA bwana ABOOD kawanunua? Natumai nanyi kesha waleteeni uchuro mtazikwa karibuni. CHADEMA itabaki imara hadi mwwisho wa DAHARI
 
Nimeona kamanda Sugu ameingiza wanachama zaidi ya 200 wapya na ni wananchi wa kawaida kabisa ambao maisha yao yamefanywa magumu na ccm.. Tunawahitaji wananchi wa kawaida kwenye kwenye ukombozi.. Sio hawa ambao walikuwa ni viongozi kabla ya kutoka ccm.. Wanapokuja hawa wanakuwa na malengo yao binafci au kutumwa ambayo mwisho wanakuja kugundua ni vigumu kupata yale waliyoyafuata wanaishia kuitisha mikutano na kutangaza kuhama kwa kashfa..
 
walitegemea kupata posho, kwa hiyo anaona sera nzuri morogoro Abood kutoa basi kupeleka watu kwenye mazishi? njaa mbaya sana

Walidhani huku kuna lundo la hela, hawakujua wazalendo wa kweli hujitolea kwa ajili ya chama na nchi yao.Let them go to hell!
 
Waende mbele hao waganga njaa,hii ndio mbinu walobakia nayo Magamba otherwise hawana mbinu nyingine zaidi ya hii.
 
Siyo vibaya..siasa ni kazi kama kazi nyingine...kama ukiona hailipi tafuta kazi sehemu (chama) nyingine. Tusidanganyane wanasiasa wote wapo walipo kwasababu ya njaa zao na tamaa ya madaraka. Haya ya kusema kwamba fulani alikuwa mzigo ndani ya chama au fulani alipotea njia ni porojo tuu........wakati mwingine tuwe wakweli

mtanzania; bora umewaambia ukweli CDM mana kwao kuambiwa ukweli huo ni dhambi... siasa ni fedha hakuna mwanasiasa anayefanya kazi bure .. kila mtu anahaki ya kuhama chama sasa wameona CDM kuna matatizo si chama cha kuendelea mbele ni chama cha mtu mmoja au wawili basi wameamua kurudi CCM kwa imani kuwa ndio chama sahihi.. mbona tumeona ccm wanaenda chadema mbona hawasemi ni wachumia tumbo???.... ukweli uko wazi hao jamaa ndio walikuwa mhimili mkuu wa CDM morogoro sasa wameshatamba zao kwa babayao ....
 
ccm ni kama kisima.. watazunguuka weeee! mwisho a siku watarudi kuteka maji..... kuna thread humu mzee slaa bado hajarudisha kadi.. hehehehe ... ccm si mchezo
 
Na Severin Blasio, Morogoro

ALIYEKUWA Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), mkoani Morogoro, Bw. Abeli Ruanda pamoja na Mwenyekiti wa chama hicho wilayani Morogoro Bw. Rajabu Ally ’Kiselengo’, wametangaza rasmi kuhamia CCM.

Wakizungumzia na gazeti hili kwa nyakati tofauti, viongozi hao walidai kujiunga upinzani kwa bahati mbaya kama abilia awapo barabarani ambapo linapotekea gari lenye umbo na rangi nzuri hulazimika kuingia ukiamini ni chombo imara wakati mashine yake ni mbovu na haiwezi kuwafikisha popote.

Mbali na kuipongeza CCM kwa uimara wake, viongozi hao walisema vyama vya upinzani havina sera ya kuwakomboa Watanzania bali viongozi wake wanataka kujinufaisha.

Chanzo: Gazeti la Majira, Dec 4, 2012

Nasikitika hao ndugu zangu wanaendekeza siasa za njaa na kufuata upepo! Tusubiri tutaona njaa yao kama itaisha ccm!
 
Na Severin Blasio, Morogoro

ALIYEKUWA Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), mkoani Morogoro, Bw. Abeli Ruanda pamoja na Mwenyekiti wa chama hicho wilayani Morogoro Bw. Rajabu Ally ’Kiselengo’, wametangaza rasmi kuhamia CCM.

Wakizungumzia na gazeti hili kwa nyakati tofauti, viongozi hao walidai kujiunga upinzani kwa bahati mbaya kama abilia awapo barabarani ambapo linapotekea gari lenye umbo na rangi nzuri hulazimika kuingia ukiamini ni chombo imara wakati mashine yake ni mbovu na haiwezi kuwafikisha popote.

Mbali na kuipongeza CCM kwa uimara wake, viongozi hao walisema vyama vya upinzani havina sera ya kuwakomboa Watanzania bali viongozi wake wanataka kujinufaisha.

Chanzo: Gazeti la Majira, Dec 4, 2012

Hili neno vigogo linaweza kuwa linatumika vibaya.
 
Sera za CDM zinataka committment. Mindset na attittude ya kivivivuvivu tuliyonayo watanzania inajidhihirisha pale mtu anapopaswa kuchapa kazi. Uvivu, ufisadi, majungu, kupenda vijiwe, wizi, kupenda posho na utajiri wa haraka haraka bila kufanya kazi ndio tabia na sera za serikali hii. Tukipata sera safi ama kiongozi serious tunamwona hafai.

Waache waende, wamezoea ukupe, ufisadi na tabia zote zisizokubalika CDM. Hawa hawaziwezi lakini pia ni haki yao ya kikatiba kujiunga na chama chochote. CCM pokea uozo unakuja
 
Back
Top Bottom