Vigogo wa CHADEMA wahamia CCM - Morogoro

Vigogo wa CHADEMA wahamia CCM - Morogoro

Napenda spirit ya wana CDM. Never give up! This shows you are politicians. Big up!
 
Watu wengi wanafikiri kuwa upinzani tanzania ni kazi ndogo, tanzania ukiwa ccm unaweza hata ukawa na jinai lakini ukaachwa eti kisa ni ccm. Narudia kuwapongeza tena makamanda wote waliopo upinzani one day yes! Msafara wa mamba na kenge wapo!
 
Na Severin Blasio, Morogoro

ALIYEKUWA Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), mkoani Morogoro, Bw. Abeli Ruanda pamoja na Mwenyekiti wa chama hicho wilayani Morogoro Bw. Rajabu Ally ’Kiselengo’, wametangaza rasmi kuhamia CCM.

Wakizungumzia na gazeti hili kwa nyakati tofauti, viongozi hao walidai kujiunga upinzani kwa bahati mbaya kama abilia awapo barabarani ambapo linapotekea gari lenye umbo na rangi nzuri hulazimika kuingia ukiamini ni chombo imara wakati mashine yake ni mbovu na haiwezi kuwafikisha popote.

Mbali na kuipongeza CCM kwa uimara wake, viongozi hao walisema vyama vya upinzani havina sera ya kuwakomboa Watanzania bali viongozi wake wanataka kujinufaisha.

Chanzo: Gazeti la Majira, Dec 4, 2012
Hapo kwenye RED sijui kwa ufahamu wangu hilo neno linamaanisha nini? inamaanisha hakuwa kiongozi bali alikuwa kwa hiyo kusema vigogo sio sahihi nikiwa namaanisha kwa sasa kuna viongozi wengine ila wao walikuwa hapo siku za nyuma.
 
Kwa hiyo unapinga vigogo wa Chadema Morogoro hawajahamia CCM?
Hiyo habari ina upotoshaji mkubwa sana.
Huyo Abel Luanda sio kiongozi wa Chadema kwa wakati huu anapohamia CCM.

Miezi mitatu iliyopita wakati wa Operation za M4C Morogoro alijiuzuru baada ya kusikia unafukuzwa (baada ya kugundulika ni mamluki ndani ya Chadema na alikuwa mstari wa mbele Kukwamisha M4C morogoro), na nafasi yake akakaimu mtu mwingine.

Habari zake ziliandikwa humu JF tena kwa Kina sana.
 
Naomba kuuliza.
- Hivi kadi za vyama hurejeshwa kwenye vyama alikotoka mtu, au hukabidhiwa kwenye chama kingine ambako mtu amehamia?
- Kadi ya uanachama ni mali ya mtu au mali ya chama?
- Huyo mwanachama aliipataje, alipewa bure au aliinunua?
- Kama halipii ada za chama ni sahihi kumtambua kuwa ni mwanachama wako hai? Nafikiri hapa umtambue tu kuwa aliwahi kuwa mwanachama.
 
- Mwanachama mmoja akiondoka ni issue sana kuziba pengo lake? Hakuna wanachama wengine?
 
Daa nimeanmini tanzania kazi kwelikeli hivi hao vigogo sio wasaliti bali wamekosaulaji wanaona hawatajiliki haraka wabinasfi hao hamna lolote ukiwa ccm bana ndani yamiaka miwili lazima uwe tajiri maisha mazuli hawana uchungu na pesa za wananchi wache waende watarudi 2
 
hao hawajawahi kuwa wapinzani bali walikuwa nyinyiemu damu, walijiunga upinzani pasipo kujua kuwa upinzani una changamoto nyingi ikiwa mojawapo chama tawala kutumia mabavu kuviminya hata kubana biashara zaowaende hao hawakuwa makamanda wapigananji, ingekuwa jeshi walipaswa wapigwe risasi na kuuawa
 
Leo hii namka2 naskia taarifa ya habari ETI TANZANIA NI YA KWANZA KUWA MASKINI KATIKA NCHI ZA KUSINI MWA SAHARA wanao itia umasikini ninani ? kama sio mafisadi na mikataba mibovu wache wahamie huko tutawakamata tu siku zao zina hesabika
 
Naomba kuuliza.
- Hivi kadi za vyama hurejeshwa kwenye vyama alikotoka mtu, au hukabidhiwa kwenye chama kingine ambako mtu amehamia?
- Kadi ya uanachama ni mali ya mtu au mali ya chama?
- Huyo mwanachama aliipataje, alipewa bure au aliinunua?
- Kama halipii ada za chama ni sahihi kumtambua kuwa ni mwanachama wako hai? Nafikiri hapa umtambue tu kuwa aliwahi kuwa mwanachama.
- Mwanachama mmoja akiondoka ni issue sana kuziba pengo lake? Hakuna wanachama wengine?
Mkuu hakuna utaratibu wowote wa kisheria unaoelekeza kufuatwa mtu unapotaka Kuhama chama ili kuhamia chama kingine. Hivyo mtu aliyehama chama, kadi ya uanachama haina kazi tena, yaani inakuwa ni takataka tu.

Sheria hauruhusu mtu kuwa mwanachama wa vyama viwili kwa wakati mmoja. Hivyo unapohamia chama kingine automatically uanachama wa chama chako cha awali unakufa hapo hapo.
 
Chama kinasambaratija hiki,siamini macho yangu.jana mjumbe wa kamati tendaji/katibu wa ilemela amebwaga manyanga,huko mbeya katibu wa wilaya wa cdm amenasa kwenye rushwa,na huku morogoro tena abiria wameshuka kwenye mkokoteni.haya yangu macho
 
Slaa nae amekiri kuwa ana kadi ya ccm,tusubiri tutayasikia tu
 
Tunawatakia kila la heri, wamsalimie na yule aliyesema 'kuliko kuhama CUF kwenda CCM ni heri kulala kingono na mama yangu'. Nadhani alitekeleza. Nao kila la heri.
 
Hiyo topic imekaa kishabiki, nani kakuambia hao ni vigogo wa Chadema?
 
Hiyo habari ina upotoshaji mkubwa sana.
Huyo Abel Luanda sio kiongozi wa Chadema kwa wakati huu anapohamia CCM.

Miezi mitatu iliyopita wakati wa Operation za M4C Morogoro alijiuzuru baada ya kusikia unafukuzwa (baada ya kugundulika ni mamluki ndani ya Chadema na alikuwa mstari wa mbele Kukwamisha M4C morogoro), na nafasi yake akakaimu mtu mwingine.

Habari zake ziliandikwa humu JF tena kwa Kina sana.

Asante kwa kuliweka ili sawa mkuu,maana nilitaka niweke sawa ila baada ya kusoma post yako nikaona umemaliza kila kitu!waache watapetape sisi mapambano yanaendelea,eti wanatoa kauli za kipuuzi kua vyama vya upinzani havina sera nzuri za kuwaletea maendeleo Watanzania,kweli ukiwa na akili za kuropoka kabla ya kufikiri kwanza ni bora ubaki c.c.m tu!
 
Nimesikia tetesi mjini Morogoro kiongozi yoyote wa Chadema akijitoa na kutangaza, CCM wanampa kitita cha uhakika, naona ndivyo walivyofanya hawa jamaa ili watoke kimaisha. Mambo ya fedha yamewahamisha kama Kevin Yondani alivyoenda Yanga jamaa hela yote ya ufisadi wanayo wao. Azizi Abood anachangia kwenye siasa ile mbaya sasa hivi, anakata mshiko vibaya vibaya kwa sababu yeye kuongea sana hajui.
 
Back
Top Bottom