Vigogo kutinga mahakamani kesi za uchaguzi


Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Messages
169,611
Likes
639,488
Points
280
Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2010
169,611 639,488 280
Vigogo kutinga mahakamani kesi za uchaguzi
Friday, 10 December 2010 20:45

Waandishi Wetu

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru), imesema wakati wowote kuanzia sasa itakamilisha uchunguzi na kuwafikisha mahakamani vigogo wa serikali wanaokabiliwa na tuhuma za rushwa katika uchaguzi mkuu uliopita. Mkurugenzi wa Takukuru, Dk Edward Hoseah, alibainisha hayo jijini Dar es Salaam jana, wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa.

Katika maadhimiho hayo, Dk Hoseah alisema iwapo viongozi walio madarakani watabainika kujihusisha na rushwa katika mchakato huo, watapandisha kizimbani na sheria itachukua mkondo wake.



“Bado tupo kwenye mapambano, mpaka sasa mchakato wa upelelezi wa kesi hizo unaendelea, mara tu utakapokamilika kesi hizo zitaanza kufikishwa mahakamani, ” alisema Dk Hoseah na kuongeza: Nchi hii inaendeshwa kwa utawala wa sheria, huwezi kumpeleka mtu mahakamani bila kuwa na ushahidi, tukiwa tunakimbilia mahakamani nchi hii tutaiporomosha.” Pia, Dk Hosea alisema rushwa ni jambo linalohitaji kufanyiwa kazi kwa muda mrefu ili kufanikisha kutokomezwa, lazima mapambano yake yahusishe kila mwananchi.

Dk Hosea alisema kuhakikisha wanafanikiwa kwenye vita hiyo hasa kwa taasisi za umma, wameanzisha kamati 200 katika wizara na idara mbalimbali za serikali. Alisema wameanzisha kamati 123 katika halmashauri mbalimbali nchini, aliwataka wananchi kutumia kamati hizo kuweza kupambana na rushwa.



Wakati Takukuru ikieleza hayo, Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), limeitaka serikali kukamilisha mchakato wa kupitisha sheria ya kulinda wananchi watakaojitokeza kufichua vitendo vya rushwa. Mwakilishi wa UNDP nchini, Philippe Poinsot, alisema serikali inatakiwa kukamilisha mchakato wake wa kupitisha sheria ya kulinda wananchi watakaoshiriki kufichua wanaotoa na kupokea rushwa.

Poinsot alisema serikali inatakiwa kuwa wazi katika masuala ya ununuzi bidhaa na huduma zake na kwamba, suala hilo linachukua asilimia 70 ya bajeti ya serikali. Mwisho
 

Forum statistics

Threads 1,238,906
Members 476,226
Posts 29,336,473