Vigogo CHADEMA kizimbani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vigogo CHADEMA kizimbani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Aug 26, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Aug 26, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Imeandikwa na John Mhala, Arusha; Tarehe: 26th August 2011

  KATIBU wa Jumuiya ya Vijana ya Chadema (BAVITA), Anold Kamunde na aliyekuwa Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Arusha, Godbless Lema, Gervas Mgonja wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma za wizi wa kutumia silaha na kupora vitu na fedha vyote vikiwa na thamani ya Sh milioni 3.5.

  Mbali na hilo pia askari Polisi, Salumu Idefonce (23) wa Kituo kikuu cha Polisi Mkoa wa Arusha amefikishwa mahakamani kwa madai ya mauaji ya mlinzi wa kampuni ya kuuza na kununua madini ya Classic Gems, Joseph Kisuda.

  Wakisomewa mashitaka na Mwendesha Mashitaka wa Serikali, Agustino Kombe, ilidaiwa mahakamani hapo, kuwa Mgonja na Kamunde, walifanya hayo wakitumia bunduki aina ya SMG na bastola katika tukio lililotokea Ngarenaro jijini hapa Juni 8.

  Kombe alidai hivyo mbele ya Hakimu Mkazi wa Mkoa wa Arusha, Rose Ngoka, kuwa
  watuhumiwa hao walitenda kosa hilo kwa kumpora Elizabeth Mkuka, fedha taslimu Sh milioni 1.8 na simu mbili.

  Aliendelea kudai kuwa Mgonja na Kamunde walitenda kosa hilo saa 3 usiku kwa kiasi hicho cha fedha na simu mbili za Sumsung na BlackBerry zote zikiwa na thamani ya Sh milioni 1.6.

  Viongozi hao walikana mashitaka yao na kesi yao itatajwa Septemba 8 na walirudishwa rumande kwani upelelezi haujakamilika na walinyimwa dhamana kutokana na uzito wa kesi yenyewe kisheria.

  Katika kesi ya Idefonce, Mwendesha Mashitaka wa Serikali, Sabina Slayo, mbele ya Hakimu Mkazi wa Mkoa wa Arusha, Devotha Msofe, alidai kuwa mtuhumiwa anashitakiwa kwa mauaji pamoja na wenzake wawili katika tukio la Mei 21 katika kampuni hiyo ya madini.

  Wenzake ambao wako rumande ni Abdul Philipo ‘Baba Salimu’ na Prosper Saimoni ‘Otieno’.

  Mshitakiwa hakutakiwa kujibu lolote kwani Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji ila Mahakama ya juu yake.

  Kesi hiyo itatajwa mahakamani hapo Septemba 6 na alirudishwa rumande hadi siku hiyo.

  Habari za nje ya Mahakama zilidai kuwa viongozi wa Chadema wataunganishwa na washitakiwa wengine waliokuwa walisomewa mashitaka juzi katika Mahakama hiyo kwa mashitaka hayo hayo.
   
 2. s

  smz JF-Expert Member

  #2
  Aug 26, 2011
  Joined: Dec 18, 2010
  Messages: 251
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Huu uandishi mwingine sijui inakuwaje, maana inawachanganya hata wasomaji: "Aliyekuwa katibu wa mbunge Godbless Lema", huoni kama unawachanganya wasomaji. Wengine wanaweza fikiria ni Lema mwenyewe.

  Kwa nini Mh Lema atajwe kwenye kesi isiyomhusu wala mtu mwenyewe hahusiki naye. Ingetosha kwa mwandishi kusema 'Gervas Mgonja" amefikishwa mahakamani kwa makosa ya ujambazi. Mshtakiwa alishawahi kufanya kazi katika ofisi ya mbunge wa Arusha mjini. Tosha!!.

  Ya nini kurefect jina la Mbunge wetu mwanzoni mwa habari, Hii ina maana gani, au mwandishi anataka kumuhusisha Mh Lema na hiyo kesi?

  Waandishi tafadhali epukeni kutumia majina ya watu bila sababu ya msingi. Kwanza mliripoti kwa mara ya kwanza kwamba huyo mshitakiwa ni katibu wa mbunge Lema. Hadi mwenyewe alivyokanusha ndo mmebadili, lakini hamtaki kumwondoa Mh Lema kwenye hii habari yenu.

  Sasa kumwita aliyekuwa katibu wa Mbunge kuwa ni kigogo wa CHADEMA kuna ukweli hapo. Huu ndo upotoshaji. Andika vitu vilivyo wazi bana. Kama huipendi CHADEMA ni wewe tu.!!!
   
 3. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #3
  Aug 26, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Inaweza kuwa SIO kutoipenda CHADEMA bali ujanja wa mwandishi na mhariri wake. Tasnia ya habari/uandishi sasa hivi inavamiwa sana, kuna vyuo lukuki vimeibuka vya "uandishi wa habari" vinaibua shaka/doubt na ubora wao
   
 4. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #4
  Aug 26, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,004
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  Nani kigogo sasa? Hivi nini maana ya neno kigogo?
   
 5. F

  FUSO JF-Expert Member

  #5
  Aug 26, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,866
  Likes Received: 2,340
  Trophy Points: 280
  Uandishi wa kishabiki - hawa ndio waandishi wetu siku hizi.
   
 6. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #6
  Aug 26, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  source please
   
 7. J

  John Marwa JF-Expert Member

  #7
  Aug 26, 2011
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 275
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Daaaaah! hii aibu kubwa kwa BAVICHA na CHADEMA jamani nashauri CHADEMA isiwaamini wanachama wake, ni lazima kufahamiana nani ni nani? historia yake? kazi? anaishi vipi na wapi? mienendo yake iko vipi? Kombati, uwezo wa kuandamana,.na kuonesha vidole viwili isiwe sababu ya kumuamini mtu! Kuna siku tutakuja patwa na makubwa zaidi ya hili.
   
 8. Fasta fasta

  Fasta fasta JF-Expert Member

  #8
  Aug 26, 2011
  Joined: Feb 15, 2011
  Messages: 620
  Likes Received: 114
  Trophy Points: 60
  Waandishi kuweni makini mnaweza ingia mkenge ikala kwenu. Huu mchezo wa kuchezea majina ya watu ukome. Chadema msiwachekee.
   
 9. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #9
  Aug 26, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Ni vigumu sana kuwachafua Chadema!
   
 10. mkolosai

  mkolosai JF-Expert Member

  #10
  Aug 26, 2011
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 1,148
  Likes Received: 638
  Trophy Points: 280
  Huyu mwandishi msameheni hajui atendalo.
   
 11. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #11
  Aug 26, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Kweli taaluma ya habari imevamiwa na vibaka. Yaani hata mwanacha naye ni kigogo! Taarifa yenyewe imejichanganya, heading inasema vigogo, huku anasema aliyekuwa, wapi na wapi.
   
 12. WAHEED SUDAY

  WAHEED SUDAY JF-Expert Member

  #12
  Aug 26, 2011
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 7,157
  Likes Received: 1,249
  Trophy Points: 280
  Duh! hata waandishi wa habari nao siku hizi masaburi on work, sasa sielewi wanataka kumchafua Lema au wanataka kuuza gazeti!
   
 13. Mlengo wa Kati

  Mlengo wa Kati JF-Expert Member

  #13
  Aug 26, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 2,733
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  tehetehetehe mmmmh! chadema ni chama makini???? aibu hii kwa wana magwanda!
   
 14. Janja PORI

  Janja PORI JF-Expert Member

  #14
  Aug 26, 2011
  Joined: Jul 31, 2011
  Messages: 808
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 45
  Huyu hajasoma hata ethics za journalist
   
 15. Khakha

  Khakha JF-Expert Member

  #15
  Aug 26, 2011
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 2,983
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Aargh. NANI KIGOGO HAPO? crap plus utumbo
   
 16. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #16
  Aug 26, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,640
  Likes Received: 4,747
  Trophy Points: 280
  Hivi CCM watajifunza lini kuwa kadiri wanavyojaribi kuichafua CDM siku zote inakula kwao?Jamani CCM imeshanuka watu wanaimini CDM kama mkombozi wao hivyo siasa hizo za maji taka wafanyiane wenyewe kwani hawana jipya.
   
 17. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #17
  Aug 26, 2011
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,183
  Likes Received: 1,183
  Trophy Points: 280
  Ukifaham kusoma na kuandika, ukawa na uwezo wa kununu kalam na karatasi wewe ni mwandishi wa habari tayari!.
   
 18. M

  Mchomamoto Senior Member

  #18
  Aug 26, 2011
  Joined: Aug 19, 2011
  Messages: 169
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ili kufika tunakokwenda najua kuna patashika nyingi. CHADEMA kazeni uzi tulieni, fanyeni mambo kwa busara naamini mtatutoa kwenye hili balaa. Jamani tuamini kuwa sisiemu sasa imefika omega hakuna lisilokuwa na mwisho.
   
 19. M

  Mchomamoto Senior Member

  #19
  Aug 26, 2011
  Joined: Aug 19, 2011
  Messages: 169
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Waandishi makanjanja ni wengi maana sasa kuna vyuo vya uandishi wa habari mpaka chooni hii ni hatari!!!!!!!
   
 20. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #20
  Aug 26, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Oh ni kweli sababu niliweka habari ya Lema kuwa polisi wanajua kuwa huyu jamaa hafanyi kazi kwake, lakini wanaweka habari hii kumuhusisha Lema just for political reason...

  Sababu kuu hii habari ni ya Leo cha kushangaza wanajua yote lakini Serikali ya CCM ndio inayoashiria hayo; Ina Maana wanaogoma yanayotolewa na Mh. Lema bungeni...

  Kuna Mwandishi wa habari wa Mwananchi huko Arusha ambaye aliandika sababu kuu ya Umafia wa CCM; wamemtumia Mama yake viongozi wa uhamiaji kuwa yeye sio Mtanzania...

  TUCHUNGE CCM inaanguka lakini inataka kuanguka na wengi...
   
Loading...