mbingunikwetu
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 13,664
- 18,040
Ajira za walimu ndo vizo zimeshatoka tayari na tunaipongeza serikali kwa kutoa ajira hizo. Vigezo vilivyotumika NAKUBALIANA NAVYO ila kwa bahati mbaya sana HAVIFUATWI kwa ukamilifu wake na nitatoa mifano.
Vigezo hivyo ni:
1. Mwaka wa kuhitimu ni kigezo cha kwanza.
2. Waliohitimu mwaka mmoja wanapangwa kwa kigezo cha umri. Kwa hiyo tulitegemea kuwa ISINGETOKEA aliyehitimu mwanzo asichaguliwe kisha akachaguliwa aliyehitimu baadaye KWA MASOMO HAYO HAYO KATIKA SHULE HIYO HIYO waliyoomba wote.
MFANO: Mtu mmoja ameniambia kuwa kuna walimu wawili walichagua shule moja kwa somo la biology. Mmoja alihitimu mwaka 2018 lakini hakuchaguliwa. Halafu akachaguliwa aliyehitimu mwaka 2020 kwa somo hilo hilo la biology. Shule hiyo iko Ifakara inaitwa Abubakar Asenga.
Kwa vigezo vilivyowekwa kama vingefuatwa lazima huyu aliyehitimu mwaka 2018 angechaguliwa maana ndiyo kigezo cha kwanza, hata kama huyu aliyehitimu 2020 angekuwa na umri mkubwa kuliko huyu wa 2018. Kilichofanyika ni sawa na kuipa timu uongozi kwenye ligi kwa kuwa imefunga magoli mengi lakini ina pointi chache.
Magoli yanahesabiwa tu BAADA ya kulingana POINTI na siyo kabla. Lakini pia kuna uwezekano mkubwa kuwa huenda hata umri wa huyo aliyehitimu mwaka 2020 ukawa mdogo kuliko yule aliyehitimu mwaka 2018 na akaachwa.
PENDEKEZO: Ili kukomesha kabisa tabia hii ya upendeleo inayoligawa taifa naomba IUNDWE TUME MAALUMU kufuatilia malalamiko na ipitie mchakato uliotumika ili HAKI ITENDEKE.
Ni vizuri waziri mwenye dhamana katika mchakato huu wa ajira za walimu akalifuatilia hili, na asipofanya hivyo MAMA aingilie kati.