Vigezo vya kuchagua walimu kwenye ajira ni VIZURI MNO lakini havifuatwi KIKAMILIFU

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
13,661
18,035
Ajira za walimu ndo vizo zimeshatoka tayari na tunaipongeza serikali kwa kutoa ajira hizo. Vigezo vilivyotumika NAKUBALIANA NAVYO ila kwa bahati mbaya sana HAVIFUATWI kwa ukamilifu wake na nitatoa mifano.
Vigezo hivyo ni:

1. Mwaka wa kuhitimu ni kigezo cha kwanza.

2. Waliohitimu mwaka mmoja wanapangwa kwa kigezo cha umri. Kwa hiyo tulitegemea kuwa ISINGETOKEA aliyehitimu mwanzo asichaguliwe kisha akachaguliwa aliyehitimu baadaye KWA MASOMO HAYO HAYO KATIKA SHULE HIYO HIYO waliyoomba wote.

MFANO: Mtu mmoja ameniambia kuwa kuna walimu wawili walichagua shule moja kwa somo la biology. Mmoja alihitimu mwaka 2018 lakini hakuchaguliwa. Halafu akachaguliwa aliyehitimu mwaka 2020 kwa somo hilo hilo la biology. Shule hiyo iko Ifakara inaitwa Abubakar Asenga.

Kwa vigezo vilivyowekwa kama vingefuatwa lazima huyu aliyehitimu mwaka 2018 angechaguliwa maana ndiyo kigezo cha kwanza, hata kama huyu aliyehitimu 2020 angekuwa na umri mkubwa kuliko huyu wa 2018. Kilichofanyika ni sawa na kuipa timu uongozi kwenye ligi kwa kuwa imefunga magoli mengi lakini ina pointi chache.

Magoli yanahesabiwa tu BAADA ya kulingana POINTI na siyo kabla. Lakini pia kuna uwezekano mkubwa kuwa huenda hata umri wa huyo aliyehitimu mwaka 2020 ukawa mdogo kuliko yule aliyehitimu mwaka 2018 na akaachwa.

PENDEKEZO: Ili kukomesha kabisa tabia hii ya upendeleo inayoligawa taifa naomba IUNDWE TUME MAALUMU kufuatilia malalamiko na ipitie mchakato uliotumika ili HAKI ITENDEKE.

Ni vizuri waziri mwenye dhamana katika mchakato huu wa ajira za walimu akalifuatilia hili, na asipofanya hivyo MAMA aingilie kati.
 
Mimi mbona naona wako Sawa mkuu.Yawezekana aliyehitimu mwaka 2020 ni mkubwa zaidi kiumri,kuliko aliyehitimu mwaka 2018.Ukumbuke kuajiriwa serikalini kuna age ikifika unakosa sifa.
 
Mimi mbona naona wako Sawa mkuu.Yawezekana aliyehitimu mwaka 2020 ni mkubwa zaidi kiumri,kuliko aliyehitimu mwaka 2018.Ukumbuke kuajiriwa serikalini kuna age ikifika unakosa sifa.
Lakini yawezekana huyo wa 2018 hakukidhi vigezo vya uombaji na huenda hakutuma viambata vyote vinavyo hitajika
 
Lakini yawezekana huyo wa 2018 hakukidhi vigezo vya uombaji na huenda hakutuma viambata vyote vinavyo hitajika
Viambatanisho vyote alikuwa navyo. Ndio maana naomba hiyo iwe case study kama kweli nia ya kutenda haki ipo.
 
Mimi mbona naona wako Sawa mkuu.Yawezekana aliyehitimu mwaka 2020 ni mkubwa zaidi kiumri,kuliko aliyehitimu mwaka 2018.Ukumbuke kuajiriwa serikalini kuna age ikifika unakosa sifa.
Kigezo cha kwanza ni mwaka wa kuhitimu kama ilivyo kwenye soka kigezo cha kwanza ni pointi. Ikitokea kigezo cha kwanza waombaji wakalingana (yaani wote walihitimu mwaka mmoja) ndipo kigezo cha pili cha umri ndipo kinapotumika kama kwenye soka ilivyo kigezo cha pili ni goal difference yaani tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa. Huwezi kutumia kigezo cha pili kabla ya kigezo cha kwanza. Nimewapa hiyo case ambayo mimi nimeifuatilia nikaona kabisa haki haikutendeka.
 
Kuondoa hayo malalamiko ningeshauri wawe wanamaliza miaka ya nyuma wanapomaliza wanaenda mbele kwakufuata mtiririko.
 
Mtu mmoja ameniambia kuwa kuna walimu wawili walichagua shule moja kwa somo la biology
Watanzania kwa hizi akili tutafika kweli.

Bahati ya mtu kama ipoipo tu.
Ukikosa mshukru Mungu mwambie akukumbuke wakati mwingine

Hakuna namana watu ni wengi nafasi ni chache.

Tuache lawama hili ni janga la dunia cha mhimu usikate tamaa..kesho ingia mtaani pambana.

Omba mkuu Mungu hatokuacha sawa
 
Back
Top Bottom