Vifo vya saratani vinasababishwa na tabia za kimaisha

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,502
9,282
Utafiti mpya umehitimisha kwamba maradhi ya saratani yanaweza kuzuilika kwa kudhibiti visababishi vya maradhi hayo kama matumizi ya tumbaku na pombe pamoja na uzito mkubwa wa mwili.

Utafiti huu ni kulingana na jarida la tiba la nchini Uingereza la Lancet. Utafiti huo umeongeza kuwa asilimia 44.4 ya vifo vilivyotokana na saratani kote ulimwenguni kwa mwaka 2019 vilichangiwa na tabia za watu.

Watafiti wamegundua tabia hatarishi 34, ambazo ni pamoja na uvutaji wa sigara, unywaji wa pombe na uzito mkubwa ambazo zinaongoza miongoni mwa tabia hizo.

Ripoti hiyo ilijikita katika tafiti zilizofanywa kwa watu milioni 10 waliokufa kwa aina 23 za saratani tangu mwaka 2019.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom