Gongo yatajwa kusababisha saratani ya tumbo

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,005
9,872
Utafiti mpya uliofanywa na wanasayansi wa shirika la kimataifa la utafiti wa saratani, IARC na wale kutoka Kenya, Tanzania na Malawi umebaini pombe kuwa kinywaji hatarishi na kichocheo cha saratani ya tumbo, ESCC, hususan miongoni mwa wanaume.

Ukiwa umechapishwa katika jarida la kitabibu ya Lancet, utafiti umetaja aina ya pombe kuwa ni zile kali za kisasa na zinazotengenezwa kienyeji kama vile gongo nchini Tanzania, Chang’aa nchini Kenya na Kachasu nchini Malawi.

Wanasayansi hao kutoka IARC, Chuo Kikuu cha Moi nchini Kenya, Taasisi ya utafiti wa Tiba Kilimanjaro nchini Tanzania na Chuo cha Tiba cha Malawi wamesema saratani ya tumbo inaweza kuzuilika kwa kuacha pombe hizo kali.

Mkuu wa utafiti huo Dkt. Valerie McComack kutoka IARC amesema “hadi sasa mchango wa unywaji pombe katika saratani ya tumbo katika ukanda wa Afrika Mashariki hauko bayana, miongoni mwa sababu ikiwa ni ugumu wa kutambua wigo wa vinywaji vya kienyeji na vya kisasa kwenye ukanda huo.”

Kwa mantiki hiyo anasema utafiti huo mpya unazingatia kwa mapana unywaji wa pombe za kienyeji na unaonesha Dhahiri mzigo wa saratani ya tumbo unaweza kupunguzwa Afrika Mashariki kwa kupunguza unywaji wa pombe.
Utafiti ulifanyika vipi?

Utafiti ulihusisha uchunguzi wa tabia za unywaji kwa watu 1279 waliokuwa wamelazwa hospitali wakiugua saratani ya tumbo na wengine 1346 wasiougua saratani ya tumbo, na ulifanyika Malawi, Kenya na Tanzania.

Kwa kina wahusika walichunguzwa aina za pombe za kienyeji walizotumia na kubaini viwango vyao vya unywaji kama ni cha juu au cha chini na wanakunywa mara ngapi kwa wiki na kwa kiasi gani.
Matokeo ya utafiti

Watafiti walibaini uhusiano wa kina kati ya hatari ya kupata saratani ya tumbo na unywaji wa pombe na hatari ilikuwa kubwa zaidi kwa wale wanaokunywa pombe kupindukia.

Hata hivyo wamesema utafiti zaidi unahitajika.

Mwaka 2020 saratani ya tumbo ilisababisha vifo vya watu 544,076 duniani kote.
Takwimu zinaonesha saratani hii ya tumbo ni nadra sana Afrika Magharibi ilhali imeshamiri Kusini na Mashariki mwa Afrika.

Kando ya pombe, sababu nyingine ni unywaji wa vitu vya moto kupindukia, matumizi ya tumbaku, na afya duni yam domo.

Mwaka 2020, kulikuwepona wagonjwa wapya 3000 wa saratani ya tumbo nchini Kenya, ilhali nchini Tanzania idadi ilikuwa 2,600 na Malawi 1800.
 
Dah!Mbona kinywaji "chetu" kinafanyiwa figisu sana?"Sisi" wanywaji huwa tunaidanganya gongo kwa kunywa supu ya ngozi ya ng'ombe.😂😂😂😂
 
Tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana...

Unatafiki kwa kuwapa watu wanye hiyo gongo...
 
ushindwe na ulegee ...
hata ukiisema vibaya bia yetu hautofanikiwa kuichafua
 
Back
Top Bottom