yash_ed
Senior Member
- Jan 9, 2020
- 142
- 381
Inasikitisha sana yale yaliyotokea kipindi MV Bukoba inazama leo hii ndiyo yale yale yaliyoikuta ndege yetu na kusababisha vifo visivyotarajiwa.
Sina uzoefu na ndege ila siku ya tukio sikuwa mbali na eneo husika, baada ya ndege kupata ajali eneo la mbele la ndege liliingia ndani ya maji na kubakiza mkia na eneo la kati vikiwa havijafikwa na maji.
Kilikuwa ni kitendo cha kuvutwa ile ndege na kusogezwa eneo lina kina kidogo ndiyo mlango ukafunguliwa.
Yakafanywa yale yale ya MV Bukoba, akatokea kijana wa hovyo asiye na maarifa akafungua mlango wa ndege na kusababisha abiria walokuwa ndani ya ndege na rubani wetu maskini wamejifunga mikanda ili kungoja taratibu za uokoaji, kijana wa hovyo akafungua mlango na kuingiza maji kwenye ndege.
Ndicho kilichofanya abiria hao 19 kufariki Dunia, ni jambo baya mno.