Vidonge vya mateja vimenifikirisha sana,

Vidonge vya mateja vimenifikirisha sana,

Alexido jz instagram

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2026
Posts
2,847
Reaction score
6,704
Nilikua mishemishe kukusanya oda za detergents huku na kule, ni kawaida kula chocho zote msako bako Kwa bako, nimeingia hapa mara nika wakuta mateja wamejaa, ni njiani tu hawana shida hao, sasa kilicho nifikirisha Teja Mmoja akatoka vidonge rangi ni kama kijani sijui rangi gani ile, lakini kavitoa Kwa Siri huku anaficha nikajiuliza kama ni vidonge vya kutibu Kwa Nini Teja avifiche? Na sizani kama ni cocaine ile no ni vidonge ila nadhani wanapata stimu, hofu kama ni vidonge kawaida Kwa nini aangalie huku na huku na kama ni drug je vinauzwa pharmacy? Na je pharmacy wanatambua Hilo? Mana Kuna mtu Alisha nambia wahuni huvuta Hadi petrol, nilishangaa sana, hivo muonekano ni vidonge kama vidonge na vina rangi na vimo kwenye kipacckage yake kama paracetamol ilivo wekwa ila vyenyewe ni vina rangi Fulani hivi, dah
 
Ndio mkuu ule muonekano ni vidonge kama vidonge yani tuseme kama fragil, ila rangi yake sikuimasta vizuri, vilikua vinatolewa Kwa kufichwa
Ni madawa hayo, isingekuwa madawa yasingefichwa. Halafu sisi huku kwetu usisahau tuko mbali na nchi zinazotengenezwa cocaine( Chile,Colombia ) na tuko jirani na nchi zinazotengenezwa heroine au bidhaa zinazofanania na heroine ambazo ziko Mashariki ya kati hapo. Kuna uwezekano hicho kidonge ni product inayofanania na heroine maana baadhi ya watumiaji wa heroine kabla ya kuanza kutumia unga,hupewa kwanza hivyo vidonge halafu wakiwa mateja sasa ndo wanapewa unga.
 
Back
Top Bottom