Video ya Rose muhando imeharibiwa na Director Jowzeey. Je, ni njama?

Ujinga mtupu

JF-Expert Member
Aug 16, 2017
851
1,887
.

Hivi imekuaje? Huyu jamaa anajiita Director Jowzeey kumharibia Malkia wa Muziki wa Injili Afrika Mashariki Rose Muhando na kumtolea video mbaya yenye giza na isiyo na mvuto.

Kuna sauti ya Rose Mhando inasambaa mtandaoni ambayo inaonyesha msanii wa nyimbo huyo akilalamika sana kwa uchungu akieleza jinsi gani walikesha usiku na mchana kuandaa video hiyo, na Director alilipwa hela yote lakini mwisho wa siku aliishia kutoa video mbaya sana ambapo kumeonekana kama kuna njama ambazo Director amefanya makusudi kwa msanii huyo.

Jowzeey hajaongea chochote mpaka sasa kuhusiana na tuhuma hizo.

 
Sasa mkubwa sisi video iliyoharibiwa hatujaiona, sauti inayosambaa mitandaoni hatujaisikia, Rose Muhando tunamsikia tu hatumjui, Jowzeey hatumjui kabisaaaaa tunapata wakati mgumu kweli yaani kuchangia

Basi tuonee huruma tuwekee hata video tu iliyoharibiwa
 
Back
Top Bottom